SoC03 Afya ya mtanzania mikononi mwa baba na mama ntilie

SoC03 Afya ya mtanzania mikononi mwa baba na mama ntilie

Stories of Change - 2023 Competition

DON YRN

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Posts
606
Reaction score
1,453
Kwa mujibu wa Wikipedia, Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa. Hivyo basi, ili binadamu awe na afya iliyo bora yaani asisumbuliwe na magonjwa, yapaswa azingatie kula vyakula vyenye virutubisho vyote kama protini, wanga, mafuta. Anatakiwa kula chakula kwenye mazingira yaliyo salama hasa mazingira yake binafsi na mazingira yanayomzunguka. Bila afya bora ya mtu au jamii kwenye Nchi yoyote, ni sawa na bahari au ziwa au mto ulio hatarini kukauka kami siyo kupotea. Afya ya mtu au jamii inapaswa kulindwa kwa gharama yoyote ili isipotee maana mtu ndiye mjenzi wa nchi husika kama nchi yetu pendwa Tanzania.

Biashara ya Mama au Baba lishe(Mama au Baba ntilie) yaani biashara ya kupika na kuuza chakula, ni biashara inayoshika kasi sana nchini Tanzania hasa kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga, n.k. Ni biashara inayofanywa na rika na jinsia mbalimbali kwa lengo la kujipatia kipato(fedha) ili kuendeshea maisha ya kila siku. Kuna watu wanasomesha watoto wao, wameoa au kuolewa kupitia hii kazi, kwa ufupi ni kazi au biashara tegemezi kwa Watanzania wengi sana ikizingatiwa kuwa kulingana na watu wengi kuwa makini na kufanya kazi zingine mbalimbali na kutokupata muda wa kupika chakula majumbani mwao hivyo hutegemea kununua chakula kilichopikwa na mama au baba ntilie.

Nchini Tanzania, inaonekana ni biashara ambayo ni mtu yoyote anaweza kuifanya ikizingatiwa kama una vyombo vya kupikia tu mambo mengine kama usafi utajifunza mbele ya safari. Ni kama unaenda kuuza nguo za mtumba tu.

Biashara ya Baba au Mama ntilie nchini Tanzania inafanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni biashara rasmi. Hii hufanyika kwenye eneo maalumu mhusika kuwa na leseni maalumu zinazomthibitisha kuwa ni halali kufanya biashara ya kuuza chakula kilichopikwa na hulipa kodi mbalimbali(mgahawa), kundi hili sitalizungumzia sana.

Kundi la pili ni biashara isiyo rasmi. Hii biashara hufanywa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoidhishwa kama sokoni, stendi ya basi, n.k. na sehemu ambazo hazijaidhisha kama vile pembezoni mwa barabara au hata eneo lolote la wazi.

DSC_3110.JPG

Mama lishe wakiwa katika shughuli zao katika soko la Kimataifa la samaki Feri. Chanzo: Michuzi blog.

MAMA-NTILIE-768x576.jpg

Mama Ntilie akiwa katika shughuli zake. Chanzo: Mtanzania digital.

1.jpg

Mama lishe wakiwa katika shughuli zao. Chanzo Sufiani mafoto.

Ni kweli kama wananchi ili tujenge nchi yetu Tanzania, tunatakiwa kuwa na afya bora ikiwemo kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuhara damu kuumwa tumbo na magonjwa mengine kama ya kinywa na meno.

Biashara ya mama au baba ntilie nchini mwetu kwa ujumla inafanyika katika mazingira yasiyo salama. Biashara hii inapaswa kufanywa kwenye mazingira maalumu na salama yenye upekee sana.

Kama tusemavyo chakula ni dawa, hivyo sidhani kama Serikali yetu inaruhusu kufanya biashara ya kuuza dawa za binadamu pasipo kuwa na vibali maalumu. Sidhani kama kuna mtu anayeweza kufanya biashara ya dawa za binadamu kama anafanya biashara ya kuuza nguo za mtumba kando kando ya barabara au sokoni na apange kwa mafungu kama ndizi, bamia. Hakuna!.

Biashara ya kuuza chakula kilichopikwa nchini mwetu, asilimia kubwa inafanyika kwenye mazingira hatari yanayopelekea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu, kuhara damu na magonjwa ya kinywa na meno kuwa ni magonjwa ya kujirudia rudia kila mara. Kinga ni bora kuliko tiba, viongozi hampaswi kufumbia macho hili suala kwa kuhatarisha afya za wananchi kwa kigezo cha kwamba ni biashara inayofanywa na watu wa hali ya chini huku watu wakiangamia kwa vifo vya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuhara damu. Miongozo maalumu iandaliwe ili biashara hii ya chakula kilichopikwa ijumuishwe kwenye muongozo kama ilivyo biashara ya maduka ya dawa za binadamu.

Biashara inafanyika kando kando ya barabara na kuna mtaro wa kupitisha maji machafu au sokoni na kwa jinsi masoko mengi yalivyo hasa kipindi hichi cha mvua kwa mkoa wa Dar es Salaam, hali huwa inatisha. Lakini hapo utakuta kwenye mazingira hayo kuna mtu anapika chakula na kuuzia wananchi wenzake huku suala la usafi wa mazingira likiwa sifuri yaani hakuna. Huyu mpishi anakuwa hana muongozo wowote kuhusu usafi ili mradi yeye anafanya kile anachoamini kuwa ni sahihi kwenye uandaaji wa chakula, kumbe sivyo. Hii hali ni hatari sana.

Afya ya mtu au jamii kwa ujumla inapaswa kulindwa, biashara ya mama au baba ntilie au biashara ya kuuza chakula chochote haipaswi kufanywa kwenye mazingira hatarishi(mazingira machafu). Kama nchi hatupaswi kila mwaka kuwa kwenye kampeni zinazotumia mamilioni ya shilingi kutokomeza magonjwa ya mlipuko wakati hizo pesa zingepaswa kupelekwa kwenye magonjwa mengine kama fistula. Hili la magonjwa ya mlipuko tungeliweka kwenye kundi la kuhimiza watu kufanya usafi kwenye mazingira na kunawa mikono yao kwa sabuni na maji tiririka ili wajikinge ila siyo kula chakula kisicho salama au kupikwa kwenye mazingira hatarishi. Sisi ni Watanzania, tuna haki ya kuishi na kulindwa afya zetu. Kama suala la afya ya Mtanzania wameachiwa Baba na mama ntilie, basi wawezeshe kwenye mfumo wa pesa yaani mitaji, elimu ya afya na mazingira na kuboresha mfumo mzima.

Wako katika ujenzi wa Taifa,
DON YRN.
 
Upvote 5
Waheshimiwee mama lishee maana Kuna wengine wanapikaga pilau tamu unakulaa mpk unataman uliye naye nyumban awe anapika km mm lishee ,lkn ndio hvyo ajui kupika pilau Bali anajua kuchemsha mchele..

HESHIMA KWA MAMA LISHE.waboreshewe mazingira na mikopo isiyo na riba kubwaa mama Samia awafanyie mpngo maana Hela za kuuza bandari anazo nyingii sana agawanae na baba lishe na mama lishee..
 
Waheshimiwee mama lishee maana Kuna wengine wanapikaga pilau tamu unakulaa mpk unataman uliye naye nyumban awe anapika km mm lishee ,lkn ndio hvyo ajui kupika pilau Bali anajua kuchemsha mchele..

HESHIMA KWA MAMA LISHE.waboreshewe mazingira na mikopo isiyo na riba kubwaa mama Samia awafanyie mpngo maana Hela za kuuza bandari anazo nyingii sana agawanae na baba lishe na mama lishee..
Naam naam
 
Back
Top Bottom