Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
1. Utangulizi
Tuko katika kizazi chenye kudhani kuwa kuishi vizuri ni kuwa na fedha. Fedha inaonekana ni kila kitu. Tunadhani kuwa ni fedha ndizo hutufanya tununue nyumba, gari, nguo, chakula na maisha mazuri kwa ujumla, na wengine kwenda mbali zaidi na kupata jeuri ya kujiona wanaweza hata kununua watu na utu wao, madhali wana fedha. Kwa mtazamo huo wengi tumepotoka na kuona fedha ni chanzo au mtaji wa chochote kile anachokihitaji mtu. Si kweli kabisa, huo ni udhaifu wetu mkubwa wa kuamini uongo kuwa ni ukweli, kwa kuwa tu unasemwa na kuaminiwa na watu wengi.
Kuna wenye fedha nyingi lakini wana uhitaji mkubwa kuliko hata mafukara. Kiuhalisia fedha ni matokeo tu, na ni ya mwisho kabisa, si chanzo wala si mtaji wa mafanikio. Fedha ni kipimo tu cha thamani ya kitu kingine. Fedha, vyeo, umaarufu, magari, usomi, nyumba, mavazi ya kifahari, nk., ni matokeo ya vyanzo vya mitaji mingine kabisa ambayo ndiyo misingi, mihimili au nguzo za mafanikio halisi katika maisha yetu. Bila nguzo hizo, hakuna awezaye kupata fedha, umaarufu, vyeo, magari, usomi, nyumba au mavazi ya kifahari. Katika makala haya, tutaijadili nguzo ya kwanza.
2. Nguzo ya Kwanza ya Mitaji ya Mafanikio ni Afya Njema
Neno afya lina maana tofauti kulingana na uelewa, hali na muktadha. Kuna afya ya uzazi, akili, jamii, uchumi, mwili mzima, au afya ya kitu au suala lolote linalopaswa kuonekana jema au zuri. Kwa muktadha wa makala haya najikita zaidi kujadili Afya Njema (Good Health) ya mwili inayomaanisha utimilifu, ukamilifu au uzima wa mwili wote na viungo vyote pamoja na akili. Afya njema si tu kutokuwepo kwa magonjwa na/au udhaifu wa mwili, bali pia kuwa na jamii safi, salama na inayostawi. Huitwa afya ya jamii.
Wataalamu wa afya hukiri kuwa afya njema ni nguzo muhimu na ya kwanza kabisa katika nguzo za mitaji ya kufanikisha maisha ya kila siku kwa kila mtu. Afya njema ni mahusiano yako mema na mwili wako kwa kuupa unachostahili ili uweze kufanya kazi kwa ufasaha na ufanisi. Bila kuwa na afya njema hakuna jambo lolote analoweza kufanya mtu yeyote yule.
Tunapokuwa na afya njema ndipo viungo vyote vya mwili (ubongo, moyo, mapafu, mifupa, misuli, nk), hufanya kazi vizuri. Kwa hakika afya njema ni nguzo ya kwanza ya mitaji ya kutuletea mafanikio kimaisha, ikiwemo kupata fedha.
Ni dhahiri kuwa mtu yeyote mwenye akili timamu na hekima, lazima atambue kuwa afya njema ya mwili ni baraka au zawadi kubwa kabisa kuliko zote anazotupa Mungu. Afya njema ni utajiri wa kwanza na wa kweli maana kuanzia hapo ndiposa tunafanya lolote na kupata chochote. Utajiri wa kwanza mzuri ni afya njema (The first good wealth is good health). Tunakwenda popote pale tukiwa wazima. Bila hivyo hakuna kinachoendelea.
Mwili wenye afya njema ni punda wa kutekelezea au kutendea jambo lolote. Wataalamu wa afya hutushauri kuwa makini sana na afya ya miili yetu. Tunaambiwa mtu yeyote asiyeona umuhimu wa afya yake ya mwili ni sawa na asiyejali gari lake. Usipoweka mafuta ya kulainisha vyuma, usipokarabati gari yako mara kwa mara, mwishowe huchakaa na kufa haraka. Tukinywa maji safi na salama, tukivuta hewa safi, tukila lishe asilia yenye virutubisho, mazingira yetu yakiwa safi, tunaupa mwili afya njema. Hauharibiki haraka!
Ukishapata hewa safi, maji safi na salama, na lishe stahiki, mwili huhitaji mazoezi ya viungo vyote na kupumzika. Wataalamu hudai kuwa mwili ukikaa tu huzubaa na kulemaa. Ni sawa na gari lisilofanya kazi hupata kutu na kukongoroka kabisa. Waganga wazuri wa mwili ni hewa safi, maji safi na salama, lishe nzuri ya vyakula asilia, mazoezi na mapumziko. Pia kufanya kazi yoyote ile halali ya kutoa jasho kama kulima, ni mazoezi tosha. Yanaleta faida mbili kwa mpigo, yaani kuimarisha mwili na kuzalisha mali.
Niwashauri walioko maeneo ya mijini kama Dar es Salaam na kwingineko, wajizoeze kutembea kwa miguu badala ya kupanda magari. Wanaweza wasifike mapema wanakokwenda lakini hawataugua au kufa mapema! Ulemavu si tu kukosa utimilifu wa viungo, bali pia ni kubweteka na kukaa tu bila kuufanyisha kazi mwili. Mwili ukifanya mazoezi huwa safi (fresh) na akili hupata ufanisi zaidi. Naamini pia kuwa mazoezi huondoa msongo wa mawazo na hasira. Wanabiolojia nao huthibitisha kuwa sumu nyingi mwilini hutoweka kabisa au hupungua sana kwa kutoa jasho mazoezini.
Wapo watu wengi wakiwa bado ni vijana au watakapoanza kuzeeka na kupata madhara ya kutotunza miili yao, wanaanza au wataanza kujiuliza na kujuta sana: kwanini walikunywa pombe badala ya maji safi na salama; walivuta sigara badala ya kuvuta hewa safi; walikula vyakula ovyo (ilimradi vitamu mdomoni), badala ya vyakula vya kuupa afya mwili. Watasema walipenda kukaa tu vijiweni au kuangalia televisheni na kupanda magari kila waendako, badala ya kutembea kwa miguu ili kuuchangamsha mwili.
Kwa jinsi hiyo, tutavamia vituo vya afya kukarabati miili yetu lakini itazidi kukongoroka kwa haraka na kumaliza mali zetu. Inauma sana pale mtu anapotumia mwili wake kufanya kazi nyingi za kujiletea maisha mazuri, lakini baadaye huishia kupoteza mapato yake kuuharibu mwili huohuo! Aghalabu tunatumia afya zetu kutafuta mali kisha tunaishia kutumia mali hizo kuharibu afya zetu. Ni jambo la ajabu kabisa kuona tunanunua uharibifu wa miili yetu, kisha tunaanza kugharamia kuiponya miili hiyohiyo!
Hatuutilii maanani umuhimu wa kuwa na afya njema mpaka tuugue. Maradhi mengi (si yote), ni adhabu tunayopata kwa kutotunza miili yetu. Magonjwa ni njia ya mwili kugoma kufanya kazi, sawa na gari linapogoma kuwaka baada ya kukosa matunzo. Kuugua hutukumbusha umuhimu wa afya njema. Kuna wengine hawawezi kula mboga za majani, matunda, vyakula vya kunde, viazi, nk., na kunywa maji mengi mpaka waambiwe na madaktari. Tusisubiri mpaka tuugue ndipo tukumbuke umuhimu wa kuwa na afya njema inayotuwezesha kufanya kazi zote za kuendesha maisha yetu.
3. Hitimisho
Wanafalsafa huamini kuwa kila anayezaliwa ana uraia wa falme mbili tofauti. Ufalme wa afya njema na wa maradhi. Ni juu yetu kuchagua ni uraia upi unaofaa kuishi nao. Na bahati mbaya wengi tunachagua ufalme wa afya njema lakini tunajikuta tunaishi na uraia pacha - maradhi na afya njema kwa pamoja! Hata hivyo, uraia pacha wa falme hizi haupo kwa kuwa maradhi na afya njema havichangamani. Mwishowe tunauawa mapema!
Miili hii tunayo kwa muda mfupi sana, kwa kuwa huchakaa na kuisha (perishable). Lazima tuitunze na kuitumia vizuri kwa faida yetu na warithi wetu kabla haijakuwa udongo. Ni vizuri tule vyakula vizuri (si lazima viwe vitamu bali viwe bora na asilia), na tufanye mazoezi; ndiposa tutakufa vizuri bila kutaabika kuanza kuikarabati. Inapendeza sana kukata pumzi tukiwa tumekaa kwenye kiti huku tukiwapa urithi na wosia mzuri watoto wetu.
Afya Njema ni Mtaji Wako - Ni Utajiri Wako: Jitunze, Jiongoze na Jiongeze!

Upvote
7