Shilinde_
Member
- Sep 12, 2022
- 7
- 6
AFYA YA AKILI inajumuisha maeneo kadhaa muhimu, iwe kifikra, kihisia, kisaikolojia, na hata kitabia, bila kusahau maeneo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kadhalika.
Kama unatambua uwezo ulionao, na unakabiliana na changamoto za afya ya akili, huku ukiendelea na majukumu ya kiuzalishaji, uwe ni mfanyakazi, mfanyabiashara, au mjasiriamali, tambua kwamba afya ya akili yako iko sawa.
Hata hivyo, afya ya akili haimaanishi kutokuwepo kwa changamoto ya/za afya ya mwili, kwa mfano, ukiwa hauna ugonjwa wowote wa kimwili, haimaanishi afya yako ya akili haina changamoto; unaweza ukawa unaumwa kimwili ila afya yako ya akili ikawa haina shida.
DHANA YA AFYA YA AKILI ilianza kujengeka tangu mwaka 1843 ikihusishwa kwenye jina la kitabu kilichoandikwa na William Sweetser. Kuanzia hapo, na hasa baada ya Clifford Beers (1876 - 1943) kuanzisha harakati za afya ya akili, kumekuwa na harakati mbalimbali zinazohusisha afya ya akili.
Mpaka kufikia mwaka 2021, tangu 1994, kumekuwa na jumla ya maudhui 26 yaliyotumika kuadhimisha siku ya afya ya akili duniani (Oktoba, 10) kila mwaka.
Takwimu zinaonyesha kumekuwa na ongezeko la changamoto za afya ya akili na hali ilivyo, uwezekano wa ongezeko zaidi uko dhahiri endapo jitahada za kupambana na hali halisi hazitaongezeka. Kwa mfano, mpaka kufikia mwaka 2003 kulikuwa na takriban watu milioni 450 waliokuwa wanakumbana na changamoto za afya ya akili.
Mpaka kufikia mwaka 2019, takriban watu bilioni moja walikuwa wanapitia changamoto za afya ya akili.
Ukweli ni kwamba tuna jukumu kubwa la kupambana kuhakikisha hatushindwi kubadilisha hizo takwimu kwa kuzipunguza.
Unyanyapaa dhidi ya watu wenye matatizo ya afya ya akili bado ni moja ya kikwazo kwenye kukabiliana na tatizo, achilia mbali imani potofu, kukosekana kwa uelewa wa kutosha, upungufu wa wataalamu husika.
Watu wenye kipato cha chini ndio wenye nafasi kubwa ya kuathirika na ndio wanaopata shida zaidi wanapopatia hizo changamoto, japokuwa, bado ni suala linalomhusu kila mtu.
Hata hivyo kumekuwa na mawazo potofu ambayo nayo ni vikwazo kwenye harakati za afya ya akili. Kwa mfano;
Sio wachache wanaoamini kwamba matatizo ya afya ya akili yanahusiana na imani za kishirikina.
Kuna wengine wanaamini mtu mwenye tatizo la afya ya akili lazima ana upungufu wa akili. Hali halisi ni kwamba, uwe kipanga, tajiri au maskini, vyovyote vile, suala la afya ya akili linakuhusu.
Pia wapo wanaoamini kwamba, unatakiwa kushughulikia afya ya akili yako pale tu unapokumbana na changamoto zenyewe. Usisuburi mpaka tatizo likupate ndio uanze kulishughulikia, badala yake unapaswa kujua namna ya kukabiliana nalo tangu kabla.
Wengine wanaamini matatizo ya afya ya akili hayazuiliki, japokuwa inawezekana kujiepusha nayo. Mtu aliyejijengea mazoea ya kutengeneza mahusiano mazuri na kila mtu, anayetafuta msaada ya kisaikolojia mapema, anayelala vizuri, mwenye mazoea ya kufanya mazoezi, kula vizuri, asiyetumia vilevi na kadhalika, ana nafasi kubwa ya kujiepusha na matatizo ya afya ya akili.
Pia sio ajabu kukutana watu wanaoamini kwamba matatizo ya afya ya akili ni dalili ya udhaifu. Hili sio suala la nani yukoje na ana uwezo upi; ni suala la yeyote, popote.
Kuna wanaoamini kwamba, kama hakuna anayekwambia una dalili ya/za changamoto ya afya ya akili, anamaanisha ni kweli hauna hizo changamoto. Unaweza ukawa unashida ya afya ya akili na isijulikane kwa watu wengine, na kutokana na uhaba wa uelewa wa changamoto zenyewe, wengi wanaamini tatizo la afya ya akili ni la eneo fulani, kwa hiyo kwa mfano, kama huna dalili za sonona basi huna sonona. Sio hivyo.
Magonjwa ya afya ya akili yanaambukiza. Ni hoja niliyowahi kuisikia nikiwa kijiweni na washkaji, ila nashukuru iliibuka kipindi nikiwepo, na ilisaidia kueneza uelewa kuhusu afya ya akili siku ile. Magonjwa ya akili hayaambukizi, ila kuna uwezekano, kwa mfano ukiwa karibu na mtu mwenye huzuni, wewe pia unaweza kupata hisia za namna hiyo kwa sababu mwenzio kashea na wewe masaibu anayokutana nayo, na hiyo ni kwa sababu binadamu tunauwezo wa kuakisi hisia za wenzetu, ila haimaaishi ni changamoto zinazoambukiza kama baadhi ya magonjwa ya kimwili.
Mawazo potofu ni mengi na ni kizuizi cha kusongesha gurudumu la harakati za afya ya akili.
Nini Kifanyike?
Ni muhimu kila mmoja kujitambua kama mdau. Pia sekta mbalimbali, anzia za kiserikali, binafsi hadi za kiraia, inapaswa zishirikiane kwa dhati kwa namna yoyote ili kueneza uelewa kuhusu afya ya akili. Wataalamu wa afya hadi taasisi za kitaaluma zisiache kujihusisha na hizi harakati.
Serikali inapaswa kuwekeza kwenye eneo la afya ya akili anzia kwenye miundombinu, hadi rasilimali watu, huku ikiendelea kuwezesha taasisi mbalimbali, za kiraia na binafsi.
Sera, na sheria mbalimbali kuhusu afya ya akili ni muhimu zipitishwe.
Pia kuna haja ya kuwa na mitaala ya afya ya akili kwenye kila eneo la kitaaluma, anzia mashuleni hadi vyuoni.
Ni vyema makampuni na mashirika yawe na warsha mbalimbali kuhusu afya ya akili kila baada ya muda fulani, ili kusaidia kuimarisha ustawi wa afya ya akili kwa watumishi.
Kimsingi, utawala bora, utekelezaji wa sera za kuhamasisha afya ya akili, tafiti mbalimbali, uimarishwaji wa miundombinu ya taarifa, ni miongoni mwa hatua ambazo zikichukuliwa zitafanikisha jitihada stahiki.
Ni muhimu pia kuwezesha watu wenye changamoto za afya ya akili kupata huduma za kimatibabu kirahisi.
Haki za binadamu ni muhimu zilindwe ili kuhakikisha ustawi wa afya ya akili. Uvunjifu wake ni moja ya chanzo cha matatizo ya afya ya akili.
Pia ni muhimu, endapo mikakati inayohusisha afya ya akili itajikita kwenye tafiti mbali mbali ili pawe na uelewa wa kutosha kuhusu kila hatua inayochukuliwa.
Suala la kuwashirikisha wadau waliowahi kupitia au wanaopitia changamoto za afya ya akili, katika uandaaji wa sera, mipango na mikakati, lina mchango mkubwa pia.
Yote kwa yote, unapokutana na changamoto ya afya ya akili usikae kimya. Ni afadhali umshirikishe hata mtu wako wa karibu ili kwa namna moja au nyingine upate suluhisho.
Pia kuna chama cha wanasaikolojia Tanzania (TAPA) chenye wataalamu wa unasihi na hata wadau wa afya ya akili wanaoweza kuwa sehemu ya mabadiliko yako.
FUNGUKA, USIKAE KIMYA.
Shilinde x+

Upvote
2