SoC02 Afya Yetu Maamuzi Yetu

SoC02 Afya Yetu Maamuzi Yetu

Stories of Change - 2022 Competition

Kidaya

Senior Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
108
Reaction score
95
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Afya ni hali ya kuwa sawa kimwili, kiakili na kijamii na sio tuu kutokuwa na magonjwa.

Ili kuwa na afya njema ni muhimu kujikinga na vitu vinavyotuathiri afya ya mwili, akili na mahusiano ya kijamii.
Tofauti na majanga ya asili yanayotokea bila uwezo wa mwanadamu kuamua, mambo mengi yanayotuathiri kiafya yapo ndani ya uwezo wetu kuamua kutoyapata kutokana na namna tunavyoishi.

Katika makala hii tutaangazia mambo hayo ambayo tukiamua kubadilika tunaweza kujihakikishia kwa asilimia kubwa kuwa na afya bora.

A. Afya ya Mwili
Miili yetu huwa na afya njema tunapozingatia kinga dhidi ya magonjwa.
Ingawa haiwezekani kujikinga kabisa tusipate ugonjwa wowote katika maisha yetu, ila tunapozingatia njia ya kujikinga na magonjwa tunapunguza uwezekano wa kuugua mara kwa mara na kujihakikishia umri mrefu wa kuishi.

Kwa magonjwa yanayoambukiza (mfano malaria, kipindupindu, ukimwi, n.k.) tunaweza kupunguza uwezekano wa kuugua kwa kufanya yafuatayo;

1. Kuzingatia usafi binafsi wa mwili, mavazi na malazi, usafi wa vyakula na usafi wa mazingira yanayotuzunguka

2. Kujikinga na visababishi vya magonjwa kama vile virusi, bacteria na fangasi kwa njia zinazoshauriwa na wataalam wa afya kama kunawa mikono, kuepuka mazingira hatarishi ya kuambukizana magonjwa, na kuzingatia matumizi sahihi ya vitakasa mikono, barakoa, kondom na vyoo.

3. Kujikinga, kuua na kudhibiti uzalianaji wa viumbe wanaosambaza magonjwa kama vile mbu, nzi, kunguni, panya n.k

4. Kuimarisha kinga ya mwili kwa kuzingatia ulaji wa mboga za majani na matunda, na kupata chanjo kwa magonjwa yenye chanjo.

Kwa magonjwa yasiyoambukiza (mfano kisukari, shinikizo la damu, saratani n.k) tunaweza kupunguza uwezekano wa kuugua kwa kufanya yafuatayo;

1. Kuzingatia ulaji wa mlo kamili (wenye virutubisho vyote) na kuzingatia njia salama za kutunza na kuandaa vyakula.

2. Kuacha matumizi ya tumbaku na mazao yake (mfano kuacha uvutaji wa sigara, shisha n.k) na kuepuka unywaji wa pombe kupita kiasi

3. Kufanya mazoezi ambapo tunashauriwa kwa angalau nusu saa kwa kila siku kwa angalau siku tatu kwa wiki.

4. Kuacha tabia bwete na kuzingatia kuwa na uzito unaoendana na urefu (BMI)

5. Kuepuka na kujikinga na kemikali hatarishi na mionzi kwa kadri inavyowezekana

6. Kuzingatia kinga na chanjo kwa magonjwa ambayo vichochezi vyake vina kinga au chanjo mfano saratani ya shingo ya kizazi.

7. Kuwa na mazoea ya kujichunguza miili yetu na kupima afya mara kwa mara ili tatizo ligundulike mapema hivyo kuwa rahisi kulitibu.

B. Afya ya Akili na Jamii
Kuwa sawa kihisia, kisaikolojia na tunavyohusiana na jamii hutegemea tunavyojisikia, tunavyofikiri, tunavyotenda, tunavyotatua changamoto zinazotukabili, tunavyokabiliana na magumu, tunavyohusiana na wengine katika jamii, na kuelewa mambo ya dunia yalivyo.

Kila mmoja wetu hupitia changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri afya ya akili na jamii. Ili changamoto hizo zisituletee athari kubwa kama magonjwa ya akili na kukataliwa na jamii, wataalam wa afya na wa ustawi wa jamii wanatushauri kufanya yafuatayo;

1. Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubaliana na uhalisia wa mambo yalivyo na kutafuta njia mbadala za kukufanya ufikie lengo ulilokusudia.

2. Kujiaminisha kuwa "haijalishi ukubwa wa changamoto unayoipitia, ipo nafasi nyingine, ni suala la muda tuu."
Hii husaidia kujiepusha na maamuzi ya kukata tamaa na kufanya maamuzi mabaya kama kuiba, kudhuru, kujidhuru, kuua au kujiua.

3. Kuwa na mtu unaemuamini wa kumshirikisha changamoto unazozipitia na kushirikiana kuzitafutia ufumbuzi mfano ndugu wa karibu, wanasaikolojia, maafisa ustawi wa jamii, viongozi wa dini n.k.

4. Kutumia muda wako wa ziada kwa kupumzika, kushiriki katika shughuli zinazokupa furaha kama kilimo cha bustani, kuhudumia mifugo, kuangalia mpira/filamu, kushiriki matamasha ya michezo, kutembelea wasiojiweza, kuhudhuria ibada n.k. ili kuepuka kushawishiwa kufanya mambo mabaya/hatarishi kutokana na msukumo rika.

5. Kudhibiti hasira na kuepuka ugomvi na visasi ili kufanya maisha yako yawe ya furaha na amani.

6. Kujipa muda wa kutosha wa kufanya jambo fulani kutegemea na uwezo wako na kufanya mambo mapema ili kuepuka kukimbizana na msukumo wa muda kuisha (deadline)

7. Kuilisha akili yako vitu sahihi kwa kujifunza, kusoma, kusikiliza na kuangalia mambo yanayokubalika katika jamii inayotuzunguka.

Tukifanya maamuzi sahihi ya kutunza afya zetu kimwili, kiakili na kijamii, ni wazi kuwa tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kukabiliana na maradhi yanayotugharimu rasilimali muda na fedha, na yanaigharimu serikali fedha nyingi kuweka miundombinu za kuhudumia wagonjwa.

Pia tutapunguza kwa kiasi kikubwa matukio tunayoyaona na kuyasikia yanayoashiria changamoto ya afya ya kiakili na kijamii kama vile mashambulio ya kudhuru mwili na mauaji, unyanyasaji wa kijinsia na ukatili kwa wazee na watoto.

Kidaya .B.N
chriskidaya@gmail.com
 
Upvote 13

Hongera sana kwa makala ambayo nzuri sana.
 
Nashukuru sana kwa makala yako nzuri sana. Tutaifoward na kwa ndugu wengine.
 
Asante, shukrani sana. Naomba kura yako
 
Back
Top Bottom