Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 11,462
- 21,124
Kumekuwapo na uivishaji wa ndizi kwenye makontena ya umeme Dar es Salaam.
Sifa ya ndizi hizi ni kwamba zina rangi nzuri, tamu ila hazina harufu sana kama ndizi za kuzalisha kienyeji.
Mchakato wa uzalishaji ndiyo unanipa mashaka.
Kwanza, ndizi hukatwa chane na kuchovywa kwenye maji yanayosemekana yana dawa. Kuna kibarua amewahi kulalamika kwamba maji yale yanawasha.
Basi wakishazichovya kwenye maji haya ya 'dawa' basi hupangwa kwenye kreti za mbao kama zile za kubebea nyanya,, kisha hupangwa kwenye kontena la umeme.
Siku ya kwanza hafunguliwa hali ya ubaridi. Lengo ni kushusha joto la ndizi ili liwe sawa sawa kwa ndizi zote.
Siku ya pili, hupandishwa hali ya joto ili kuivisha.
Siku ya tatu hupigwa baridi ili zitoe rangi.
Siku ya nne hupigwa joto tena. Zikiwa tayari, hupigwa baridi ili kuzuia zisiendelee zaidi kuiva, na hapa huwa tayari kwenda kuuzwa.
Swali langu lipo kwenye ubora na usalama wa ndizi hizi kwa afya haswa ukizingatia dawa inayodaiwa kutumiwa katika mchakato mzima.