Against lockdown

Your browser is not able to display this video.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Your browser is not able to display this video.
 

Mnatumia nguvu nyingi sana kuhalalisha uzembe wenu na kushindwa kwenu kuingia lockdown kisa umaskini, mshukuru Mungu kwa namna moja au nyingine hiki kirusi hakionekani kuwaua Waafrika wengi hata wakiathirika, ni jambo ambalo limewashangaza wanasayansi mpaka leo, kwa jinsi tulivyo na umaskini huu wa Kiafrika ukiongeza na uzembe, ilipaswa tufe kama sisimizi tena kwa mamilioni.
Waafrika hatuna jeuri ya kusema kwamba kuna chochote tumefanya kikubwa cha kuzuia maafa, wacheni wengine waseme, sisi tuendelee kutembelea bahati na kuendelea kuomba chanjo au dawa ipatikane kabla kirusi hakijashtuka kwamba kimeisaza Afrika.
 
Umemuelewa huyo Dr kwanza anavyo sema au una bwabwaja?
Ina maana huyo Dr naye ana mawazo ya kimasikini na video zote wanaongea kitu kimoja sikiliza ili ulewe.

Nyie wenzetu Kenya matajiri ndio maana mmesubiria maambukizi ya pande ndio mfungue nchi,sasa hizo akili au matope.
 

Hizi nguvu mnatumia kuhalalisha kwenu kushindwa kupima kisa umaskini wa kujichokea mlipaswa mzielekeze kwenye kuhamasisha jamii wachukue tahadhari, jana mumefanya sherehe eti mumepona corona nyote nchi yote ilhali madereva wenu wakiingia mataifa majirani wanakutwa na corona karibia wote.
Nakuambia tena, Afrika tushukuru japo wengi tumeathirika lakini hatufi kama wenzetu, haina maelezo ya kisayansi, tuna bahati sana.
 
Naona nyie nguvu yenu ipo kwenye kuifungua nchi wakati maambukizi yameongezeka,wajanja nao wametumia nafasi hiyo hiyo ya kukopa huko WB,wanajipigia hela nimeona wenzio wanalia lia ktk twitter account ya the Citizen TV.

Huku watu tahadhari wana chukua huku wakiendelea na shughuli zao,nyie endeleni kujifungia sasa nasikia kuna kipindupindu ,kesho sito shangaa mkivamiwa na Kwashakor na utapia mlo.

Ila si shangai King Kaka hakukosea kuwaita nyinyi ni Wajinga.
 

Sisi tumechukua tahadhari kwa kutumia ushauri na misingi ya kisayansi, hatujajichokea kama nyie ambao mlishindwa kufanya chochote mnatembelea bahati tu kisa umaskini.

Na hata tukifungua, tutafungua taratibu kwa kutumia hatua na mikakati inayoshirikisha ubongo na elimu, sio kama mnavyofanya huko.
Tatizo lenu kubwa ni kwamba mnaelekea kwenye uchaguzi, sasa serikali inaogopa kupoteza umaarufu maana wapinzani wamewapumulia shingoni, mlikua kila mkitangaza idadi ya waathirika, hapo hapo wapinzani wanahutubia na kuwalaumu, hiyo ikasababisha muanze mbinu za kulaumu mapaipai ili mpate mwanya wa kusitisha.

Sasa imewapa afueni, sema mkajikuta kwenye tatizo ilipotokea madereva wenu wanagunduliwa kuwa na kirusi wote kwenye mataifa majirani, ila hilo mumefaulu kutatua kwa kuagiza iwe inawekwa siri kila dereva wenu akigunduliwa na kirusi.
Kwa kifupi mumeamua watu wajifie ila wapinzani wasipate pakuingilia, na ndio maana nikasema bahati yenu kubwa ni kwamba hiki kirusi hakiui sana Afrika, vinginevyo mngepukutika sana maana mlishajichokea na kuachia vyote.
 

Kwanini unasema tulipaswa kufa kama sisimizi tena kwa mamilioni?

Sawa,ugonjwa haujatuathiri kama wengine, hii ndio inaonesha kuwa matatizo ya Africa mengi yanatakiwa kutatuliwa na waAfrica wenyewe na kwa njia zinazoendana na mzingira na uhalisia wao.

Ugonjwa huu ni mpya hakuna mwenye elimu nao na control nao kwa 100%, kila mtu anafanya trial n error, Lockdown imeonesha kupunguza maambukizi, je hizi after effects za Lockdown bado mpaka sasa hazijapatiwa ufumbuzi.

Ok! Kwetu haujaleta madhara sasa, mnatuambia nini? Kukataa ile njia yao na yetu!?

Mkuu huo mstari wako sio kabisa unanishangaza---

kwa jinsi tulivyo na umaskini huu wa Kiafrika ukiongeza na uzembe, ilipaswa tufe kama sisimizi tena kwa mamilioni.


Alexander
 

Afrika huwa tunakufa kama nzige hata kwa magonjwa ambayo yalishapata madawa kama vile Malaria, sasa huu ugonjwa ambao ndio mpya duniani haujawa na data za kutosha kujua au kufahamu unaathiri watu gani na kwa namna gani. Njia sahihi kwenye pandemic yoyote siku zote huwa ni kupunguza maambukizi, ila kwa umaskini wa Waafrika, isingewezekana kwa baadhi ya mataifa, maana ndio ungewaua kabisa.

Narudia tena, Afrika tushukuru sana kwa miujiza fulani ambayo haijapata ufumbuzi, corona haijatuua, imetuathiri tu na kutuacha tudunde mitaani bila vifo, ila ingekua kama aina ya magonjwa ambayo hutumaliza, tungekosa hata kwa kuzika watu, na tuache kujisifia kwamba kuna lolote la maana tumefanya kuzuia corona, na pia zaidi ya yote ni mapema sana kuanza kuringishia mitaani kama mlivyofanya Tanzania eti corona festival sijui bash, ujinga uliokubuhu, mngesubiri kwanza dawa ya uhakika ya hiki kitu ipatikane, na iliyokidhi vigezo vyote vya kisayansi sio hivyo vikombe vya babu mnavyojiaminisha huko.
 

Stories za mtandao tuuu bash hiyo imefànyikq wapi, acha kujenga picha ya Dar ya Mange Kimambi wakati Dar halisi haiko hivyo kaka.Katika hili la huu ugonjwa kila njia ya mtu ina nafasi ya kuwa sahihi na kuwa si sahihi chamsingi kila serikali ipambane kutoka na uhalisia wa taifa lao katika nyanja mbali mbali.


Alexander
 

Hamna cha kila serikali itumie mbinu zake, na hapo ndio mnakosea, hii hata mabingwa wa ukaidi akina Korea Kaskazini, Iran, Urusi, China wote raundi hii wamekubali kushirikiana na dunia, sembuse kajamba maskini wa Kiafrika. Kitu kipya kama hiki ambacho kimeduwaza, kushangaza na kupumbaza wanasayansi wa dunia, tena waliobobea kwenye fani za utaalam wa magonjwa haipaswi kujifanya wakaidi eti mna namna yenu, mnaishia kuwaponza majirani.
Kwa mfano Iran alijifanya mkaidi mwanzoni akaishia kuharibu Uarabuni baada ya yeye kuwa kitovu cha maambukizi ukanda wote huo.
Yaani tushukuru sana hiki kitu kimetuhurumia Afrika, nakumbuka nikitazama video fulani ya waziri Ummy akisema yaani tu basi maana akitazama Watanzania, hamuwezi kabisa.
 
Tatizo lugha, amekurupuka from nowhere
 
Hii kitu ni mafua ya kawaida yakiwa na siasa pamoja na biashara ndani yake. Magufuli hilo amelijua mapema, hakuna ugonjwa hapo ni mbinu za kuifanya dunia yote iwe chini ya watu flani (mwenye kunielewa na afumbue macho yake).
 
Uko sahihi, mpaka October tutajua nani alikuwa sahihi.
 
Haya ni mafua ya kawaida tu. Mengine yote uyaonayo ni mbwembwe za kibiashara kama ARV.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…