Aga Khan na Viongozi wa BAKWATA 1980s

Yaaani mzee wa bakwata na ccm alikuwa na ushawishi kuliko rais wa nchi mwinyi?
Hizi ngano endeleeni kulishana huko kwa mtoro na kichangani.
Cc Dr Matola PhD
 
Madrasa ilikuwa inatowa elimu gani?
 
Madrasa ilikuwa inatowa elimu gani?
Dr. M...
Hili swali nimelijibu mara nyingi sana na ukitaka kusoma zaidi kuhusu madrasa kuna paper ya Ishumi Idara ya Elimu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam bahati mbaya sikumbuki ''citation,'' yake lakini ukifika Maktaba ya Chuo Kikuu wakiangalia kwenye ''catalogue'' itapatikana.

Abel GM Ishumi anaeleza kuwa watu wa kwanza kujua kusoma, kuandika na hisabati ni Waislam na haya wakisomeshwa katika madrasa.

Hizi zinaitwa 3Rs yaani. Reading, Writing and Arithmetic.
Uislam uliingia Pwani ya Afrika ya Mashariki ukiambatana na elimu.

Johann Krapf alipofika Vuga kwa Chief Kimweri kamkuta Chief Kimweri na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.

Elimu au shule haikuletwa na Wamishionari kama inavyofundishwa katika historia ya Tanganyika.
 
Hapa nitakubaliana na wewe tu kwa misingi kwamba hizo 3Rs zilikuwa ni za kidini au Kiislamu.

Kwa sababu hata leo mtoto ambaye hajawahi kukanyaga shule lakini Madrasa anafundishwa alifu be tee see, anazijuwa kuzisoma na pengine kuandika pia.
 
Dr M...
Una uhuru wa kuangalia hili kama akili yako inavyokuaminisha.
 
Kitendo cha kutetea dini kila wakati kinaudhi sana
 
Kitendo cha kutetea dini kila wakati kinaudhi sana
Guluma,
Hii ni historia ya kweli ya tatizo lililopo katika jamii yetu.

Hakika inaudhi sana kuona jamii moja inakandamizwa.

Ikiwa hupendezewi na haya ninayojadili hapa usisome.

Nakufahamisha kuwa nimekuwa Mwandishi Bora hapa JF Jukwaa la Historia kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
 
MZEE

Kauli ya Rais Mwinyi kama kweli aliitoa basi ilikuwa inatosha kumfanya Agakhan atoe msaada wa Kielimu ikiwamo Ujenzi wa Chuo Kikuu Kwa Waislamu nchini Tanzania.

Habari za Kauli au msimamo kinzani wa Songambele Kwa suala husika kupelekea Agakhan kusitisha kusudio lake haingii akilini ( it doesn't click into the mind)
 
Uzalendo...
Jinsi unavyofikiri wewe na mimi hivyo hivyo.
Lakini kwa kuwa ni watu wa BAKWATA historia yao inafahamika.

Mkasa huu nilihadithiwa na watu wawili Riyaz Gulamani aliyekuwa Katibu wa Elimu wa Aga Khan na Tewa Said Tewa na wote walikuwako katika kikao kile na maelezo yao hayakutofautiana.

Historia hizi zina mengi sana ya kustaajabisha.
Ikipatikana nafasi nitahadithia hapa sote tushangae.
 
Hapa nitakubaliana na wewe tu kwa misingi kwamba hizo 3Rs zilikuwa ni za kidini au Kiislamu.

Kwa sababu hata leo mtoto ambaye hajawahi kukanyaga shule lakini Madrasa anafundishwa alifu be tee see, anazijuwa kuzisoma na pengine kuandika pia.
See=Thee
 
Bakwata ni thehebu la serikali ya TZ ndo maana awapendi umoja wa wa ISLAM DUNIAN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…