Afrika yaendelea kuitenga Kenya, makao makuu ya Banki ya Afrika yahamishiwa Kampala.

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Kama itakumbukwa vizuri, Kenya ilitumia nguvu nyingi sana kupigania kiti cha kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika(AU), Afrika ilikataa nakumuangusha mgombea wa Kenya, balozi Amina Mohammed.

Kama vile haitoshi, Kenya tena ikajitosa katika kinyang'anyiro ka kutaka makao makuu ya " Secretariat of African free trade area", lakini kwa vigezo vile vile vya kwamba Kenya ilisaliti nchi za Afrika katika kipindi cha ukombozi, Kenya ilikataliwa na badala yake HQ ikapelekwa Ghana.

Kuonyesha kwamba Africa bado ina machungu sana kwa kitendo cha Kenya cha kuisaliti Afrika, nchi za Africa zimeamua kuhamisha HQ ya benki ya Africa " Africa Export and Import Bank" (Afreximbank), toka Nairobi kwenda Kampala Uganda.

Wanasema "Mwenye kutenda ubaya husahau haraka sana, ila aliyetendewa ubaya ni vigumu sana kusahau".
 
Nafkiria ilipekwa kwa wakombozi...kumbe hata nynyi hamuaminiki
 
Nafkiria ilipekwa kwa wakombozi...kumbe hata nynyi hamuaminiki
Ulizia " Mulungushi club", huu ni umoja ulioundwa na Nyerere, Kaunda na Obote, ndio chimbuko la "Front line states" ambao baadae umegeuzwa kuwa SADC.
 
UPI number of stupidity=Joto la Jiwe.
 
Hamuaminiki...mtawateka wakuu...nynyi bakini na mapambio ya ukombozi tu...
Ulizia " Mulungushi club", huu ni umoja ulioundwa na Nyerere, Kaunda na Obote, ndio chimbuko la "Front line states" ambao baadae umegeuzwa kuwa SADC.
 
La kuvunda halina ubani.
Kenya uvundo wake ni mkali mno.
 
....Kenya ilisaliti nchi za Afrika katika kipindi cha ukombozi, Kenya....
Nasuburi utetezi wa kenye kwenye hili.
===
Hata hivyo nimefuatilia link iliyopo post number one ya uzi huu maelezo ni tofauti. Hiyo bank ndiyo iliomba kuweka makao yake kenya...lakini kenya wakafanya ucheleweshaji wa karibu miaka mitatu...hiyo benki ikaona isiwe tabu wakaenda Uganda. Hakuna sehemu yoyote ilipoandikwa Kenya ilihujumu ukombozi wa Afrika ndiyo maana imenyimwa furusa ya African Export-Import Bank
 
Ukisoma vizuri ni kwamba kulikua na mchuano wa wapi hiyo HQ ya hiyo Bank ipelekwe, katika hicho kipindi cha mnyukano, Bank kwa muda iliweka makao yake hapo Nairobi.

Baada ya mnyukano ndio ikaamua kuhamishia Uganda, japo wametoa sababu za kucheleweshwa kwa approvals, serikali ya Kenya ilishawapa uhakika kwamba kila kitu kimekamilika wasiondoke, kumbuka kuhamisha HQ ni gharama sana na ni jambo kubwa saba, ukiona wanefikia uamuzi wa kufunga ofisi pamoja na kuambiwa kila kitu kimeshakamilika, basi ujue kuna tatizo kubwa sana.

Hivi kwa akili yako unategemea hilo litasemwa hadharani kwamba kwasababu Kenya ilisaliti Afrika ndio sababu inakataliwa katika mambo Mengi ndani ya AU?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…