Aga Khan kujenga kituo cha Saratani kwa Billioni 13.8 jijini Dar es Salaam

Aga Khan kujenga kituo cha Saratani kwa Billioni 13.8 jijini Dar es Salaam

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
HOSPITALI ya Aga Khan, Dar es Salaam, imezindua rasmi ujenzi wa Kituo chake cha kisasa cha Tiba ya Saratani kitakachonufaisha hadi watu milioni 1.7 katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

Kituo hicho kitakachojengwa katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam, kitapokea hadi wagonjwa 125 wanaohitaji huduma ya mionzi kwa siku.
Ujenzi huo unakuja wakati data rasmi kutoka kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, zinaonyesha kuwa wagonjwa 68 kati ya 100 wa saratani hufa kila mwaka.

Kutokana na changamoto hiyo, Mradi Kabambe wa Saratani Tanzania (TCCP) uliozinduliwa Januari 2020 na Shirika la Afya la Aga Khan (AKHS), umeamua kujenga kituo hicho kabla ya mradi kumalizika mwaka 2024.

Akizungumza jana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hicho kilichogharimu Sh13.8 bilioni, Binti Mfalme Zahra Aga Khan alisema tukio hilo linaashiria dhumuni kubwa la mradi huo ambao ni kuboresha huduma za matibabu ya saratani mipakani nchini.

"Takwimu za Shirika la Utafiti wa Saratani la Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa Tanzania inapokea wagonjwa 42,000 kila mwaka na wastani wa vifo ni 28,000 kwa mwaka," alisema.

“Takriban asilimia 75 ya wagonjwa hao hugundulika wakiwa katika hatua za mwisho. Hii ni changamoto kubwa inayoathiri uwezekano wa kupona,” aliongeza Princess Zahra.

Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) nchini Tanzania Bi Stephanie Mouen alisema anaamini kuwa hadi mwisho wa mradi wa TCCP huduma bora za uchunguzi zitawafikia walengwa milioni 1.7 katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

Alisema mradi huo pia utasaidia kudhibiti vyema maambukizi ya saratani kwa kuongeza idadi ya wagonjwa wanaogundulika katika hatua za awali kutoka asilimia 20 hadi 50.

"Lakini pia itatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kutoka ngazi ya chini hadi kliniki, pamoja na kuongeza uelewa wa umma kuhusu saratani kupitia vyombo vya habari na njia nyingine za mawasiliano," alisema Bi Mouen.

Hafla hiyo iliyoambatana na maonesho ya makala mbalimbali za utoaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo, ilihudhuriwa pia na Mwalimu huyo ambaye aliwashauri Watanzania kuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya mara kwa mara.

Chanzo: The Citizen
 
Hicho kituo wangekijenga Makao makuu jjiji Dodoma,maana ndo katkat ya nchi ,kila mtu anaweza kufika kirahisi .ni upuuz kuweka huduma ya afya kubwa kiasi hicho mbali na wananchi .poor location.
 
Wanafanya hivyo kwa sababu wanatupenda sana waTz au kwa sababu watavuna mabilioni zaidi kupitia mifuko ya bima ya afya, hasa hasa shamba la bibi NHIF ambayo watumishi nchi nzima hukatwa mishahara kila mwezi?
 
Nchi imejaa wasomi hewa..hivi hizo hela nusu kwanini msiwekeza kupambana na tatizo la kansa nchink..kujua tatizo na kupambana nalo..tunaita public health approaches..

Ila kwakua Wasomi hewa wanamini kujenga hospitali ndio kutatua tatizo..sawa jengeni.

#MaendeleoHayanaChama
 
... miradi ya aina hii inatakiwa iwe ya serikali kwa 100% badala ya kuziachia sekta binafsi. Matibabu ya kansa gharama zake sio mchezo mchezo; serikali inapaswa kubeba majukumu ya aina hii.
Seikali ikitekeleza miradi ya aina hii sekta binafsi watakula vipi asali ya NHIF? Hata wakitekeleza, mashine zitakuwa zinaharibiwa kwa makusudi kila siku, halafu mnaelekezwa muende Aga-khan ambako mashine ni nzima..
 
Seikali ikitekeleza miradi ya aina hii sekta binafsi watakula vipi asali ya NHIF? Hata wakitekeleza, mashine zitakuwa zinaharibiwa kwa makusudi kila siku, halafu mnaelekezwa muende Aga-khan ambako mashine ni nzima..
... inasikitisha sana! Gharama za matibabu ya kawaida kama malaria kwa hiyo hospitali zinatisha; sijui matibabu ya kansa gharama zake zitakuwaje! Ila kama gharama za kujenga hicho kituo ni 13b/- sioni kwanini serikali inashindwa kujenga vituo kadhaa vya aina hiyo nchini hususan kikanda kipaumbele kwa yale maeneo ambayo yamekuwa proved kuathirika zaidi na tatizo la kansa.
 
Aga khan hawahawa ambao ukilazwa katika hospitali yao kwa ugonjwa wa maleria tu gharama zake mpaka ukipona sio chini ya laki 5?
Sipati picha huyo mgonjwa wa saratani akihudumiwa kwa mwezi mmoja tu gharama yake itafikia kiasi gani.
Mwananyamala hospital hukuiona mkuu?
 
Aga khan hawahawa ambao ukilazwa katika hospitali yao kwa ugonjwa wa maleria tu gharama zake mpaka ukipona sio chini ya laki 5?
Sipati picha huyo mgonjwa wa saratani akihudumiwa kwa mwezi mmoja tu gharama yake itafikia kiasi gani.

Afya kwao ni biashara na sio huduma.
 
Watakaotibiwa kwenye hicho kituo watakua watu wa hali fulani hivi
 
Back
Top Bottom