joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Pan-African lender dumps Nairobi for Kampala HQ
This deals a blow to Kenya as it denies Nairobi the benefits that come with hosting such top international organisations.
Kama itakumbukwa vizuri, Kenya ilitumia nguvu nyingi sana kupigania kiti cha kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika(AU), Afrika ilikataa nakumuangusha mgombea wa Kenya, balozi Amina Mohammed.
Kama vile haitoshi, Kenya tena ikajitosa katika kinyang'anyiro ka kutaka makao makuu ya " Secretariat of African free trade area", lakini kwa vigezo vile vile vya kwamba Kenya ilisaliti nchi za Afrika katika kipindi cha ukombozi, Kenya ilikataliwa na badala yake HQ ikapelekwa Ghana.
Kuonyesha kwamba Africa bado ina machungu sana kwa kitendo cha Kenya cha kuisaliti Afrika, nchi za Africa zimeamua kuhamisha HQ ya benki ya Africa " Africa Export and Import Bank" (Afreximbank), toka Nairobi kwenda Kampala Uganda.
Wanasema "Mwenye kutenda ubaya husahau haraka sana, ila aliyetendewa ubaya ni vigumu sana kusahau".