Afungwa jela maisha kwa kumnajisi mtoto wa miaka 7

Afungwa jela maisha kwa kumnajisi mtoto wa miaka 7

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha jela Mwalimu Johnwell Mwamboya (38) mkazi wa Iyela jijini Mbeya baada ya kupatikana na kosa la ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka saba.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Tedy Mlimba mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Wakili Julieth Katabaro wakati akisoma maamuzi ya kesi ya jinai namba 50/2023 iliyokuwa ikimkabili Mwalimu huyo

Mahakama imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi nane (8) wa upande wa mashtaka akiwemo mtoto aliyefanyiwa kitendo cha ubakaji mara kadhaa na mtu huyo, daktari aliyemchunguza mtoto huyo na jirani aliyegundua mtoto huyo kunajisiwa

Mahakama imesikiliza kwa umakini ushahidi wa Jamhuri na ule wa utetezi kupitia mashahidi wake wawili na kujiridhisha bila kuacha shaka kwamba mtu huyo alimbaka mtoto huyo wa darasa la pili kwani hata wakati wa uwasilishwaji ushahidi mhathirika wa tukio hilo ambaye ni mtoto (7) alimtaja na kumtambua mbele ya Mahakama mshtakiwa aliyetajwa kwa jina maarufu la Mwalimu Jofu licha ya kwamba yeye alikuwa akikana kutenda jinai hiyo

Mahakama imesema Jamhuri imethibitisha shauri hilo bila kuacha shaka hivyo kumtia hatiani kwa kosa hilo

Akizungumza kabla ya hukumu kutolewa, Mwendesha mashtaka wa serikali Wakili Julieth Katabaro aliiomba Mahakama kutoa adhabu kama sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na watu wengine katika jamii kutokana na kuendelea kushuhudiwa kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti hasa kwa watoto na wanawake miongoni mwa jamii ikiwemo kwa wanaoendekeza imani za kushirikina

Ndipo Mahakama ikamhukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela Mwalimu Mwamboya (38) huku ikiweka wazi haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 tangu kutolewa kwa hukumu hiyo

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mwalimu Johnwell Edward Mwamboya (38) Mkazi wa Iyela jijini Mbeya alikuwa akidaiwa kwamba katika tarehe tofauti kati ya Januari na Februari 2023 alikuwa akimlaghai mtoto huyo kwa pipi na biscuit na kumbaka akiwa kwenye shule yake ya watoto wadogo ambayo ni jirani na familia ya mhathirika huku ikielezwa kuwa Mwalimu huyo alikuwa akimtishia kutosema nje ya hapo atamuuwa kosa ambalo ni kinyume na kifungu namba 130 (1) (2) (e) na 131 (1) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ilitofanyiwa marekebisho mwaka 2022 madai ambayo hata hivyo yameelezwa kuthibitika bila kuacha shaka mbele ya Mahakama.

Source - JamboTv
 
Back
Top Bottom