Agenda ya kubadili Katiba si ya Rais Magufuli, ni agenda ya wapambe

Agenda ya kubadili Katiba si ya Rais Magufuli, ni agenda ya wapambe

Kwanini kama siyo ajenda ya rais kina kesy walipoongea bungeni spika akasema hiyo hoja ilete tukimaliza uchaguzi na itapita na umemsikia ndugai kama wanataka wabunge wengi wa ccm bungeni kwani kuna mambo yao wataka kuyapitisha na ulimsikia Ali hassan mwinyi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Ni haki ya Spika Ndugai kufanya hivyo na kuonyesha fikra zake, lakini si fikra za Mkuu wa nchi alishakanusha kwa kusema "hataongeza hata dakika" uamini mpaka sasa Mkuu.
 
Msitufanye wajinga.... wanachofanya hapa ni kutupa "trial balloons".
 
Thanks, Wabunge ni Watanzania kama wewe hayo ni mawazo yao na sio kusudio la Mkuu wa nchi, usijali puuzia uvumi huo.
Naona unapima uelekeo wa upepo. Siwezi puuzia. Inaonesha wazi kuwa watu waliotokea ukanda hou wanatabia hiyo.
 
AGENDA YA KUBADILI KATIBA SI YA RAIS MAGUFULI, NI AGENDA YA WAPAMBE.

Nawasalim wana JF

Nimeamua kuandika andiko hili ili kutoa ufafanuzi wa maneno na taarifa zinazosambaa mitaani, mitandaoni na viunga mbalimbali vya taifa letu kuwa Rais Magufuli ana mpango wa kubadilisha “ Katiba ili aweze kutawala milele” Hoja hii ni ya uongo, upotoshaji na iliyojaa chuki na uzandiki wa hali ya juu sana, na ni hoja ya kipambe zaidi kuliko ukweli mwenyewe, aidha huu ni uvumi wa kisiasa usio kuwa na tija kwa taifa letu na unastahili kupuuzwa kwa nguvu zote.

Rais Magufuli kila mara amekuwa akikanusha taarifa hizi kwa kusema na hapa namunukuu “ Baada ya muda wangu kuisha sitaongeza hata dakika” Je taarifa hizi za kuongeza muda zinatoka wapi au ni agenda ya nani? Bila shaka ni agenda ya wapuuzi wanaotaka kumchonganisha Mkuu wa nchi na watu wake. Rais Magufuli ni kiongozi mwema mwenye haiba ya usikivu na “Kiongozi mwenye kuheshimu Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ Aidha ni mwenye busara anayetambua umuhimu wa kuilinda na kuiheshimu katiba ya nchi.

Wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati tuache kutoa taarifa za uongo zenye uchonganishi wa rais na watu wake, Hakuna taarifa rasmi au hotuba yoyote ambayo mkuu wa nchi aliwai kusikika akisema ana mpango wa kuongeza muda wa madaraka au kubadili katiba ya nchi hakuna kabisa, lakini kwa sababu ya ukosefu wa agenda kisiasa kumekuwepo na uvumi wa kiudaku udaku juu ya dhana hiyo isiyo na mashiko ya aina yoyote.

Aidha wote wanaozusha jambo hilo hawana ushahidi wa aina yoyote isipokuwa tu wanaongozwa na mihemko, chuki na propaganda za kishamba katika kuchonganisha mtu na mtu, tujenge hoja na kuendesha siasa safi tunapokuwa majukwaani na si kuzusha wala kukashifu rais na kumsemea mambo ambayo hajawai kuyasema.

Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli amefanya makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano bila shaka wana JF wanakubaliana na mimi kuwa uchumi wa vitu na watu uliofanywa na serikali ya JPM umenoga na pengine ndio sababu ya kuanza kuzusha mambo ambayo hayana tija katika ustawi wa maendeleo ya Mtanzania wa kawaida, Nashauri wana JF tupingane na wazushi wanaomzushia rais wetu kipenzi na tushikamane kutangaza mema ya JPM.

Nawatakieni Jnne njema.

Deogratias Mutungi

0717-718619
nilipoona tu Mutungi nikajua ni walewale tu
 
1. Kutaka kuuua upinzani.
2. Kuzuia mikutano na shughuli zote za kisiasa tangu 2015
3.Mchezo wa kupitisha wabunge bila kupingwa.
4. Urafikiwake na wakina M7 na kagame ni mbinu moja wapo.

5Kujenga uwanja wa ndege Chato na Ikulu ni dalili ya kutaka kubadili ukomo wa urais na kutaka kututawala milele.

MUNGU AEPUSHIE MBALI.
 
Kwanini kama siyo ajenda ya rais kina kesy walipoongea bungeni spika akasema hiyo hoja ilete tukimaliza uchaguzi na itapita na umemsikia ndugai kama wanataka wabunge wengi wa ccm bungeni kwani kuna mambo yao wataka kuyapitisha na ulimsikia Ali hassan mwinyi

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
Hata Jiwe mwenyewe aliwahi kutamka hadharani kuwa miradi mingi alioanzisha hakuna wakuweza kuyamalizia wala kuyalinda. Alisema anaweza kuja mwingine hata hizi ndege tulizozinunua akaamua kuzipiga bei.

Hivyo basi ni wazu kuwa anataka kubaki madarakani kwa kisingizio cha kulinda ndege zake pamoja na kuendeleza miradi yake
 
Mchawi hakuambii atakuroga, ila ukiwa na jicho la tatu utaona kila ukipita kwake anachota mchanga wa nyayo zako

Hapo jua anakulia timing
Mtu kama Spika kuzungumza wazi kuwa wanangoja uchaguzi uishe ili wamuongezee Magufuli muda wa kutawala inatafakarisha sana

Ndugai atazungumzaje hayo bila kuwepo na mtu anayechagiza hayo?
 
Ili hoja yako ilete maana, na ili kuondoa hii hofu, haitoshi kwa yeye kusema tu muda wangu ukiisha nitaachia madaraka, ingependeza kama angeenda hatua moja zaidi mbele kwa kuwakemea wale wapambe wanapendeza hiyo hoja akiwemo Spika na wengineo.

Unajua matatizo mengi yanazikumbuka nchi za Afrika chanzo sio viongozi chanzo ni wapambe wao.

Hata Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alisema mara nyingine alipotaka kung'atuka mapema tu wapambe walijitokeza kumwambia Mwl using'atuke maana nchi yetu bado ni changa.

Lakini baadae akaja akagundua kwamba nchi wanayoizungumzia si Tanzania bali familia zao kwa maana hawakuwa na uhakika kama mwalimu akiondoka wao wataendelea kubaki na nafasi zao. Hiyo ndio ilikuwa hofu yao kubwa na Mwalimu hakuwachelewesha aliwaumbua live.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo hadi Raisi Mstaafu Mwinyi ni Mpambe???
Ndio ni mpambe. Tena mpambe nuksi kwani aliingia kwenye upambe ili kuwezesha mwanae apate urais wa Zanzibar.
Lakini huyo mzee atakufa uzeeni kwa aibu kwani upambe wake hautamsaidia na mwanae ataaibishwa na Wazanzibari kwa kura
 
Sio kweli Mkuu, mbona rais anakubalika kuliko wakati wote, upo nchini au nje? kama upo nje nitakutumia mchanganuo wa takwimu za uchumi wa vitu na watu.
Hatuhitaji propaganda za kwenye makaratasi wakati hali halisi tunaiona. Watumishi wana hali mbaya, miaka mitano sasa maslahi yao hayaboreshwi, wafanyabiashara wakubwa wengine wamefunga biashara zao, watanzania wakawaida wengi wamepunguzwa kazi, juzi tu hapa Total wametangaza kuondoka unadhani waliojariwa wote Tanzania nzima ni wangapi na familia zao ngapi ziliwategemea, ukija wafanyabiasahea wadogo ndio kila siku wanaumizwa na kodi za kila siku, wakulima ulija hao ndio usiongee kabisa, wastaafu na mafao kila siku wanalia. Ndio maana nilikwambia sio Watanzania wote ni wajinga kutuletea propaganda za takwimu za kupika.
 
Mkuuu umempa Magufuli sifa asizozistahili kabisa.
Magufuli kumwita msikivu sio sawa kabisa.

Magufuli aliwahi kutamka

"Mimi mtu akinishauri ndio ameharibu kabisa maana sitafanya kile anacho nishauri".
JPM.
 
AGENDA YA KUBADILI KATIBA SI YA RAIS MAGUFULI, NI AGENDA YA WAPAMBE.

Nawasalim wana JF

Nimeamua kuandika andiko hili ili kutoa ufafanuzi wa maneno na taarifa zinazosambaa mitaani, mitandaoni na viunga mbalimbali vya taifa letu kuwa Rais Magufuli ana mpango wa kubadilisha “ Katiba ili aweze kutawala milele” Hoja hii ni ya uongo, upotoshaji na iliyojaa chuki na uzandiki wa hali ya juu sana, na ni hoja ya kipambe zaidi kuliko ukweli mwenyewe, aidha huu ni uvumi wa kisiasa usio kuwa na tija kwa taifa letu na unastahili kupuuzwa kwa nguvu zote.

Rais Magufuli kila mara amekuwa akikanusha taarifa hizi kwa kusema na hapa namunukuu “ Baada ya muda wangu kuisha sitaongeza hata dakika” Je taarifa hizi za kuongeza muda zinatoka wapi au ni agenda ya nani? Bila shaka ni agenda ya wapuuzi wanaotaka kumchonganisha Mkuu wa nchi na watu wake. Rais Magufuli ni kiongozi mwema mwenye haiba ya usikivu na “Kiongozi mwenye kuheshimu Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’’ Aidha ni mwenye busara anayetambua umuhimu wa kuilinda na kuiheshimu katiba ya nchi.

Wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati tuache kutoa taarifa za uongo zenye uchonganishi wa rais na watu wake, Hakuna taarifa rasmi au hotuba yoyote ambayo mkuu wa nchi aliwai kusikika akisema ana mpango wa kuongeza muda wa madaraka au kubadili katiba ya nchi hakuna kabisa, lakini kwa sababu ya ukosefu wa agenda kisiasa kumekuwepo na uvumi wa kiudaku udaku juu ya dhana hiyo isiyo na mashiko ya aina yoyote.

Aidha wote wanaozusha jambo hilo hawana ushahidi wa aina yoyote isipokuwa tu wanaongozwa na mihemko, chuki na propaganda za kishamba katika kuchonganisha mtu na mtu, tujenge hoja na kuendesha siasa safi tunapokuwa majukwaani na si kuzusha wala kukashifu rais na kumsemea mambo ambayo hajawai kuyasema.

Myonge myongeni lakini haki yake mpeni, Rais Magufuli amefanya makubwa ndani ya kipindi cha miaka mitano bila shaka wana JF wanakubaliana na mimi kuwa uchumi wa vitu na watu uliofanywa na serikali ya JPM umenoga na pengine ndio sababu ya kuanza kuzusha mambo ambayo hayana tija katika ustawi wa maendeleo ya Mtanzania wa kawaida, Nashauri wana JF tupingane na wazushi wanaomzushia rais wetu kipenzi na tushikamane kutangaza mema ya JPM.

Nawatakieni Jnne njema.

Deogratias Mutungi

0717-718619
watanzania siyo wajinga na siyo tu ni suala la kubadili katiba ni kwamba MAGUMU akipita tena awamu hii hatoki madarakani na ndo raisi wa maisha kama M7
 
Wakati Magufuli mwenyewe hata akipinga hii mada anapinga kilaini laini tu tena kwa msimu. Jana kaongea yoooteee mpaka ya ubwabwa wa Rungwe ila la kuongeza muda aka mute!

Sisi wote hatuwezi kufanywa wajinga!
 
Back
Top Bottom