Ndugu zangu nawasalimu kwa lugha adhimu kabisa ya kiswahili......
Najua wengi wetu hususani vijana wenzangu kila mara tunapoianza siku mpya kwetu ni kama kuingia vitani kupambania ukombozi wa taifa letu, haijalishi umeajiriwa au umejiajiri. Mtu yoyote anayejihughulisha na shughuli halali ni wazi kuwa sio tu anatafuta kipato cha kumkidhi yeye binafsi, bali pia mtu huyu anapambania uhai wa Taifa lake kupitia ulipaji wa kodi za moja kwa moja au zile zisizo za moja kwa moja.
Ni jambo la kizalendo na kila mtu anayeioenda nchi yake hatoona tatizo kutimiza majukumu yake hasa katika kulipa kodi ili fedha hizo kupitia Serikali ziweze kuboresha huduma mbali mbali hasa miondombinu, elimu pamoja na afya.
Ningetamani Serikali yetu iwe mpatanishi wa kweli, hasa katika kujenga urafiki wa kudumu kati ya Wananchi wake pamoja na huduma ya afya, kama ningepata nafasi ya kuandika kwa kufuata vipaumbele basi katika maadui wa nchi wale watatu ningesema adui mkubwa ni MARADHI, alafu UJINGA na ndipo anafuta umasikini.
Afya zinapokuwa imara maana yake unakua na watu madhubuti na wanaowajibika ipasavyo katika majukumu yao, watoto wataenda shule kwasababu watakua na utimamu wa miili, serikali itavuna mapato kwakua watu watakua wapo bize kwenye kutafuta vipato sio kutafuta uhai, kama alivyosema dada yetu Waziri mwenye dhamana ya afya ya Watanzania UMMY MWALIMU kuwa "Afya sio biashara, afya ni huduma".
Leo naililia Serikali yangu kwa uchungu mkubwa, huwenda wanahangaika kujenga mashule ili kupambana na mitazamo ya kimataifa kwamba kuwa na wasomi wengi katika nchi ni moja ya kiashiria kwamba hiyo ni nchi iliyoendelea, lakini inasahau kuweka nguvu katika kujenga vituo vingi vya kutolea huduma bora za afya, kuajiri watoa huduma bora za afya, kununua vifaa tiba vizuri na vya kisasa lakini kubwa KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI NA GHARAMA RAFIKI KUTOKANA NA HALI ZA WATANZANIA inasikitisha na kukatisha tamaa sana.
Wakati serikali inatumia nguvu kubwa katika kuzalisha wasomi, wasomi hao wanawahi kufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu. Huku Serikali ikisahau pia kuwa ongezeko la umri wa kuishi pia ni kiashiria cha maendeleo katika taifa husika. Inachekesha na kuhuzunisha..... hii ni sawa na mtu anayejenga mwili kwa mazoezi kukazana kujenga mikono pekee bila kuzingatia usawa katika viungo vingine kama tumbo, kifua, miguu n.k.
Ni rai yangu kwa serikali, kwakua imeanza kuona umuhimu wa kupunguza gharama za matibabu basi iangalie uwezekano huo haraka iwezekanavyo kwakua URAFIKI WA KUDUMU WA AFYA NA WATANZANIA ni muhimu na usiohitaji mjadala hasa wa kisiasa.
Lakini pia kwa Wanachi wenzangu,ni afadhali kuzingatia mambo muhimu hususani yanayoshauriwa na wataalam wa afya ili kuepuka kwenda hospitali mara kwa mara, kuzingatia lishe bora, mazoezi na muda wa kupumzika.
Mwisho niwasisitize Wananchi wenzangu kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano katika sensa ya watu na makazi 2022, Agosti 23 ili kuweza kupata idadi yetu kamili kwa maendeleo ya nchi hususani maboresho katika huduma za afya

Upvote
1