Mbegu zenyewe za asili mnajua zililetwa na nani? Au mlizikuta porini mkazivuna? Asili yetu ni mizizi, uyoga, magome ya miti na matundapori, mbegu zote mnazoita za asili zililetwa na hao mabeberu mnaowaita toka kwao, nendeni mkasome historia. Na wimbi hili halikwepeki ni walewale waliotangulia wanaendelea
Walileta mbegu, wakaleta biblia, wakaleta quran, wakatambulisha manabii zao na mandevu yao, wakatuletea na majina wote leo tuna majina ya kizungu, kiarabu au kiisraeli, wakaleta tiba, wakatufundisha kusoma, wakaleta simu, magari, mabati tujenge makanisa, shule na wakaleta hata nguo tuache kutembea uchi. So tusijitoe ufahamu na kuleta umuch know wakati hatujui hatukujua hata kutengeneza mkaa kabla hawajaja. Oh na kiberiti walituletea nilisahau na hadi leo hatujaweza kutengeneza hata njiti moja