Dr Wilson255
Member
- Aug 23, 2022
- 7
- 6
UTANGULIZI:
AFYA:Ni hali kujisikia vizuri kimwili,kiakili,kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote. Afya ya binadamu itakua njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya.Afya inajumuisha mambo yafuatayo.
1. Chakula chenye virutubisho vyote vikiwemo protini,wanga,na mafuta(hiyo iwe katika asilimia kidogo sana).
2. Kuwa msafi wa mwili na mazingira yako,kama vile(kuoga na kusafisha mazingira yanayokuzunguka)
3. Mandhari yenye hewa safi husaidia katika kuhifadhi afya ya binadamu katika mwili na akili,mazingira wakati wote huchukuliwa kama jambo muhimu sana katika hali ya afya ya binadamu,hii humanisha mazingira ya asili, mazingira ya kujengwa na mazingira ya kijamii.Mfano wa vitu kama vile maji safi,hewa safi,makazi salama, huchangia afya nzuri hasa kwa afya za Watoto wachanga na Watoto.Utafiti mwingine unaonyesha kua ukosefu wa maeneoya burudani husababisha kupungua kwa afya na ustawi.4.Kwa mana ingine afya pia ni”hali ya mtu kutosumbuliwa na maumivu na udhaifu,Pamoja na uwezowa kutumia sehemuzote za mwili.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA KUJENGA AFYA IMARA KATIKA TAIFA.
1. Serikali inatakiwa kuandaa wataalamu wa mambo ya afya na kujenga hospitali nyingi hata vijijini kwasababu watu wengi hupoteza Maisha kwa kukosa huduma za afya,hii itasaidia kupunguza vifo na hasa Zaidi kwa Watoto wadogo na wachanga ambao ndio taifa la kesho,lakini pia itasaidia kutunza afya za wazee ambao kulingana na umri wao kinga zao za mwili zinaweza kushuka na kuwa rahisi kushambuliwa na magonjwa, itasaidia sana serikali kujenga hospitali nyingi sana mpaka vijijini kutunza afya za nguvu kazi kwenye jamii ili pia kuongeza uzalishaji katika taifa.
2. Watu wanatakiwa kua na ustadi wa kufanya mazoezi kwa wingi.Hata mjamzito anapaswa kufanya mazoezi,ingawa si kazi ngumu.
3. KUHUSU BIMA YA AFYA; Serikali Kuhakikisha kila mwananchi anakua na BIMA afya ambayo anaweza kupata matibabu hospitali yoyote ndani ya nchi,serikali inaweza kuweka makato kulingana na kipato cha kila mtanzania,pia serikali inaweza kutunga sheria mfano ya kila mtanzania kuchangia shillingi 500 kwa kila wiki kwenye bidhaa inayonunuliwa na mtu yoyote ndani ya nchi na pesa yote hiyo iwe inakwenda kwa ajili ya kulipia mfuko wa BIMA ya afya wa taifa ili mfuko uweze kua na uwezo wa kuendelea kuhudumia watanzania wote kwa usawa.
Mfano kwa makadirio ya sasa Tanzania inaweza kua na watu 60,000,000 na kila mtanzania akichangia 500 sawa na shilingi sawa na shilingi bilioni 30,000,000,000/= kwa wiki,kwa mwaka mzima ni sawa na trilioni 1 na bilioni 560,000,000,000/= Kiasi hiki cha pesa kila mwaka kinaweza saidia kuhakikisha kila mtanzania anakua na BIMA ya afya itakayoweza kumsaidia apate matibabu bure na kufanya vipimo vidogo na vikubwa vya afya.
Mfano wapo ndugu zetu watanzania kwa bahati mbaya hupata matatizo ya magonjwa kama vile figo kufeli na kushindwa kufanya kazi hivyo itawahitaji wafanye kusafisha figo ambayo hugharimu karibu laki nane kila wiki na itamtaka afanye kwa Maisha yake yote, kwa wenye kushindwa kugharamia basi hupoteza Maisha yao na kufariki dunia,kama serikali itafanikiwa kufanya hivyo na kusaidia kila mtanzania kua na bima ya afya basi watanzania Zaidi ya milioni moja tutawaokoa kila mwaka na kuwaepusha na vifo.
MALENGO NA MIPANGO BORA YA MAENDELEO ENDELEVU KWA WATOTO WACHANGA HASA KATIKA UKUAJI WAO NA UCHUMI PIA.
1. Sera bora kwa familia.Mabadiliko kwenye maeneo ya kufanyia kazi yanahitaji sera kama vile likizo zinazolipwa kwa mzazi,manufaa ya kifedha,muda kwa kunyonyesha. Hakuna wakati ulio muhimu Zaidi kwa Maisha ya mtoto kama miaka yao ya kwanza utotoni,ndio mana tunaishauri serikali na biashara wawekeze kwenye sera ambazo haziinuia tu ukuaji wenye afya bali pia kujenga uhusiano mzuri kati ya wazazi na Watoto wao kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii.
LIKIZO ZA KULEA ZILIZO NA MALIPO.
Takriban miezi sita inayolipwa kwa wazazi wote kati ya hiyo wiki 18 zinazolipwa zitengewe mama.serikalina biashara zinastahili kujikakamua hadi miezi 12 kwa Pamoja ya likizo inayolipwa.Ikiwa serikali itaamua kulipa kwa mama anapokua likizo ya kulea ina uhusiano mkubwa sana kua asilimia kubwa sana ya vifo kwa Watoto itapungua, pia itasaidia sana kupunguza kutelekeza Watoto hasa kwa wanawake wasio katika ndoa au mabwana.
Kuwepo kwa mazingira mazuri kunyonyesha na kukamua maziwa,uwepo wa vifaa bora huwawezesha akina mama kuendelea kunyonyesha Watoto hata baada ya kurudi kazini.Tukumbuke afya ndio msingi IMARA wa shughuli zako zote za Kila siku,bila afya Bora,IMARA ni vigumu sana kufikia malengo yako.
NINA IMANI UMEWEZA KUJIFUNZA JAMBO KUBWA NA NZURI KATIKA MAKALA HII NILIYOIANDAA,NAOMBA NIPIGIE KURA YAKO NIWEZE KUSHINDA.

Upvote
2