Afumaniwa sasa anajutia na hana solution

Afumaniwa sasa anajutia na hana solution

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,261
Reaction score
9,733
Kuna rafiki yangu nasoma naye chuo wote tuko mwaka wa mwisho chuo flan hapa dodoma.
Sasa kuna kijana flan ni askari polisi wanafahamiana kwa kuwa wote wametokea musoma, hivyo basi jamaa uwa anaishi kwa huyo askari. Pale kwa askari anaishi kwenye nyumba za polisi na pale anaishi na wadogo zake wawili wa kike, mmoja yuko form 2 na mwingine form 4.
Sasa yule askari alikuwa akimchukulia huyu rafiki yangu kama ndugu yake na akadhan kuwa naye atawachukulia wadogo zake kama wadogo wake pia lakini kumbe ni tofauti.
Huyo askari anajiendeleza kimasomo hivyo basi mchana anakuwa masomon na shift zake ni za usiku tu. Bas kwake uwa anabaki huyu rafk yangu na wale watoto wa kike wawili.
Sasa yeye uwa ana mahusiano ya kimapenzi na yule wa form 4 na uwa ana do naye kila mara.
Nakumbuka siku ya kwanza kujua uhusiano wao, ilikuwa mwaka jana ambapo huyu rafiki yangu aliniambia kuwa kamtwisha mimba yule binti na akawa ana hofu sana.
Kusema kweli nilishangaa sana, na nikamuuliza hivi haoni kuwa ni hatari sana mtu kamwamini anakula bure kwake, jamaa ni askari anahangaika kuwasomesha wadogo zake na kuwatunza wazazi wake yeye anataka kuwaharibia maisha wadogo zake?
Jamaa akasema ooh sijui bahati mbaya lakini mwisho wa siku hiyo mimba waliitoa.
Uhusiano ukaendelea kama kawaida na kila siku nlikuwa namwambia za mwizi arobaini ipo siku atafumaniwa na ndiyo atajua kuwa usaliti mbaya.
Sasa ilikuwa jumatano wiki hii, askari kaingia lindo jamaa kama kawaida chumbani na binti mara mlango ukafunguliwa jamaa kumbe alisahau koti, ile anaingia chumbani akapishana na mdogo wake anatoka mbio akiwa uchi wa mnyama anakimbilia chumbani kwake mara akaingia chumbani akamkuta rafiki yangu akiwa kavaa condom ameppigwa butwaa.
Askari akachukua koti akatoka nje, rafiki yangu kahisi kifo maana kuna siku katika story askari aliwahi mwambia eti siku akimkuta mdogo wake kaleta bwana ndani kama ana bunduki atampiga risasi.
Ilikuwa usiku kama wa saa 6 rafiki yangu akavaa haraka akakimbia akaenda lala guest kesho yake ndiyo akarudi chuo.
Nguo zake, laptop na vitu vyote kaviacha nyumbani kwa askari na anaogopa kurudi.
Jana yule binti akiwa shule alimpgia rafiki yangu akamwambia amepigwa sana na amesema mambo yote.
Jamaa anahaha hapa na mbaya zaidi nyumbani kwao ana mchumba tayari.
Ama kweli za mwizi arobaini eti anaomva nimfuatie vitu vyake.

Nimemwambia mimi bado nahitaji kuishi sitaki pigwa maana wakurya wana hasira hakawii kumaliza hasira zake kwangu.
 
nikielewa "aolution" nitarudi kuisoma habari yote...nakamchango nitatoa
 
Wewe huoni hata aibu kusema huyo rafiki yako, mimi ningeisha mkwepa kabisa mtu kama huyo na asinge kuwa tena rafiki yangu.

Rafiki gani hana utu, anakula bure analala bure kwa mtu amabye kamuona kama ndugu yake, halafu umeona kafanya nini kwa mtu amabye alimfanya kama ndugu yake.

Achana naye huyo b@wege wala usiseme tena rafiki yako, mwisho na wewe utaonekana uko same type kama yeye.
 
mi nafikiri dogo alikuwa na maana ya solution na sio aolution. Si unaona a key ikokarinu na s key! Dogo kuwa mwangalifu huu ni mwaka wa mwisho ujue!
 
Mzinifu mkubwa huyu mshenzi! Mana mi ningeelewa kama angekuwa na future na huyo binti haijalishi ni mdogo wa rafiki yake! Lakini mara ana mchumba kijijini halafu limekimbia halisemi chichote kwa mwenzie kwamba ntamuoa tusome tumalize mjinga kwelikwelivna muharibifu!
 
Unapofanya jambo kama hilo lazima ujue kunasiku kitanuka, sasa cha muhimu, kama ulivyo sema kuwa afande bado kijana mdogo sana, tafuta mzee yeyote unaejua kuwa wanaheshimiana sana na jamaa, kisha mueleze kila kitu, yeye atakushauri nini cha kufanya, wewe na huyo mzee mnaweza pamoja mkaenda kwa jamaa na kuomba msamaha, ila ujue huo undugu wenu fake ndo kwisha kabisa.
 
Huyo jamaa muache aliface peke yake. Tena angefunguliwa kesi ndo ingenoga zaidi!!
 
Huyo askari nae kiazi kweli.....
Unamwamini kijana kiasi hicho?

 
Then na sisi tuje tukapige mtungo ama msaada upi kutoka jf??
Vidume kazi kwenu
 
Huyo askari ni mstaarab sana mwambie huyo rafiki yako atafute namna yoyote akamwombe msamaha. OGOPA UNAMFANYIA MTU UBAYA WOTE HUO HALAFU HAKUULIZI CHOCHOTE
 
Ushauri wa bure,
Huyo mpuuzi asamehe kila kitu alichoacha kwa huyo polisi. Kwa upumbavu kama huo wala msiende kumtafuta mzee wa kuwasindikiza. Mtaanzaje kumweleza mzee mwenye busara zake upuuzi huo,halafu unasema mko chuo, sasa huko mnasoma nini?

Hilo ni lake na alibebe mwenyewe, ila msisogee wala kupita mitaa anayoishi huyo polisi.
 
Back
Top Bottom