Afsa Elimu Rombo Asema Walemavu Hawana Umuhimu kwa Taifa!

Afsa Elimu Rombo Asema Walemavu Hawana Umuhimu kwa Taifa!

Habari za muda huu.

Habari za kusikitisha kabisa ni kwamba mmoja wa wakaguzi wa ELIMU wilayani Rombo ametoa kauli chafu na ya kuudhi kama si kudhalilisha kwa kundi la Walemavu.

Mkaguzi huyo amesema ya kwamba WALEMAVU hawana UMUHIMU kwa taifa hili. Aliyasema hayo alipokuwa akikagua darasa la WALEMAVU lililojengwa na wafadhili.

Hatua hiyo imepelekea Walemavu wilayani humo kugomea darasa hilo kufuatia kukasirishwa na kauli hiyo ila wafadhili hao waliwafariji walemavu hao ya kwamba wako nao kwa kila jambo kwani kila mmoja wetu ni MLEMAVU MTARAJIWA.

Juhudi za kumpata Afsa Elimu Wilaya kuzungumzia kadhia hiyo zinaendelea.

Source: ITV HABARI ZA MCHANA

Hivi huu ubaguzi unaolelewa taratibu hapa nchini dhidi ya baadhi ya makundi katika jamii kwa nini wanaobainika kuwatenga na kuwadharau wengine wasichukuliwe hatua kali ili iwe mfano kwa wengine?

Kuna mijitu sijui ilitakiwa izaliwe ni NGIRI??? Ana confirmed contract gani na MUUMBA WAKE kuwa akitoka hapo Landcruiser yake kamwe haitopata ajali na yeye kupoteza moja ya viongo vyake?? Kwa kila binadamu, kipindi chetu chote cha maisha ni MLEMAVU MTARAJIWA. Lolote laweza kutokea muda wowote na kukuachia kilema hadi kufa kwako!!!!
 
Ni kauli ambayo haifai kutolewa na kiongozi kama yeye, hivi jina lake nani, hafai hatakuongoza familia yake, kama anayo.

Hata kama ana familia mshenzi huyu atakuwa anafakamia hadi chakula cha watoto!! Nyambafu kabisa huyu jamaa!!!
 
Ina maana hata umuhimu wa babu hauoni.Kweli huyu balaa
 
Wamwulize Mudhihir! Nani alijua atakujapoteza mkono? Huyo Afisa Elimu aende akapate kitubio. Hajawatendea haki ndugu zetu wenye ulemavu! Kabla hajafa lazima naye auonje ulemavu huyu!
 
Ni kauli ambayo haifai kutolewa na kiongozi kama yeye, hivi jina lake nani, hafai hatakuongoza familia yake, kama anayo.

Jamani huyo atakuwa ni kichaa tu!! kama sio kichaa basi ana mapepo na ni mchawi mkuu!!
 
Dawa yake ni kumkata miguu yote na mikono alafu kumuuliza je ni muhimu na yeye kuendelea kuwepo au? Inasikitisha sana kuwa na watu wa aina hii na wanaachiwa tu hivihivi..aaaaagh!
 
Back
Top Bottom