SoC03 Afya bora kwa chachu ya maendeleo

SoC03 Afya bora kwa chachu ya maendeleo

Stories of Change - 2023 Competition

My beginning

Member
Joined
May 31, 2023
Posts
11
Reaction score
8
Nini maana ya afya?

Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na maradhi au ugonjwa wowote.
Afya bora hutokea pale ambapo binadamu anafuata taratibu zote za afya Kwa usahihi.

Kusudi binadamu awe na afya njema na bora ni lazima kufahamu mambo makuu manne ambayo ni;

1. Mlo kamili au lishe kamili
Lishe hii imejengwa na nafaka kamili kama vitu visivyo kobolewa, matunda ya aina mbalimbali, mboga mboga za aina mabalimbali, protini, mafuta na sukari.

2. Kupumzika
Hapa tunashauriwa kupata pumziko Kwa masaa sita mpaka nane Kwa ajili ya kuupa ubongo nafasi ya kuchambua mambo Kwa usahihi na Kwa kina.

3. Mazoezi
Kama binadamu wenye afya njema inatupasa kufanya mazoezi Kila siku Kwa ajili ya afya bora.

4. Hewa safi
Uwepo wa hewa safi na salama hufanya tujisikie vizuri na kuzalisha hisia chanya katika akili zetu.

Zifuatazo ni faida za kuwa na afya bora;

Afya bora huondoa uchovu kimwili na kiakili

Hii itafanya mtu kuwa mwepesi kimwili na kiakili Kwa Sababu ya mlo kamili au lishe kamili anayopata, hivyo itamfanya kuwa mwepesi na kuchangamsha akili ili kusudi afanye kazi Kwa kiwango kikubwa cha utendaji.

Afya bora huongeza damu na kuimarisha Kinga ya mwili
Hii utokea hasa kwenye ulaji mwingi wa mboga mboga na matunda Kwa wingi, hutokea mtu anapofanya mazoezi mara Kwa mara hii husaidia kufanya mzunguko wa damu kuwa vizuri zaidi na kupelekea kuimarisha Kinga ya mwili.

Afya bora husaidia kusawazisha homoni mwilini
Utekelezaji na ulaji wa mlo kamili husaidia kusawazisha homoni mwilini na kupambana na changamoto za homoni kama vile kushuka Kwa Kinga mwilini, kutoshika ujauzito Kwa muda mrefu, ujauzito kuharibika mara Kwa mara na kuziba Kwa mirija ya uzazi.

Afya bora husaidia uhifadhi wa kumbukumbu
Kupumzika Kwa muda unaofaa itasaidia kuhifadhi kumbukumbu za muda mrefu kuhusiana na kitu fulani. Hii itasaidia utunzaji wa vitu vidogo vidogo amabavyo ni muhimu kabisa, ubongo utachukua taarifa na kupeleka sehemu ya hifadhi ya kumbukumbu na hii itafanya kuwa mwepesi kupata kumbukumbu kuhusiana na kitu fulani.

Afya bora hupambanana magonjwa mbalimbali
Ulaji mzuri wenye lishe ndani yake husaidia kupambana na magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu, kisukari, chemba moyo na unene uliopitiliza.

Afya bora huzalisha hisia chanya na kuleta uso wenye furaha na kuondoa msongo wa mawazo
Afya njema na bora huleta hisia chanya Sababu ya kujisikia vizuri, hewa safi na hali ya mazoezi mara Kwa mara,Hii pia huondoa msongo wa mawazo na kumfanya mtu ajisikie vizuri muda wote kitendo ambacho kinapelekea mtu huyo afanye kazi Kwa ufanisi mkubwa na kiwango cha hali ya juu Kwa sababu ya kutokuwa na msongo wa mawazo.

Afya bora huleta umakini katika kazi
Ulaji mzuri wa chakula, kupumzika, mazoezi na hali safi ya hewa huleta ubora, umakini na ufanisi katika utendaji wa kazi. Hii hutokea pale ambapo mtu anafuata taratibu zote za afya Kwa usahihi. Hii itafanya kuwa na hali ya kujiamini Kwa viwango vyote vya kazi.

Afya bora husaidia kudumisha kusambaa vizuri Kwa virutubisho mwilini na kuleta afya mwilini.
Hali hii itasaidia mfumo wa mmngenyo wa chakula kufanya kazi Kwa ufanisi mkubwa na itapelekea afya ya mwili kuimarika.

Zifuatazo ni hasara au madhara yanayosababishwa na ukosefu wa afya bora;

Uchovu wa kimwili na kiakili.
Kutokana na ulaji mbovu wa chakula, kutofanya mazoezi, muda mchache wa kupumzika hupelekea uchovu wa kimwili na kiakili. Hii ni kwasababu ya afya ya ubongo inakuwa haina virutubisho vya kutosha vya kufanya kazi kikamilifu. Ulaji mbaya wa chakula hufanya afya ya ubongo na akili kulemaa na kushindwa kufanya kazi Kwa viwango vya juu na Kwa umakini mkubwa katika sekta fulani au kazi fulani.

Msawazisho mbovu wa homoni mwilini.
Ukosefu wa afya bora hupelekea msawazisho mbovu wa homoni mwilini, Hali ambayo hupelekea mvurugiko wa homoni. Baadhi ya dalili za mvurugiko wa homoni ni kama vile uchovu, kukosa usingizi, homa za usiku na kizunguzungu cha mara Kwa mara, ongezeko la tumbo na nyama zembe, maumivu ya viungo, maumivu wakati wa tendo la ndoa. Hivyo mvurugiko wa homoni mwilini huweza kuleta madhara mbalimbali kama vile kutoshika ujauzito Kwa muda mrefu, ujauzito kuharibika mara Kwa mara, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kuzeeka mapema, kuziba Kwa mirija ya uzazi na kutokea Kwa saratani ya kizazi.

Uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa mbalimbali
Ukosefu wa afya bora hupelekea maambukizi mbalimbali ya magonjwa na mwisho wa siku hupelekea vifo vingi na kupunguza utendaji mzuri wa kazi Kwa jamii na taifa Kwa ujumla. Baadhi ya magonjwa yanayoweza kutokea baada ya ukosefu wa afya bora ni kama vile shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo, kisukari, unene uliopitiliza na saratani.

Utendaji mbovu wa kazi
Hali hii ya ukosefu wa afya bora huondoa umakini mkubwa, umaridadi na utendaji mzuri wa kazi kwa sababu mwili unakuwa tayari umechoka na afya ya ubongo imelemaa hivyo humuondolea mtu ufanisi mkubwa kazini na kufanya kazi Kwa viwango vya chini.

Mwili dhaifu usio na uimara
Hii ni Kwa Sababu mtu anakosa virutubisho muhimu mwilini na akilini hali inayopelekea kudhoofika Kwa mwili na kushindwa kufanya kazi sawa sawa na Kwa viwango vya juu,pia kuwa na urahisi wa kukumbana na maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na upungufu wa Kinga mwilini.

Kama binadamu, watu wenye malengo, ndoto, maono na chachu ya maendeleo ya mafanikio Kwa jamii na taifa Kwa ujumla, tunapaswa kuzingatia kanuni bora za afya na suala Zima la ulaji wa mlo kamili katika harakati za kupambania na kuleta chachu ya maendeleo kwenye sekta fulani.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom