Afya ya ubongo pamoja na maendeleo yake kwa watoto wetu miaka 0-20

Afya ya ubongo pamoja na maendeleo yake kwa watoto wetu miaka 0-20

bulajunior

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2024
Posts
624
Reaction score
898
Wakuu habari za leo,

Huku tukiendelea kupambana na maisha tukumbuke kuacha kizazi chenye akili sawa sawa! Ubongo ndo kila kitu jamani kwenye maisha ya kiumbe japo vingine havina ubongo lakini lazima kuwe na system mbali mbali ambazo zinaendesha sehemu zingine za mwili wa kiumbe huyo!

Kama tunavoamini sayansi kuwa TUMEUNDWA na vitu ambavyo tunakula kila siku na kila tukila virutubisho huchambuliwa na kupelekwa mahala fulani kwenye mwili kwa sababu ndo vinatakiwa pale. Kuna kirutubisho kinaitwa Omega 3 fatty acid na vipo vya Aina mbili yaani EPA na DHA hivi ni muhimu Sana kwenye maendeleo ya ubongo hasa kwa vijana wetu tunaowazaa.

VINAPATIKANAJE; vipo katika vyakula vya Baharini yaani samaki na wengine pia lakni ajabu ni kwamba DAGAA hawa ni wamebeba omega 3 fatty acids kwa wingi zaidi. Tunijitahidi Sana kuwapatia watoto wetu hivi vyakula kabla hawajafika miaka mitano maana ubongo wa binadamu hukua kwa 90% anapokuwa amefikisha miaka mitano sasa kama hakupa virutubisho hivo tayari ubongo wake utakuwa na shida tu.

Nashauri pia kwenye kuwapa watoto wetu vyakula vyenye Omega 3 fatty acids kama dagaa wengi hawapendi kula dagaa watoto wanakataa Hadi wanalia kabisa ukiwapa dagaa, mzazi kuwa mbunifu ili mtoto ale mbembeleze mwahidi zawadi endapo akimaliza kiasi fulani ulichokusudia wewe tusiwaache tu maana wao hawajui watachagua ubwabwa maharage na juice tu. Asanteni sana.
 
Akipata dagaa hakuna haja ya kujisumbua kutafuta samaki?
 
Back
Top Bottom