Against lockdown

Safi Sana.
 
Corona ni vita kuu ya tatu ya dunia kila taifa lina mbinu na njia zake kuweza kuhakikisha linaibuka mshindi, Tanzania imekataa na haitokubali kuchezeshwa ngoma isiyojua nani mpigaji, hatuwezi kuchezeshwa ngoma ya korona na watengenezaji wa korona wenyewe kwa malengo yao binafsi....hakuna haja ya kutoa mapovu ilihali Tanzania si nchi yako, na wala hatukuhitaji ktk nchi yetu...hatutokuwa na lock down ya kuweka watu ndani kama watumwa kwa kuogopa kivuli cha kiumbe asiyeonekana, wenzenu karibia tuvune mpunga na mahindi shambani, ili mtakapochiliwa jela zenu za majumbani mje kununua chakula chetu kwa tuitakayo....tulianza na mungu tutamaliza na mungu nyie endeleeni kuwaabudu wazungu....
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenena vema. Hakuna cha kuogopa, ni kupambana.
 
Hii kitu ni mafua ya kawaida yakiwa na siasa pamoja na biashara ndani yake. Magufuli hilo amelijua mapema, hakuna ugonjwa hapo ni mbinu za kuifanya dunia yote iwe chini ya watu flani (mwenye kunielewa na afumbue macho yake).

Na hapa ndio umetulia ukaona umeandika kitu cha watu kusoma...
 

Hamna cha vita kwenye corona, waachieni wataalam wafanye kazi zao, acheni kuchanganya siasa na hili suala, pande zote mbili mnaharibu, upinzani unataka kutumia corona kama mwanya wa kuipiga chini serikali kwa sababu yenyewe ilizembea, nayo serikali ili kujilinda kutoka kwa mashambulizi ya upinzani, imepambana na kutumia nguvu nyingi kupuuza hili janga na kutaka kuaminisha watu kwamba imefagia corona hamna tena Tanzania.

Mnatuponza sisi majirani zenu, mngekua na ukuta mjifie huko wala usingeskia tukisema, tungewaacha mfe au mpone, ila unakuta madereva wenu wanang'ang'ania kuingia kwenye nchi za watu, wakipimwa wanakutwa mamia kati yao wanasheheni mdudu wanataka kuingia kuambukiza.
Na sio madereva tu, kuna wengine tumechangia makabila na kiasi kwamba ni vigumu kutenganisha watu....hivyo tumeunganishwa kwenye kiuno na hii ndio inatuletea balaa.
 
Fungeni mipaka kabisa na nchi ya Tanzania kila MTU ajue lake, katika vita hakuna udugu, nyinyi mbaki na uzima wenu na sisi tubaki na virus vyetu huo ndo msimamo wetu na hatupangiwi na yoyote yule,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fungeni mipaka kabisa na nchi ya Tanzania kila MTU ajue lake, katika vita hakuna udugu, nyinyi mbaki na uzima wenu na sisi tubaki na virus vyetu huo ndo msimamo wetu na hatupangiwi na yoyote yule,

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbona unaandika kama uliyelewa pombe tayari muda huu.
 
Your browser is not able to display this video.
 
😃😃😃
 
well said
 

Sasa mkuu wenzetu huko wanaanza ku release Lockdown na wanaweka mipango ya kuishi bila ya lockdown, nimeona Mh.Uhuru Kenyatta naye anafikiria hilo, je sababu zao na zenu zinafanana au ndio kisa wanafanya wao? Au sababu ndio hii unayoileta kuwa ugonjwa hauna madhara sana kwetu Africans,je unadhani mkiachia itapunguza ueneaji au nini kitakuwa in positive way mtakapoachia kama focus ni kuzuia na kupunguza maambukizi?

Na je mkishaachia hiyo Curfew, mtaachia madereva wetu kuja kisa hakun madhara sana ya ugonjwa kwa Africans au mtaendelea kuzuia au mtasubiria watayofanya wazungu ili ku-copy?

Mimi naamini kila njia ni sahihi mpaka pale itakapoonekana kushindwa, ugonjwa ni mpya mpaka wataalam unawasumbua.


Alexander
 

Tutaondoa lockdown na curfew kimikakati na kwa kutumia ubongo, sio kujiachia na kujichokea kama mnavyofanya huko Tanzania.
Kwanza kabisa ifahamike sisi hatutumii mgongo wa kwamba kirusi kwa vile hakiui watu Afrika basi na sisi tujichokee na kuachilia, tunafuata ushauri na maelekezo ya wataalam kwenye misingi ya kisayansi, maana hao hao ndio walishauri tufanye curfew na lockdown na wakashauri ziweje.
Kwanza kabisa uhamasishaji na ushinikizaji wa tahadhari utabaki pale pale, upimaji wa kila anayeingia nchini lazima ufanyike, iwe dereva wa majirani au madereva wetu wenyewe wanaporudi, lazima kila mtu apimwe. Upimaji wa sisi tulio ndani lazima uendelee, maana kuna umuhimu mkubwa wa kujua tumeathirika kwa kiasi gani, ili kuwalinda wale bado hawajaathirika.

Na pia sio kwamba tutaachia kila kitu, huduma ambazo sio za muhimu sana kama vile vilabu vya disko vitaendelea kufungwa mpaka siku dawa ya kuponya au tiba itapatikana na iliyokidhi vigezo vya kisayansi. Hatutafanya mnavyofanya huko eti corona bash/party
Mshukuru sana hiki kitu hakiui Afrika, kwa huo ujinga mnaoufanya mngezikana huko hadi kuihama nchi

 
Mshachemka hamba cha mkakati wala nini.
 
Utaishia kutoa povu tu,lakini TZ is CORONA free kaka,but you're still twerking with the shit!
 
Duh
 
Kwahiyo hizi lockdown huku afrika ni mbwembwe tu maana waliyoweka na wasioweka wote hali ni zilezile tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…