Tutaondoa lockdown na curfew kimikakati na kwa kutumia ubongo, sio kujiachia na kujichokea kama mnavyofanya huko Tanzania.
Kwanza kabisa ifahamike sisi hatutumii mgongo wa kwamba kirusi kwa vile hakiui watu Afrika basi na sisi tujichokee na kuachilia, tunafuata ushauri na maelekezo ya wataalam kwenye misingi ya kisayansi, maana hao hao ndio walishauri tufanye curfew na lockdown na wakashauri ziweje.
Kwanza kabisa uhamasishaji na ushinikizaji wa tahadhari utabaki pale pale, upimaji wa kila anayeingia nchini lazima ufanyike, iwe dereva wa majirani au madereva wetu wenyewe wanaporudi, lazima kila mtu apimwe. Upimaji wa sisi tulio ndani lazima uendelee, maana kuna umuhimu mkubwa wa kujua tumeathirika kwa kiasi gani, ili kuwalinda wale bado hawajaathirika.
Na pia sio kwamba tutaachia kila kitu, huduma ambazo sio za muhimu sana kama vile vilabu vya disko vitaendelea kufungwa mpaka siku dawa ya kuponya au tiba itapatikana na iliyokidhi vigezo vya kisayansi. Hatutafanya mnavyofanya huko eti corona bash/party
Mshukuru sana hiki kitu hakiui Afrika, kwa huo ujinga mnaoufanya mngezikana huko hadi kuihama nchi