Afungwa jela maisha kwa kubaka Mtoto wa miaka mitatu

Afungwa jela maisha kwa kubaka Mtoto wa miaka mitatu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, imemhukumu John Sanare (23), Mkazi wa Kimnyaki wilayani hapo kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kubaka kichanga cha miaka mitatu na miezi miwili.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Gwantwa Mwankuwa, aliyekuwa akisikiliza shauri hilo.

Akisoma mwenendo wa kesi hiyo, Hakimu Mwankuwa alisema mshtakiwa Sanare ametiwa hatiani kwa kutenda makosa mawili ambayo ni ya ukatili dhidi ya mtoto na ubakaji.

“Mahakama hii imejiridhisha kuwa upande wa mashtaka umefanikiwa kuijenga kesi hii na ushahidi uliotolewa haujaacha shaka yoyote.

“Kwa kuwa mahakama imejiridhisha kuhusu makosa haya, inatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa wote wanaotenda ukatili kwa watoto katika jamii,” alisema Hakimu Mwankuwa.

Makosa hayo ni kinyume cha kifungu cha 130 (1) 2 (e) na kifungu cha 131 (3) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16.

Katika hati ya mashtaka, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwanasheria wa Serikali, Penina Ngolea, kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 10, 2022 katika Kijiji cha Kimnyaki, wilaya ya Arumeru.

Nje ya Mahakama hiyo, wanaharakati wanaoongoza vita dhidi ya ukatili wa kijinsia, akiwamo Ofisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi, walieleza furaha yao baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani mshtakiwa na kumpa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.

“Pia tunapenda kutoa shukrani kwa jamii ambayo ililiibua suala hili na kulifikisha katika vyombo husika vikiwamo hospitali, polisi na mahakamani na leo (jana), hukumu imetoka,” alisema.

Pia Ofisa wa Kitengo cha Kutetea Haki ya Mtoto kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Farida Masenika, alidai kuwa kwa sasa mwelekeo si mzuri ingawa alisema serikali iko macho kupambana na wote wanaofanya vitendo hivyo vya ubakaji wa watoto.

Alisema pia mahakama hivi sasa inafanyakazi kwa haraka, kwa kuwa kesi hyo imeendeshwa kwa miezi mitano pekee na haki imetendeka.

NIPASHE
 
Tatizo masingizio ni mengi kama kweli kabaka mtoto wa miaka 3 uyo sio wa kufunga naye abakwe na waty watatu kulingana na miaka ya mtoto akitoka apo atajinyonga mwenyewe
 
Raia kama hawa wangekuwa wanafungwa jela maalumu ya wao pia kupigwa pipe tu kila siku...
 
Serikali ibadilishe adhabu

Inatakiwa hawa watu wapelekwe kufanya kazi ngumu.

Pia ndugu jamaa na marafiki tusipoteze muda kuendesha au kufatilia kesi kama hizi.
Hizi kesi twatakiwa tuzimalize kwa kuwalaza wahusika kabla hawajaenda polisi
 
Back
Top Bottom