Sonko Bibo
JF-Expert Member
- May 24, 2019
- 957
- 1,493
- Thread starter
- #21
Tuendelee,,,,
AGANO JEUSI. 3.
Niliipokea simu na kuiweka sikioni, sauti naijua ni ile ya Vero.
Sasa ubaya ni kwamba kulikuwa na utulivu wa hali ya juu sana kiasi kwamba sio lazima mtu uweke loud speaker hata kwa sauti ile ya kawaida ya simu mtu aliyepo pembeni anasikia tu.
Vero alianza na shutuma moja kwa moja “Ina maana umenipotezea kisa huyo Malaya wako Nadia? Na kwanini usimwambie tu ukweli kuwa una mke na watoto juu?”
Hii ni kauli iliyosikika vyema sana masikioni mwa mke wangu, nikabaki nikipiga hesabu kichwani ni namna gani nitampunch kwenye hili mpaka akae sawa.
Maana nilikuwa nimeumaliza msala, ila hii simu ndiyo imeurudisha upya.
Vero baada ya kumaliza kubwata, alikata simu.
Sikutaka hata kumtazama mke wangu usoni, maana sikujua ni taswira gani atakuwa ameweka muda huu. Nilikaa zangu kimya tu.
Mke wangu alianza kulalamika kuwa “Nilijua tu ipo siku na muda, yote yatajidhihirisha mbele ya macho yangu, na leo imekuwa hivyo, yaani nilikuwa na mashaka na ruti zako hizi za usiku.
Haya baba wewe si umeona humu ndani huridhiki mpaka umeenda kuvitafuta huko nje sawa.”
Nilikaa kimya sikutaka kuzungumzia hilo jambo wakati huu wa usiku, maana kuendelea kulijadili ilikuwa ni kuongeza petrol kwenye moto, unategemea nini?
Nililala mpaka asubuhi ambapo niliamka mapema sana na kwenda buchani kununua nyama kwaajili ya supu.
Lakini baada ya kuja nayo mke wangu alikataa kupika akidai niwapelekee Malaya wangu wanipikie.
Kiukweli hali ile ilinitafuna sana ndani, japo sikulionyesha hilo.
Basi ilibidi nizame jikoni mwenyewe kuandaa mchemsho ule ambapo baada ya kumaliza niliendea chapati ili tupate kifungua kinywa na wanangu.
Za kwake tulimbakishia maana alikuwa bado kaking’ang’ania kitanda lakini nilijua hizo zote ni hasira maana hakuwa na hata lepe la usingizi.
Huku nikiwaza je niende nimtafute Nadia ili nifanye kweli maana nashutumiwa ilihali hata kula sijala, sasa si ni bora nikale kabisa ili hizi shutuma ziwe za haki kwangu?
Baada ya kumaliza kunywa supu nilitoka zangu na kuzunguka zunguka pale mtaani ili walau kupoteza muda.
Kuna sehemu kuna kijiwe cha kahawa basi hapo huwa watu wanacheza drafti, bao na karata.
Ambapo nilikaa sana mpaka ilipotimu saa saba nikarudi nyumbani, nikakuta watoto wameshaogeshwa maana siku hii hawakwenda shule kulikuwa na sikukuu ya kitaifa.
Niliamua kuwatoa out wanangu huku nikimuacha mke wangu nyumbani maana sikuona haja ya kubeba kisirani na kwenda nacho sehemu ambayo nilitakiwa kwenda kupoteza mawazo.
Tulienda sehemu moja nzuri ambapo watoto walikuwa wakicheza michezo mbali mbali na watoto wenzao huku mimi nikiwa nimekaa zangu nachati na Nadia na kumsimulia jinsi hali inavyozidi kuwa mbaya kupitia jina lake.
Alinisikiliza sana, mwisho akaniambia kuwa kuna muda inabidi upunguze upendo kwa mkeo yaani akae akijua kuwa kuna siku linaweza kutokea jambo lolote lile la usaliti yaani asikae katika hali ya kujiamini sana.
Nikamuuliza ana maana gani kuniambia hivyo? Haoni kama ndio na mimi nitakuwa nimeamsha chachu ya usaliti kwa mke wangu?
Akaniambia kuwa Ninaishi kwenye dunia ya kufikirika sana kuliko ulimwengu halisi, akasema kuwa nimejiwekea Imani kubwa sana kwa wanawake kiasi kwamba siku nitayojua kuwa haiko vile navyoamini naweza kuua ama kujiua.
Hapa nilimuona Nadia kama profesa wa mapenzi hivi yaani aliyoyazungumza Nadia ni ukweli kabisa yaani hata nilikuwa nikijaribu kuimagine kuwa labda siku nikamkuta mke wangu kakumbatiwa na msela chobizi nikawa najiona naweza nikaua kabisa, yaani kiwango cha wivu kilikuwa juu sana.
Ilifika kipindi nikawa hata nikiwa kwenye mihangaiko yangu Napata mawazo ya ajabu sana juu ya mke wangu kule nyumbani.Hii yote inatokana na wivu.
Basi nilijikuta namuuliza alipo, akaniambia.
Nikamwambia kuwa jioni nitafanya hima walau tuonane hata tuzungumze maana inaonekana amejaa madini.
Mida ya saa kumi kasoro niliwarudisha watoto nyumbani, kisha nikatoka na kwenda moja kwa moja mpaka maeneo ya Ubungo ambapo aliniambia Nadia kuwa nitamkuta.
Baada ya kuonana tulienda Makonde pale samaki samaki ambapo tulikaa wote tukaagiza juice, yeye akaagiza kuku akawa anakula huku tunaongea.
Hii ndio siku niliyopata nafasi ya kumtazama vyema Nadia, kwanza nilibaini kuwa mwanamke huyu ni mkubwa pengine hata kunizidi.
Nikamuuliza, “Hivi Nadia una miaka mingapi?”
Akacheka kisha akaniambia kuwa “Wewe ni mdogo kwangu wala hata usijisumbue, nakuzidi.”
Sikuona haja ya kuendelea kuhoji maana hata picha inajionyesha tu.
Baadae Nadia aliniomba samahani maana ana kiu ya walau bia mbili. Nikamwambia aagize, ambapo aliagiza Heineken mbili akaletewa akawa anakunywa huku akijaribu kubadili hali ya mazungumzo.
Baada ya kuchangamka akawa hana ile aibu maana yake akajiona ananimudu kimaongezi, na mimi nilizidi kumshindilia bia maana nilikuwa najua hawezi kuishia kunywa mbili tu nilikuwa radhi anywe mpaka aseme basi.
Mtoto chotara la kiarabu na mswahil huyu na kama unavyojua mtu mweusi akipiga kolabo na taifa lolote la weupe hutokea kitu bora kabisa hapa ulimwenguni, ukimuangalia lazima mate yakudondoke, Kaumbika halafu ni mrefu wa wastani sura yake muda wote imepambwa na tabasamu laghaishi.
Baada ya kilevi kumkolea alianza kubwabwaja bila mpangilio ambapo na mimi niliitumia nafasi hiyo kumpakata na yeye akajilaza japo nilijua kuwa ananiigizia kulewa maana alikuwa anajimudu.
Lakini na mimi niliamua kumjaribu kama anaweza kuingia kwenye himaya yangu.
Hakusita aliingia na kujilegeza akiwa ananiangalia kwa macho yaliyojaa uhitaji. Uhitaji ambao haukuwa wa kitu kingine zaidi ya mikuno tu.
Nikamwambia nafikiri tuondoke mahali hapa twende nikupeleke ukapumzike sasa, akaniuliza unanipeleka wapi kupumzika? Kwakuwa ilikuwa ni saa moja na madakika na giza lilikuwa tayari kwenye uso wa dunia nikamwambia anielekeze kwake nikodi bajaji nimpeleke.
Akaniambia kuwa anaishi makongo juu, Basi nilitoka nje ambapo niliita bajaji nikarudi nikamchukua Nadia na kumpakiza ndani safari ya kwenda Makongo juu ikaanza.
Tulifika nje ya geti moja jeusi akabinya kengele mlinzi akaja kufungua, tukazama ndani na kuifuata nyumba moja ambayo ilikuwa inajitegemea maana humo kwenye fensi kuna kama viapartment vidogo vidogo vinne.
Hivyo yeye alikuwa amechukuliwa na baba yake kamoja kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe.
Basi baada ya kumfikisha mlangoni nilimdeshi kama nataka kuondoka, akanishika shati na kunivutia ndani huku akiniuliza kuwa “Unataka kuondoka uniache na nani? Yaani uninyweshe pombe nichangamke kisha uniache peke yangu?”
Nikamuuliza kwani anataka nikae kwake nifanye nini wakati anafahamu kuwa nina mke nyumbani na anahitaji kampani yangu?
Ni kama hakunisikiliza akazidi kunivutia kwake hadi nilipozama ndani kabisa kisha akaubamiza mlango na kulock na funguo kabisa.
Basi kwakuwa wahenga walisema akiutaka mpe ashinde nao, ikibidi alale nao kabisa.
Yalianza madoido ya kupelekana kisiwa cha huba yaani ilikuwa ni full fujo, shika hapa na pale, mara huku mara kule mara imo, ni miguno na mikunjo ya kwenda hakuna kulegezeana kila mtu anataka awe mbabe wa mechi yaani kama umekaa pembeni ukiangalia mbilinge hizi, unaweza kujiuliza hivi watu huwa wanataka kuonyeshana nini haswa maana sio kwa mitindo ile.
Dakika arubaini na tano zilitosha kabisa kuhitimisha ngwe ya kwanza ambapo tulikuwa tukiangaliana tu huku kila mmoja akihema, kisha ndipo Nadia alinyanyuka toka kwenye sofa akinikokota twende bafuni ndio kubaini kumbe shughuli tuliianzia sebuleni na kuimalizia hapo hapo?
Basi niliinuka toka pale na kwenda bafuni huku tukipitia chumbani, kilikuwa ni chumba chenye kila hadhi ya kuishi huyu kiumbe, yaani utadhani ni chumba cha hoteli, hapo ndipo nikabaini kumbe ni kweli wahuni kama hatutafuti pesa basi hata ile picha tu ya maisha mazuri hatutaiona, cheki mtoto anaishi maisha ya ndoto ya wahuni kibao.
<<<<<Oya wahuni,!!! Ukigundua kuwa huna kazi, elewa maana ya kazi kwanza. Kazi ni kwamba una mkataba unaotambua vipengele vya kazi yaani kuanzia masaa stahiki ya wewe kufanya kazi na kupumzika, masuala ya afya kwa maana ya bima yako, na pale unapougua basi stahiki zako zinabaki pale pale. Pia kuna malipo ya likizo na posho za matukio mbali mbali bila kusahau mafao.
Sio shughuli za kila siku zinazokuingizia kipato hiyo sio kazi, hiyo ni shughuli hata kama unalipwa mshahara lakini kama mkataba wako hauzingatii stahiki zako kama mfanyakazi basi hiyo yako sio kazi bali ni shughuli tu.
So hapa nazungumza na wale wahangaikaji wenzangu wenye shughuli mbali mbali, Ukiwa ndio unaanza maisha hakikisha kuwa unajitengenezea paradiso yako chumbani.
Unaweza ukadownload chumba kimoja kutoka pale Five star hotel yoyote na kukifanya kuwa chumba chako maana majukumu unakuwa bado huna. Ishi maisha ya ndoto yako mapema kabla majukumu hayajachagama.
Maana baadae hautapata fursa ya kuyafanya hayo ukizingatia haujakaa sawa watoto pale wanahitaji matunzo kama vile Ada, nguo, chakula hasa lishe bora, makazi yanayostahili kwaajili ya familia. Na kama unavyojua mjini makazi yanayofaa ni gharama sana kuyamiliki.
Chukueni hilo liwafae wahuni wote.>>>>>
Basi tuliingia bafuni ambapo nilionyesha mbwembwe kwa kumuogesha huyu mtoto wa kike…..Japo nilijua fika kuwa ni bitch, lakini nilijitahidi kumcare kama mwanamke mwenye stahiki zote sikujali mapokezi yake yatakuwaje lakini hivi ndivyo nilivyo yaani najitahidi kuwa romantic pale. Inapotakiwa na sio muda wote hata kama ni sehemu ya kazi unakuta dume zima linajilazimisha kuwa romantic basi utakuta linajirembusha macho kama vile lishoga, ni vile tu hawajui ni namna gani wanakera eti.
Baada ya kumaliza kuoga tuliingia chumbani ambapo miguso na mahaba vilianza upya taratibu kabisa muda huu nikiwa nishatoa lile wenge la ashki za mwanzo…
Hivyo ngwe hii akili nilikuwa nimeituliza haswa, yaani nilitumia hisia zangu nyingi sana kwa huyu mtoto wa kike, na hakika alifurahia sana mpaka kunimwagia misifa ambayo sijui kama ni kweli niliistahili ama laa!
Mida ya saa nne kasoro ndio Nadia alikuwa ananitoa kunisindikiza nikachukue usafiri ambapo tulikuta bajaji zinapakia watu huku wakidai wanaishia pale Mlimani city.
Nadia aliniaga huku akiniambia kuwa nimejua kumnyoosha yaani hajawahi huku akinituhumu kuwa nilimpania,
Nikamuuliza ina maana pombe zote zimeisha? Akajibu kuwa hakuwa amelewa pombe bali hamu tu na kuhusu kunywa pombe alidai ana kichwa kizuri halewi haraka wala.
Basi tuliagana na mimi nikaingia kwenye bajaji tayari kuondoka, maana huyu dereva alionekana ni kwamba alikuwa kaleta mteja hivyo wakati wa kurudi ndio ikabidi apakie tu ili asirudi bila mteja.
Nyumbani nilifika saa tano na madakika yake, ambapo nilimkuta wife yupo kawaida tu lakini swali lake la kwanza ni kuwa “Ndio mmeachana na Nadia sasa hivi?”
Nikamwambia kuwa awe na subira basi sio nafika nyumbani zinaanza kelele pia sijamzoea hivyo, maana nyumbani panatakiwa pawe sehemu ya tulizo kwa mwanaume na si vinginevyo.
Basi nilikaa kwenye sofa pale akanipakulia chakula nikanza kula na baada ya kumaliza kula yeye aliaga wa kwanza kuwa anatangulia kwenda chumbani nikamjibu sawa.
Na hapo ndipo nikakumbuka simu yangu kumbe niliiweka silent mode wakati nikiwa na Nadia kuanzia pale Samaki, samaki.Aisee kucheki hivi nilikuta missed call kumi zikiwemo meseji za kutosha kufungua nikakuta ni za mke wangu, kanipigia mara sita na Hamadi kanipigia mara mbili, nyingine ni ya Baba mwenye nyumba wangu wa huku Temeke nae kapiga mara mbili.
Nikaona nianze na baba mwenye nyumba ili nimsikie ana usemi gani.
Alipokea na kuniambia kuwa amepata taarifa kuwa nina mpango wa kuhama lakini akaniuliza mbona imekuwa kimya kimya bila kumshirikisha au kuna sehemu alinikwaza?
Nikamwambia ni kweli lakini kuhusu kwamba eti labda kanikwaza sio kweli, bali ni kutokana na majukumu yangu yameegemea kule nakohamia so nimeona nisogee ili niwe karibu kuepuka pia usumbufu wa usafiri.
Akasema sawa, sikuwa na haja ya kumkazia huyu mtu maana kama nilivyotanguliza sifa zake hapo mwanzo huyu ni mtu na nusu yaani, Pia niliona hatia kidogo maana taarifa kazipata kupitia mtu mwingine na sio mimi.
Pili iliniumiza kuona kuwa mwanamke ndio sababu ya taarifa hizi kuzagaa kwa watu. Sasa hii ni kwa hili ambalo mtu anaweza kukukabili na kukuuliza ama kukueleza, vipi yale ya ndani ambayo si rahisi mtu kukuuliza?
Hapa ndipo nikaelewa ni kwanini taarifa huvuja na kuyafikia masikio yasiyostahili kuzipata taarifa hizo.
Jibu ni hawa wanawake ambao tunaishi nao hata ukimuona ni smart kiasi gani, lakini suala la kutunza siri hawajaumbiwa kabisa hilo nakutonya leo So kama una manyatu nyatu yako baki nayo usimwambie huyu kiumbe anaeitwa mwanamke kama hutaki yafike kwenye jamii.
Maana wewe utakuwa unadhani kuwa watu hawajui kumbe wana taarifa zote maana mkeo atamwambia shosti yake, na huyo shosti yake atamuambia mwandani wake ambae ndie mtu wake wa siri. And the rest remains history…
Nilipomaliza kuongea na Mwenye nyumba nikamtwangia Hamadi, Nae akaniambia kuwa kesho yake anahitaji tuonane kuna mambo inabidi tuyazungumze na kuwekana wazi, Tulikubaliana kuwa ni vyema yeye akaja Temeke kwa mara ya mwisho apaone ili baadae tuondoke pamoja twende sehemu yoyote ili tuzungumze.
Baada ya kumalizana na Hamadi niliinuka kwenda chumbani bahati mlango ulikuwa wazi nywii!! Mke wangu alisahau kuurudishia, hivyo wakati nimefika mlangoni na kuingia ghafla nilimuona akiwa anachati lakini baada ya kuingia aliificha simu yake chini ya shuka haraka, lakini nilikuwa nimeshaona tayari hivyo hakuna alichozuia.
Nilisimama kwa nukta kadhaa kisha nikayakumbuka maneno ya Nadia kuwa nisiwawekee sana asilimia kubwa za uaminifu hawa wanawake, maana hawatabiriki hata pale unapohisi kuwa hachiti lakini amini ndio muda anakuwa anachiti na pia kauli ya Hamadi ndio huwa inaniacha hoi mpaka waleo. Kuwa Mwanamke anapenda sana kitu feki kuliko kitu real na ndio maana anabandika kucha bandia juu ya kucha orijino suala kwake sio uhalisia bali muonekano baada ya kubandika zile bandia.
Vivyo hivyo mpaka nywele na kope je atashindwa nini kukubandikia mwanaume juu ya mwanaume? Na hapa wanaume wa kubandikwa ni wale wanaume feki walamba lipsi na wapaka poda wanaoshinda gym muda wote.
Lakini muda huo huo hayupo tayari kuolewa na huyo kishtobe wake, anakuganda wewe ili uwe kama Yesu wake, yaani akiwa na shida uzitimize kama vile gharama za maisha na mengineyo.
Basi nilisimama pale nikapiga hesabu zangu kichwani kisha kama vile sijashuhudia chochote nilimsogelea na kumshika akiwa anatetemeka maana mtetemo niliuhisi baada ya kumshika, nikamkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso, kisha nikaingia kwenye shuka na kuuchapa usingizi.
Sikutaka kuwa na haraka wala, maana hata kiwango cha wivu kilikuwa kimepungua baada ya kukutana kimwili na Nadia sikuona haja ya kuanzisha vurugu maana mimi mwenyewe sikuwa mkamilifu, ukizingatia ni muda mfupi tu nimetoka kunjunjana na mwanamke mwingine pia niliona kuwa haitaniacha salama moyoni mwangu zaidi ya kunivuruga tu.
Maana kama itafika hatua ambayo nitashindwa kustahimili basi jawabu nitakalokuwa nalo ni kumuacha abaki kama mlezi wa watoto wangu, pia awe kama sehemu ya kutolea hamu tu maana maisha haya huwezi kujiashua kuwa siku zote utakuwa na pesa za kuweza kufurahia ngono na makahaba.
Hivyo atabakia kuwa akiba kifupi tutakuwa tunatumiana kwa malengo maalumu akichoka akahitaji kwenda basi ataenda tu.
Nilimuacha akiwa na maswali kama je ni kweli nimemuona au hapana lakini ni kwamba nilikuwa nimemuona kwahiyo kuhusu hilo hakutakiwa kukisia kabisa.
Asubuhi ilikaribishwa na harakati za kujiandaa kuhama hapa lakini nikimtazama wife simuoni na uchangamfu wake ule.
Nikamuuliza shida nini maana namuona hayuko sawa.
Akasema amepewa taarifa ambazo sio njema kutoka nyumbani kwao. Nikamuuliza zinahusu nini? Akasema hata akiniambia hadhani kama itasaidia maana pia hazinihusu kihivyo hizo ni za kwake yeye kama yeye.
Nikasema sawa. Lakini nilijua kinachomtesa ni lile suala la jana usiku maana kwanza alikuwa anahisi nilimuona ila haelewi ni kwanini sijamuuliza hivyo akiwa kama mwanamke nilihisi alikuwa anadhani kuwa nimeichukua kama kete ya kuhalalisha matendo yangu dhidi yake.
Tuliandaa vitu vyetu kisha niliwatoa out kwaajili ya Breakfast maana sikutaka tupoteze muda kwaajili ya kupika na masuala ya kuosha vyombo.
Kwakuwa hatukuwa na makoro koro kibao basi canter ilitosha kupakia vitu vyetu maana mimi huwa sio mpenzi wa kununua mavitu mengi ya ndani kama walivyo watu wengine hususani pale wapatapo tu pesa hununua masofa mengi yaani unakuta mtu sebule imejaa masofa na viti na meza hata tatu.
Baada ya kurudi nilitoka nikiwa nimeazimia kwenda kutafuta gari kwa ajili ya kutuhamisha. Basi ile nimetoka nikazunguka mtaa wa nyuma nikamcheki Jafari kwanza, maana huyu ni mshikaji wangu mwingine wa kitaa tu hapa, tukawa tunaongea mawili matatu maana sio muda nitatengana nao.
Tulikuwa tumesimama kibarazani kwao pale anapoishi hivyo ni sehemu ambayo inakuwezesha kuona kona nyingi za mtaa huu hasa wapita njia.
Sasa nikiwa hapo na Jafari ndipo nikaona mtu kapita kama kipanga, ile mfyuu!! Nikawaza kwa nukta kadhaa na kuguna Mhh! Huyu sio mke wangu kweli?
Kumbe niliwaza kwa sauti, Jafari akawa amenisikia. Akasema ina maana umeanza kumsahau mkeo hadi usimjue kuwa ndiye mwenyewe?
Nikamuuliza sasa huku nyuma anakwenda wapi na anaonekana ana haraka vile?
Jafari akaniuliza una Kifua?
Kauli hii kidogo ikanitisha ujue, sawa nahitaji kushuhudia na kuijua tabia ya mke wangu lakini je Nafsi yangu itaweza kustahimili matokeo ya kuyajua hayo?
Nikajikuta nazama kidogo kwenye lindi la mawazo kabla sijaamua cha kumjibu Jafari.
Lakini nikauvaa ujasiri, nikamwambia kifua ninacho tena cha kuweza kufuga sisimizi, kama umjuavyo mdudu huyo huwa hatulii kabisa.
Jafari akanikokota mpaka mtaa wa nyuma yake yaani ni kama nyumba tano toka hapo anapoishi Jafari.
Kweli ile tunatokezea kutoka kwenye uchochoro mmoja hivi namuona mke wangu kakumbatiwa na muhuni mmoja hivi anapigwa mate kwa usongo wote.
Yaani ni kama muhuni ana lengo la kukikausha kinywa cha wife, Nilitulia tuli yaani nilikuwa nimetulia kama vile yule sio wife kitendo ambacho hata Jafari hakukitarajia maana mwanzo alihisi nitaleta vagi la kuchimba shimo.
Niliwatazama kisha nikamtazama Jafari machoni kama vile yeye ndiye mwenye mke, kisha nikamuambia Jafari kuwa turudi asije akatuona.
Jafari alishangaa kwanza, asijue nina mahesabu yapi.
Lakini alikubali tu tukarudi hadi mtaa wa pili, ambapo nilimtuma binti mmoja mdogo nikampa maelekezo aende hadi pale walipo lakini azungumze na mwanamke tu amwambie kuwa njoo kuna mtu kanituma nikuite, kisha aje nae mpaka pale tulipo.
Kweli yule binti alienda mpaka pale ambapo alimdokezea hayo na kufanikiwa kuondoka pale wakiwa wote huku akimuacha yule muhuni pale pale kasimama. Kisha mimi nilimuambia Jafari kuwa tuzunguke wife asitukute hapo.
Tukazunguka na kwenda pale aliposimama yule muhuni maana wife akifika pale hatotukuta hivyo atarudi na kutukuta tukiwa huku alipomuacha huyu muhuni.
Baada ya kumfikia kwasababu anatujua alibabaika akataka kukimbia Jafari alimuwahi na kumpiga mtama wa maana, akadondoka akapigiza uso chini akapasuka mdomo.
Jafari akamuinua na kumuweka sawa akampa ngumi tatu na kumng’oa meno mawili fasta, mimi nilikuwa nimesimama namuangalia tu maana sikujua nimfanye nini roho yangu iridhike maana niliona nitaua leo.
Na hata huyo muhuni alijua kuwa kayatimba na sio kilelemama ananijua nilivyo, tifu nyingi za pale kitaa nakalisha mambanga yote.
Basi Jafari yeye aliendelea kumpiga utadhani yeye ndiye mwenye mke huku akisema kuwa tabia za vijana wadogo kama hawa ndizo zinapelekea hata heshima inapungua kwa wake zetu.
Nilichofanya nilimpiga teke la nguvu sehemu za siri kitendo ambacho nilijua ni nini nafanya maana mazoezi nilikuwa nayo ya kutosha niliyoyapata sehemu Fulani ambayo ni siri sitaitaja.
Teke lile lilimfanya muhuni yule kujikunja huku akitoa macho kama anataka kukata roho akalala chini akiwa ameshikilia sehemu nyeti.
Kisha nilikanyaga pale pale kwa nguvu mpaka ikatoka sauti iliyomshitua hadi Jafari akahisi nitaua.
Nilijua naharibu kizazi kwa huyu chalii, hivyo ndivyo maamuzi yangu yalikuwa.>>>>>>
Muhuni alilala pale chini na sisi tuliondoka hapo kufuata kichochoro kile kile alichoondokea wife. Tukiwa kwenye kichochoro hicho tunakutana na wife hapa na hapa…
Baada ya kukutana alibabaika na kujikuta ananiuliza mbona uko hapa hujaenda kuchukua gari?
Nikamuuliza unajuaje kama sijaenda?
Mmmh!! Si nakuona huku, sasa hiyo gari inapita hivi vichochoro kweli?
Nikamuambia nimempa maelekezo dereva kasema anakuja maana anapafahamu. Na wewe huku unakwenda wapi? Nikamuuliza.
Naenda kwa rafiki yangu mtaa wa pili hapo, hata sichelewi narudi sasa hivi, wawahi watoto, wako peke yao tusijetukaibiwa vitu vyetu.
Kauli hii ndio ilinichafua zaidi nikajikuta namwambia kuwa turudi tu maana huyo rafiki yake hawezi kumkuta.
Akashangaa kidogo akaniuliza kwani unajua naenda kwa nani? Naenda kwa rafiki yangu Asha sasa wewe una mahusiano gani na Asha kiasi cha kujua kama hayupo?
Nikamwambia asipoteze muda, rafiki anaeongelewa hapa namjua wala sio huyo Asha hivyo aelewe kuwa najua hayupo turudi nyumbani.
Jafari uvumilivu ukamshinda akamuuliza “Shemeji rafiki yako unaemuongelea hapa si ana vidredi kichwani, mweupe aliyejichubua kama mkongo, mwembamba hivi anapenda kukaa kijiwe Fulani?
Sasa kwakuwa wife ni wale watu ambao huwa hawakubali makossa yao, akabwabwaja “Shemeji tena tuheshimiane yaani kumbe wewe ndiye unamlisha huyu maneno ya uongo ambayo hayana ukweli wowote ndani yake.”
Mke wangu hakuwa akijua kuwa nilimuona kwa macho yangu hivyo alikuwa anajitahidi kwa kila namna ionekane Jafari ndie anatunga uongo.
Nilimuwasha banzi moja tu maarufu kama kelebu, aliona kizungu zungu pale pale na kuyumba huku akijigonga kwenye ukuta wa nyumba na kutulia.
Jafari akaniambia chief, umeua……..>> nikamuambia kuwa sio rahisi najua nachokifanya.
Baada ya dakika mbili alizinduka kutoka kwenye usingizi ule wa muda.Nikamshika mkono na kumkokota kwenda nyumbani, Jafari yeye aliamua kushika njia yake huku tukiagana pale.
Nilipomfikisha nyumbani nilimuacha pale akiwa kauvuta mdomo nikaenda kufanya utaratibu wa gari,
Baada ya kurudi tulipakia mizigo yetu na kutokomea zetu kwenda kawe.
Tulifika na kuanza kupanga mazingira yetu mle ndani na hakika niliona kuwa pamepwaya, maana vyumba viwili na sebule pamoja na kajiko kadogo, kifupi vitu vyetu vilimezwa hata visionekane kuwa ni vitu.
Baada ya kuingia mwanamke alianza kukagua mazingira ya pale home, akaja akaniambia kuwa hakika kapapenda sana panaifaa familia yetu.
Sikutaka kugusia kuhusu lile suala maana tulikuwa ni kama tumeingia dunia mpya hivyo sikutaka kuyaanza maisha mapya kwa vurugu ndio kwanza nilitoka na kuchukua boda mpaka pale shoppers plaza mikocheni.
Nikafanya kashopping kadogo kwaajili ya familia kisha nikarudi nikiwa na zawadi zao.
Baada ya kufika niliwapatia kila mmoja za kwake na hakika kila mmoja alizipenda zawadi zake.
Kisha nilimvuta my wife tukaingia bafuni kuoga wote maana choo na bafu vimeunganishwa na viko ndani ya nyumba na tunavitumia sisi wenyewe maana wale wengine wawili kila mtu ana choo chake ndani maana vile vyumba ni self contained.
Tukiwa humo maliwatoni tulifanya yetu mpaka choo hicho kikajuta kutupata wageni sisi.
Tulitoka humo maliwatoni na kuhamia chumbani ambako tulikuwa huru sana pia huko tuliendeleza libeneke, yaani ilikuwa ni varangati mpaka mke akauliza mbona ni kama unanikomoa hebu tupumzike bhana.
Ratiba ya kesho yake ambayo kulingana na ratiba ya ile familia yetu mpya ya biashara ile, hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho katika zile tatu za mapumziko.
Mida ya saa tisa nilipokea simu kutoka kwa Hamadi ndipo nikakumbuka kuwa jana yake tuliahidiana kukutana Temeke nyumbani kwangu kule…..na nimefanya uzembe nimeondoka bila kumtaarifu kama nahama,
Baada ya kuweka simu sikioni aliniambia yeye ndio anapanda kwenye basi aje Temeke, nikamuuliza ushapanda akasema ndio na ndio dereva anaondosha gari.
Nikamuambia naomba ukifika kawe msikitini Joesph hapa ushuke, akauliza ina maana uko kawe tayari yaani umekuja kututembelea kimya kimya?
Nikamjibu ndio akifika ashuke aniambie tu nije nimchukue, akasema poa.
Baada ya dakika nne Hamadi alinipigia simu nikaenda kumchukua na tukaenda kukaa mle ndani Tanganyika pekazi.
Sikutaka kumpeleka home kwangu kwanza hata sijui ni kwanini. Maana yeye hajawahi kunikaribisha home kwake japo kule kwangu Temeke alikuwa akija mara kwa mara.
Tulikaa, Hamadi alikuwa na soda mbili za kopo, akanipa moja tukaanza kunywa na maongezi juu…>>
Hamadi: Vipi Mswati, michongo inakwendaje?
Mimi: Fresh tu mwamba wangu yaani nashukuru maana hujui ni kitu gani kikubwa umekifanya kwenye maisha yangu basi tu hata nikuelezeeje huwezi kuelewa.
Hamadi: Mswati acha hizo basi mwamba, ina maana urafiki wetu ni kwaajili ya nini kama sio kupigana tafu?
Mimi: Sawa lakini nahitaji siku moja hata kama nitakufa kabla sijakulipa fadhila zangu nataka hata ukija kuzuru kaburi langu ukute alama inayoonyesha kuwa “We were brothers indeed.”
Hamadi: You are going too far my brother, mbona kawaida tu? Hiki nilichofanya It’s what brothers do for each other, that’s it.
Mimi: Ok nimekuelewa Mswati nilitaka tu utambue kuwa nathamini hiki ulichokifanya kwangu na familia yangu kwa ujumla.
Nilitaka nimchomekee kuhusu sisi kuwa kama ndugu kwa muda mrefu lakini hajawahi kunipeleka kwake zaidi ya kuishia kukutana njiani tu kama hivi lakini akaniwahi, yaani ni kama alinisoma moyoni japo najua kuwa ilitokea tu kimgongano wa kawaida.
Hamadi: Mswati, leo nataka nikupeleke napoishi ujue hapa Dar mimi nina ndugu zangu wawili wa kike maana kwetu mimi ndie mtoto wa kiume pekee. Na macho ya wazazi wangu yako kwangu.
Mimi: Itakuwa vyema maana mmoja wetu anaweza kupata tatizo ikawa ni shida kupeana msaada hivyo tukifahamiana inakuwa vyema zaidi.
Hamadi aliniambia, kwani unadhani naishi mbali sasa? Twende tuchukue bajaji itupeleke, kweli tulipanda bajaji na kwenda hadi nyumbani kwake.
Ilikuwa ni mitaa ya udoweni kabla hujafika makaburi matatu mkono wa kushoto, kulikuwa na nyumba moja nzuri ndogo iko ndani ya uzio geti kijivu tuliingia humo.
Tulikaribishwa na dada wa kazi ambae alikuwa kaajiriwa na Hamadi, hakika nilitambua kuwa huyu mwenzangu kwanza kimaisha alikuwa kanipiga gepu kubwa mno.
Kwanza niliangalia mazingira ya pale, maana mwamba kapanda garden ya ukoka na maua mle ndani yaani ni ukijani Fulani hivi unavutia sana machoni na kuirefresh akili muda wote. Pembeni kapaki gari yake aina ya vanguard, japo sikuwahi kumuona nayo pindi tunapokutana.
Ukiachilia hivyo vyote jamaa yangu anafuga mbwa tena wale niwapendao haswa maana anao wanne aina tofauti tofauti, Kuna Maligator, German sherphad, Pressa canario bila kumsahau mfalme wa mbwa Kangal.
Yaani niliwatazama hawa mbwa baada ya kuwafungulia nikawa navutiwa na namna yanavyomkubali mwamba kwanza yalikuja taratibu yakanichukua maelezo pale ikiwa ni kunusa harufu na kunitazama usoni yakiwa yanajaribu kunielewa kuwa ni mtu wa aina gani kama ni mwema ama mbaya.
Aliyenivutia zaidi ni German Sherphad kutokana na uwezo wake kwanza anakaa halafu anakuwa anakutazama kwa kuinamisha kichwa kushoto kisha kulia kama mara nne hivi yaani muda wote anakuwa anakuchunga wewe hata akienda mbali atahakikisha kuwa jicho lake halitoki kwako.
Hawa Pressa canario na Kangal wao ni mbwa wa vita zaidi maana wako kwenye kilele cha ufalme wa mbwa.
Wana miili mikubwa sana yaani nilikuwa nawaza ikitokea yakanichenjia pale sidhani kama Hamadi atamudu kuyazuia aisee maana kwanza hayana uvumilivu pale yanapoamua la kwao.
Maligator yeye alikuwa amekaa amejitenga hataki mazoea na wenzake, ni mtulivu halafu ana mwili standard umejaa misuli sio sana yaani ndiye mwepesi sana kuliko wote hapo.
Nikamuuliza Hamadi kuwa aliwatoa wapi?
Akanijibu kuwa aliwanunua, wote hao amewanunua kwa awamu nne tofauti, na yalikuja yakiwa madogo mno,
So yamemzoea kama mwenye nayo. Bila amri yake hayawezi kufanya chochote, kasoro kwa usiku ambapo yanakuwa na uhakika kuwa amelala au hayupo.
Ukileta pua yako humu bila utaratibu Mswati tunaku R.I.P siku hiyo hiyo.Aliniambia Hamadi.
Basi Hamadi alinikaribisha mpaka ndani kwake ambapo jamaa kafunga kiyoyozi cha gharama na nje ana genereta standby incase umeme ukikatwa na wale jamaa.
Ndani jamaa ana Samani za gharama sana hana mambo mengi bali ana yale ya msingi tu na hakika hapo kaweza.
Tulikaa ambapo Hamadi aliinuka na kwenda kwenye shelf moja ya pale sitting room akavuta wine moja akaja nayo akaimimina kwenye glasi mbili tukaanza kunywa.
Kifupi kilikuwa ni kinywaji kinaurefresh mwili unakuwa na nguvu hata msongo wa mawazo unajikuta umeisha kama ulikuwa nao, ni mahususi kwaajili ya kutuliza akili na kuuona upande mzuri wa maisha hata kama ulikuwa unakata tamaa ya kuishi unajikuta unaanza kuona kuna maana kubwa kuwepo duniani.
Kumbe ndio maana wenye pesa wanaishi miaka mingi tofauti na masikini.
Tukiwa tunagonga wine mdogo mdogo, Hamadi aliniambia kuwa anatarajia kusafiri kwenda Pakistani. Kuna mali anakwenda kufuata kutokana na maelekezo ya familia yetu hii, lakini akaniambia ameona ni vyema tukutane aniambie mawili matatu kuhusu hii familia.
Kwanza aliniambia kuwa nisipende sana kupokea hivi vilikizo vya siku kadhaa navyopewa na kampuni, akaniambia waonyeshe kuwa una njaa na kiu ya pesa yaani pambana kila siku upate kazi, yaani usitosheke na hivi vimilioni unavyoingiza kwa wiki. Pambana kama kuna uwezekano wa kuingiza milioni mia kwa wiki vimba nayo uipate maana hizi kazi hakuna mwenye garantii kama kesho utaamka.
Na ukizingatia kuwa wewe tayari una wale makidi wawili pambana sana ili hata ikitokea lolote unakuwa na msingi mkubwa wa kuwaachia madogo na mama yao.
Ujue ikitokea hata haupo familia iwe na nguvu ya kutosha.
Nikushauri ujikite kwenye kutengeneza pesa nyingi zitakazokusaidia hata kama itatokea hizi mishe zikabuma siku moja.
Ujue kuna tofauti kati ya kutafuta na kutengeneza pesa, sasa wewe unatakiwa ujikite kwenye kutengeneza pesa. Halafu uwe msiri sana yaani unaweza ukachukua nyumba nzima ili usiruhusu macho ya watu kuona vile unaishi.
Nakumbuka nilikwambia kuwa nina zaidi ya milioni hamsini kwenye akaunti, lakini ngoja nikwambie ukweli ni kwamba mimi nimebakiza kiwango kidogo kama robo Fulani kuifikia B. moja. Akaniambia kuwa kuna ile Beureau De Change ya pale…..Basi ile ni ya kwangu na pale yupo sister angu ndio anaendesha ile biashara. So kupitia mle ndio natunza na kutakatisha pesa zangu.
Nilishangaa kidogo lakini kwa aina ya maisha niliyoyaona anayaishi huyu jamaa nilianza kusadiki maneno yake. Huyu jamaa ni milionea wa kutupa, ila akitoka nje ya geti lake ni ngumu mtu mwingine kuamini kuwa huyu jamaa ana mkwanja mrefu kiasi hicho.
Japo utaishia kusema kuwa jamaa yuko njema yaani anajiweza lakini huwezi kumuweka katika viwango hivi alivyo.
Nilijitazama na kujitafakari nikagundua kuwa kumbe mimi ni kadagaa tu kwa huyu Hamadi, maana yake ni kuwa wakati mimi naanza kupumua kwa kuvuta hewa iliyojaa ahueni na kutoa ile iliyojaa dhiki uhalisia ni kuwa kile kiasi ambacho ninacho nikikibadilisha naweza kuwa na kama milioni ishirini na nane hadi kuikaribia tisa
Lakini hicho kiasi amini kinaweza kuishia kununua tu huu usafiri aliopaki Hamadi hapa nje.
Hamadi aliniambia niache mchezo niwe serious na maisha maana akiniangalia bado nina safari ndefu ya kwenda.
Ukweli ni kwamba huyu rafiki yangu nimemzidi miaka mitatu maana mimi nina miaka thelasini na tatu yeye ana miaka thelasini kamili.
Hamadi anasema lakini ili hayo yawezekane inatakiwa niwe invisible kwa watu, namuuliza invisible kivipi?
Ananiambia kuwa natakiwa nifunikwe haswa, yaani hata watu wakiniona wanakuwa ni kama hawanioni kabisa yaani wasipate ile hali ya kuniweka vichwani na kuanza kunijadili kuanzia mtaani hadi humu kwenye familia.
Nikamuuliza kwani familia ina watu wangapi?
Akasema kuwa ina watu wengi mno kiasi kwamba hata yeye hajui idadi yao maana wengine wamesambazwa mikoani.
Akanitonya pia kuwa hata mimi inaweza ikatokea siku moja nikapanda renki nikapelekwa mkoani nikawa Shefa mkuu wa mkoa huo.
Na hapo ndipo mtonyo utakapoongezeka maradufu maana mimi nakuwa napokea mzigo mkubwa kisha nadaiwa hesabu ambayo itakuwa inaniacha na kiasi kikubwa cha baki.
Pia aliniambia kuwa nibadilishe namna navyofanya mawasiliano maana ninavyozidi kuingia mchezoni ndivyo vizingiti vinaanza kujitokeza na hakuna anaepanga hayo bali ndiyo kanuni ya huu mchezo.
Unahitaji kuwa smart na mbunifu haswa ukiwa katika hii michezo . Kichwani unatakiwa uwe vizuri sana kuweza kuuendesha huu mchezo maana wakubwa wanakutegemea kwaajili ya usmart na uaminifu wako tu nje ya hapo hakuna wanachohitaji toka kwako.
Na ukizingua hapo ndio utaweza kukutana na watu ambao sasa hivi unapishana nao tu road na unawaona wa kawaida sana lakini uhalisia wao sio huo unaouona kwao.
Mfano mzuri uliwahi kujua kama mimi niko hivi? Alimalizia Hamadi kwa swali.
“Hapana sikuwahi hata kukufikiria katika angle hii” Nilimjibu.
Basi inabidi uwe makini sana Mswati yaani kama kipindi kile ulivyokuwa unawika pale skuli kwa maakili mengi, hapa ndipo unatakiwa kuitumia akili yako kwa asilimia mia mbili.Aliniambia Hamadi.
Nilimuelewa sana maana sitaki kurudi kwenye dhiki jambo ambalo litaleta fedheha kwa familia yangu na ukizingatia tayari nishawaonjesha aina ya maisha ambayo yanahitaji muda wote niwe vizuri mfukoni.
Basi baada ya mazungumzo hayo tulitoka huku yeye akiniambia kuwa anaenda kumuona mpenzi wake aitwae Nasra, yeye alikuwa anaishi Mbezi beach Tank bovu mitaa ya chini yake hapo kama unashuka mtoni hivi lakini hufiki mtoni.
Mimi niliondoka na kwenda mjini kwaajili ya kubadilisha kiasi cha dola ambapo nilichukua kirikuu nikawa nanunua vitu vya msingi vya ndani.
Nilitumia kama milioni nne hivi kufanya mabadiliko mle ndani na hakika sasa palivutia na kuleta ile hadhi stahiki.
Mida ya jioni nilipigiwa simu na Denis lakini sikuipokea baada ya simu kukatika ndipo nikamtafuta kwa namba yangu mpya ambayo nilikusudia iwe ya kazi. Alipokea alivyosikia sauti tu akasema naona unaanza kuklick kwenye familia taratibu na hii inanifanya niwe na Imani zaidi na wewe.
Basi aliniambia kuna sehemu natakiwa kufika kuchukua mzigo mida ya saa tano usiku na ni pale Mikocheni kwa Mwalimu.
Basi muda ulipofika nilifika eneo husika ambapo, nilirushiwa begi kisha nikatembea zangu kwa tahadhari zote nikachukua boda nikaingia zangu kawe hapo nikalala. Kusubiri ratiba za kesho yake ambapo jamaa aliniambia inabidi nikaze mwili kuendana na ratiba maana natakiwa kuanza kazi ile mpera mpera haina kupumzika.
Na nyongeza juu ya hili ni kwamba mabegi yote yanayokuwa na mzigo huwa nabaki nayo baada ya mzigo kuwa umeisha na bahati nzuri ni yale orijino kabisa kiasi kwamba ukiyaulizia madukani unaweza usiyakute ama ukiyakuta unakuta bei iko juu sana, kuanzia laki mbili kwenda juu hata kale kabegi ka kwanza ni mali safi kabisa huwezi kukaona hovyo hovyo.
Maisha yaliendelea kwa takribani mwezi mmoja na masiku kadhaa ndipo likaja kutokea jambo.
Ni hivi nilipokea mzigo mmoja nikaenda nao hadi home, nikauhifadhi kwenye begi langu moja hivi kisha nikatoka kwenda mahali kidogo hata sikumbuki vyema nilienda kwaajili ya nini lakini nakumbuka nyumbani sikumkuta mwanamke huenda alienda sokoni.
Maana watoto walikuwa shule na ilikuwa mida ya saa nne hivi. Huko nilikoenda niliacha nimefunga vizuri maana tulishagawana funguo mimi na mke wangu ili ikitokea mmoja katoka mwingine asipate shida kuingia ndani.
Sasa baada ya kurudi nikakuta kigeti kidogo cha pale getini kiko wazi jambo ambalo si kawaida maana kila mtu wa humu getini ana desturi akipita anakifunga kigeti hiki.
Sasa ile nazunguka upande ulipo mlango wa kuingia kwangu upande wa kulia wa nyumba hii, nakuta mlango wangu umeachama wazi kabisa.
Moyo ukapiga paa!!....Nikahisi hali ya hatari moyoni.
Kuingia ndani nakuta vitu viko sawa sebuleni.
Kuingia chumbani naona milango ya kabati la nguo iko wazi, kuangalia kuna mabegi hayapo mojawapo ni lile nililoweka mzigo,
Nikacheki kwenye kidroo cha kabati kiko juu kabisa ya hili kabati humo ndimo naweka kiasi chote cha pesa ninachovuna kwenye biashara hizi.
Kukifungua nakuta pesa zote zimo hakuna shida, kidogo moyo wangu ukatulia nikaona bado maisha ninayo.
Kuangalia mpaka mikoba ya mke wangu haipo na mabegi baadhi ya watoto ya shule pia yamebebwa.
Sikutaka kujiuliza sana maana najua mambo yashaharibika tayari mzigo wa maana kama milioni mia nne nitaulipaje hata nikisema nipige simu nitaongea nini mpaka wanielewe?
Na kama nilivyosikia kuwa hii familia ina watu wengi wazito hivyo ni kama CV yangu ishaharibika tayari hakuna hata mtu mmoja atakaenielewa.
Nilijaribu kuwa wao kwa muda halafu ndio anatokea mtu ananielezea yale nayopaswa kuwaeleza nikaona hata mimi siwezi kuelewa kirahisi na kama jinsi hii biashara ilivyo na kasumba nyingi yaani ikitokea hata ajali inaonekana ni tamaa imekuingia.
Nilikaa pale ndani kitandani nikiwa najitafakari kiundani kabisa huku nikijiuliza kwanini mkosi huu umenikuta mimi? Kwani nina gundu gani mimi?
Sijui hata wazo hili lilitokea wapi nilivuta simu nikampigia Hamadi, Simu iliita wee bila kupokelewa hali ambayo ilizidi kunichanganya.
Nikajaribu kama mara saba hivi ya nane ndio ikapokelewa “Hey Mswati, sorry nilikuwa bafuni broo niambie.Alisema Hamadi.
Nikamwambia kuwa nina issue inanichanganya tuonane ili tuone naitatua kwa namna gani. Akaniambia njoo home hapa chap maana najiandaa nitoke.Sikuchelewa nilitoka nikirudishia mlango maana ulikuwa umevunjwa maana kitasa kilikuwa kimeharibika kabisa.
Baada ya kufika tu Hamadi alifungua geti inaonekana aliniona kupitia kamera zilizofichwa,
Baada ya kuingia ndani nilimtazama usoni nikiwaza nimwambie huyu jamaa ama niache? Maana dunia hii unaweza kumuona mtu ni rafiki yako kumbe hujui ana maslahi yake kwako yaliyojificha.
Nilikaa kimya kisha nikamwambia “Mswati nina bonge la msala man, yaani mzigo wa watu umepigwa mida hii hii huwezi amini yaani.
Hamadi akaniambia kuwa nimueleze mzigo umeibiwa kwa namna gani?
Nikamueleza akafikiria kidogo kisha akaniambia kuwa kama hao watu wameiba mabegi basi ni wazi walitageti huo mzigo ama pesa.Akasema subiri kama wameondoka na mabegi yote kuna namna tunaweza kufanya.
Akasema kuwa mzigo huwa haupotei kirahisi hivyo hii ni familia kubwa sana, Akapiga simu sehemu na kutoa taarifa kama nilivyompa maelezo.
Baada ya muda wa kama nusu saa hivi, aliniambia kuwa tuondoke mzigo ushapatikana. Hapo nikashusha pumzi kisha nikajiuliza je nafasi yangu kwenye hii familia itakuwaje?
Lakini Hamadi aliniuliza mbona umehamia jirani kwangu na hatuambiani nikamwambia tangu siku ile tunakuja hapa ndio nilikuwa nimehamia pale.
Akasema kuwa nimeanza kujifunza code muhimu za huu mchezo, ila bado inatakiwa nijitengeneze ili misuko suko kama hii ikae mbali kabisa na mimi na familia yote kwa ujumla.
Tuliondoka huku nikijiuliza wamejuaje mzigo ulipo haraka hivyo nikakosa jibu.
Tulifika mpaka maeneo ya kwa Londa chini kuelekea mtoni ndipo nikakutana na sura za ajabu zikiwa zimewashikilia madogo wanne huku wakiwa wameshapendeza kwa kipigo.
Hao walikuwa ni vibaka tu na bahati nzuri mzigo ulikutwa uko salama kabisa Ila baadhi ya mabegi na mikoba na baadhi ya vitu vidogo ndio walikuwa wamewagawia wezi wenzao wakauze maeneo ya Keko na huko Temeke yaani wizi ukifanyika Kinondoni basi mali zinaenda kuuzwa Ilala huko mbali vingunguti ndani ndani huko.
Walikuwa wamelowa damu na walipewa maagizo wawaite wenzao walete vitu hivyo la sivyo unaanza msako wa chaka tu chaka wa kudavila vibaka wenzao.
Baada ya kuona hivyo sikuona kama kuna uwezekano wa kuaminiwa na kupewa mzigo tena so nilikuwa nikisubiri hatma yangu.
Hamadi alisogea pale akawa anaongea na wale watu kwa muda mrefu huku wakisikika kusema “Sawa kwa hilo tutakuelewa ila unadhani mkuu akisikia hii issue atatuelewa?”
Baada ya mazungumzo ya muda mrefu Hamadi aliniijia na kuniambia tuondoke, tuliondoka huku nikiwa najiona kabisa kwenye ile familia nishatolewa simo tena.
Baada ya kufika kawe tulikaa pale kwa hamadi mara simu yangu ikaita kucheki ni Denis, nikapokea akaniuliza vipi?
Nikamjibu freshi tu.
Akaniambia pole, chapa kazi hiyo ni sehemu ya kazi kikubwa kuwa macho na uwe na focus kubwa sana. Ukipoteza focus tu unajikuta uko nje ya mchezo asubuhi tu. Hapo nikashusha pumzi. Maana nilijua kishanuka tayari.
Muda huu nilikuwa nimevaa mkoti wangu mkubwa japo ilikuwa ni mchana na jua ni kali miksa joto la Dar lakini kwani mimi hivyo vyote nilikuwa navisikia sasa? Kikubwa kwangu ilikuwa ni hizi pesa za kigeni nilizoamua kuwa natembea nazo sehemu zote maana ndio jasho langu hilo. Likipotea ina maana kuwa kazi yote hii inakuwa nimejitolea.
Nilimuaga Hamadi kuwa naondoka nirudi nyumbani , maana mpaka muda huu sikuwa nimepokea simu kutoka kwa wife ina maana bado hakuwa amerudi toka huko alikokuwa.
Kweli nikachukua boda toka pale udoweni mpaka nyumbani, sasa ile nashuka kwenye boda hivi ndio nawaona mke na watoto wakiwa ndio wanaingia kwahiyo ina maana aliamua kuwapitia kutoka shule kisha ndio waje wote.
Tukaenda mpaka pale mlangoni Mke wangu akashangaa sana hata baada ya kuingia ndani alishangaa zaidi huku akiomboleza vitu vyake vingi kupotea.
Sikutaka kumwambia kuhusu kuwakamata wale vibaka sikutaka kutengeneza jalada la maswali na majibu maana kwanza kichwani sikuwa sawa na huwa sipendi sana mazungumzo muda mwingi.
Hata napokuwa na washikaji zangu mara nyingi wao ndio huwa nawaachia watawale uwanja wa mazungumzo.
Tulikaa huku nikimwambia kuwa asihofu mambo yatakaa sawa kuhusu vitu nitamnunulia vingine.
Mida ya saa tisa nilitoka na kutafuta bucha inayouza nyama ya mbuzi ambapo nilipata kilo tatu nikarudi na kuichomea familia yangu ili kujipongeza maana ilikuwa kidogo tu nirudishwe kwenye umasikini.
Mimi huwa nina kaujuzi Fulani ka kuiandaa nyama na kuichoma ambapo kama nikikuchomea basi lazima utaifurahia tu.
Mida ya jioni Denis alinipigia simu niende pale kwao, nilifika akanikaribisha ndani huku akiniita “Noriega”. Hii pekee ilitosha kunipa majibu kuwa kazi inaendelea kama kawaida.
Tulizungumza mengi sana, mwishoni alinipa mzigo ule kumbe waliupeleka kwake na nikapewa ratiba ya siku tatu mfululizo. Nikaona hii ndio chance ya kujipatia maujiko yaliyoanza kupungua.
Baada ya siku tatu mzigo ulikata nikamwambia Denis anipe mzigo mwingine niunganishe sitaki kupoa nikatoka mchezoni.
Akaniambia nipunguze hasira na kazi. Nikamsisitizia kuwa sitaki kupoa akasema kuna mzigo alitaka uende mkoani lakini basi anaghairi anipe mimi nikamjibu sawa.
Kweli ramani ya kazi ilichorwa upya nikaliendeleza tena. Zilipita kama wiki tatu tena ndipo nikiwa nasubiri mzigo uje ndio niendelee na kazi Nakumbuka ilikuwa ni mida ya jioni nilipokea simu kupitia namba ngeni.
Kusikiliza vizuri sauti ni ya kike, akajitambulisha kuwa yeye ni mke wa Denis. Akanipa taarifa ambayo iliupasua sana moyo wangu na kuniacha ndani ya maswali mengi bila majibu.
Sikuwa nikijua kama Denis ana mke lakini ndio huyu kanipigia na kunipa ujumbe ambao sikuutarajia ghafla hivi.
Je ni ujumbe upi aliopewa Boyo? Usikose sehemu ya nne.
Wako katika utunzi, Sonko Bibo. +255,653-532222..