Afsa Elimu Rombo Asema Walemavu Hawana Umuhimu kwa Taifa!

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,423
Reaction score
3,297
Habari za muda huu.

Habari za kusikitisha kabisa ni kwamba mmoja wa wakaguzi wa ELIMU wilayani Rombo ametoa kauli chafu na ya kuudhi kama si kudhalilisha kwa kundi la Walemavu.

Mkaguzi huyo amesema ya kwamba WALEMAVU hawana UMUHIMU kwa taifa hili. Aliyasema hayo alipokuwa akikagua darasa la WALEMAVU lililojengwa na wafadhili.

Hatua hiyo imepelekea Walemavu wilayani humo kugomea darasa hilo kufuatia kukasirishwa na kauli hiyo ila wafadhili hao waliwafariji walemavu hao ya kwamba wako nao kwa kila jambo kwani kila mmoja wetu ni MLEMAVU MTARAJIWA.

Juhudi za kumpata Afsa Elimu Wilaya kuzungumzia kadhia hiyo zinaendelea.

Source: ITV HABARI ZA MCHANA

Hivi huu ubaguzi unaolelewa taratibu hapa nchini dhidi ya baadhi ya makundi katika jamii kwa nini wanaobainika kuwatenga na kuwadharau wengine wasichukuliwe hatua kali ili iwe mfano kwa wengine?
 
Tunao wengi viongozi wa namna hiyo sijuhi wanafika je kwenye ngazi hizo. Tusimuhukumu kwanza labda tusikie kutoka upande wake anasema je!
 
atakuwa na laana...
na huyo kizazi chake chote atarajie kupata walemavu tupu....
 
Vichaa hadi Ma-Afisa Elimu sijui hapo tutegemee watoto wetu wataelimika au?
 
na 90% ya CCM ni vichaa....
kuna mmoja huko Lushoto eti ni mkuu wa wilaya, ana miaka 29, hivyo vituko anavyovifanya huko ni aibu kwa Ikulu iliyomtuma...

Mkuu haya madhara ni matokeo ya kipindi cha Mungai. Hesabu alichanganya na kiswahili liwe somo moja na sayansi akachanganya na Uraia matokeo maafisa Elimu wakapata mshituko wa Ubongo.
 
Wakati Mzee Mengi akitumia hela zake nyingi kuwakwamua walemavu Wale wanaokula kodi yetu ndiyo wanarudisha maendeleo nyuma kwa kauli zao.
 
Sitaki kwanza kuamini hii habari,Mungu amsamehe huyo mtoa kauli
 
Katika makundi ambayo nchi yetu haiwatendei haki ni pamoja na walemavu.niliwahi kusikia kuwa walemavu tanzania ni asilimia kumi.fikiria ,kwa mfano serikali ikiamua kuanzisha `tax free zone` kwa ajili ya walemavu.walemavu wangapi watatoka mitaani na kuongeza pato la taifa .lakini hakuna anayojali.............tukiwa ofisini tunawanyanyasa wastaafu kama vile sisi hatutastaafutunawasahau ,walemavu kama vile sisi sio walemavu watarajiwa.............
 
Huyu atakuwa Mmasai (no offense intended), maana nasikia wamasai huwa wanawa "nonino" walemavu ndiyo maana huwezi kuona masai mlemavu!
 
Wizara ya njisia na watoto!imchukulie hatua!kali liwe onyo na kwa viongozi wengine!
 
Hizo ni kauli za Magamba tumezizoea ,kutukana na kudhalilisha ndo jadi yao
 
viongozi wetu wa kipindi hiki wengi wao ni walemavu! kwa vile hawajaenda hospitali kupimwa akili tu,lkn ni walemavu wa akili
 
Kama ametamka hayo kweli nae anaulemavu wa ubongo.
 
Watu kama hawafai kabisa kupewa dhamana yeyote, maana hata hamwogopi Mungu wake. Hata hajui methali isemayo hujafa hujaumbika.
Wakati Mzee Mengi akitumia hela zake nyingi kuwakwamua walemavu Wale wanaokula kodi yetu ndiyo wanarudisha maendeleo nyuma kwa kauli zao.
 
Ni kauli ambayo haifai kutolewa na kiongozi kama yeye, hivi jina lake nani, hafai hatakuongoza familia yake, kama anayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…