Agenda ya Josephat Gwajima kuhusu benki ya mbegu za Asili izingatiwe

Umetoa ujumbe lakini asilimia 99% humu Hawajui hata hizo mbegu za kisasa na zaasili Kuna namna serikali inakwama Watu wanajua boda boda na Azam tv + Simba na yanga au baltazar
 
Sante Kwa mchango wako murua🙏

Mada inazidi kuchangamka.

Wenye maono, wapewe uongozi kuongoza Nchi na bara la Afrika katika kuhakikisha Dunia inakula vyakula salama.

Nia tunayo,

Uwezo tunao💪
Hamna uwezo wa kununua organics wala uwezo kuzalisha organics za kutosha hata mtaani kwenu nyie makapuku.
 
Afrika tunaweza kuilisha Dunia,

Tuna Kila kitu.
Huko duniani wamekuambia wana haja ya kulishwa na Africa? Udumavu umejaa tele kwenye nchi yako halafu unaongelea suala la kulisha dunia?!
Hizi ni akili au matope!
 
Umetoa ujumbe lakini asilimia 99% humu Hawajui hata hizo mbegu za kisasa na zaasili Kuna namna serikali inakwama Watu wanajua boda boda na Azam tv + Simba na yanga au baltazar

Mbegu zenyewe za asili mnajua zililetwa na nani? Au mlizikuta porini mkazivuna? Asili yetu ni mizizi, uyoga, magome ya miti na matundapori, mbegu zote mnazoita za asili zililetwa na hao mabeberu mnaowaita toka kwao, nendeni mkasome historia. Na wimbi hili halikwepeki ni walewale waliotangulia wanaendelea

Walileta mbegu, wakaleta biblia, wakaleta quran, wakatambulisha manabii zao na mandevu yao, wakatuletea na majina wote leo tuna majina ya kizungu, kiarabu au kiisraeli, wakaleta tiba, wakatufundisha kusoma, wakaleta simu, magari, mabati tujenge makanisa, shule na wakaleta hata nguo tuache kutembea uchi. So tusijitoe ufahamu na kuleta umuch know wakati hatujui hatukujua hata kutengeneza mkaa kabla hawajaja. Oh na kiberiti walituletea nilisahau na hadi leo hatujaweza kutengeneza hata njiti moja
 
Mbegu zenyewe za asili mnajua zililetwa na nani? Au mlizikuta porini mkazivuna?
Hawa vijana sijui hata kama wanajua hayo mahindi yenyewe yaliletwa na wazungu Wareno wala hayana asili ya Africa.
 
Kwamba hapa kuwa na miembe na mipapai, nazi za asili kabla ya ujio wa wareno na wakoloni?

Kujibu watu wa aina hii ni kupoteza muda.
 
Watakataa.
 
Kwamba hapa kuwa na miembe na mipapai, nazi za asili kabla ya ujio wa wareno na wakoloni?

Kujibu watu wa aina hii ni kupoteza muda.
Jielimishe kwanza! So mipapai na minazi na nyembe mlizikuta maporini? Au ilikuja kwa miujiza baada ya kumuomba yesu?
 
Kwamba hapa kuwa na miembe na mipapai, nazi za asili kabla ya ujio wa wareno na wakoloni?

Kujibu watu wa aina hii ni kupoteza muda.
Hizi hapa ndizo ndizi za asili ambazo mnataka tule ile tuishi miaka 900🤣
 
Zamani za kale watu walikuwa wanaishi hadi kufikia miaka 900 sababu watu walikuwa wanakula vyakula vinavyotokana na mbegu asilia zilizoumbwa na Mungu.

Sasa hivi mtu kufikia miaka 80 amejitahidi sana.
Kama haya mahindi ya asili??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…