Agenda ya kubadili Katiba si ya Rais Magufuli, ni agenda ya wapambe

Kwa hiyo hadi Raisi Mstaafu Mwinyi ni Mpambe???
Wanawaona watu wote hawajui kuchanganua mambo mf Kagame alikataa kuwa hataongeza muda kipindi chake kikiisha tena mbele ya BBC.Uje ukubali huyu anayekataa mbele ya Polepole kwamba hataongeza hata dk 1 [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Tundu Lisu ataleta Katiba Ile ya Warioba...
Sidhani kama mambo ya kubadilisha katiba yanasaidia sana hasa kwa nchi zetu za kiafrika. Kenya walibadilisha katiba lakini wala haijasaidia sana maana ufisadi ndio umetamalaki zaidi. Kuna nchi hazina katiba kama Uingereza lakini ziko vizuri.
 
Wameonywa tayari, Rais hana mpango na agenda hii tumuunge mkono.
Yaani Job Ndugai, Juma Nkamia, Ally Keissy na wengine wanaopigia chapuo ndoto hiyo ni wehu? Kama chama hakijawatuma mbona hawakaripiwi na chama chao kwamba wanachokitamka hadharani ni kinyume na katiba ya chama na ile ya nchi? Mbona wanaangaliwa tu?
 
Zinapotolewa pongezi hadi kufuru wakati mwingine, watoaji huwa wametumwa au wanajua ndio anachopenda kusikia?
 
KIZAZI CHA WAKATI HUU SIO KILE KIZAZI CHAKINA STEVEN WASIRA KWAHIYO HUYO UNAEMTETE KANYA KANISANI NA MSIKITINI HATA UMSAFISHE VIPI HUYO HASAFISHIKI WAUMINI WASEMA TWENDE NA LISU

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 

Eti ".....Magufuli ni mtu mwema na msikivu...."

Yaani huyu Mzee ni mtu mwema? Msikivu?

Tangu lini bwana huyu amekuwa MWEMA na MSIKIVU iwapo ametengeneza vikundi visivyo rasmi vya uhalifu na ujambazi KUDHULUMU UHAI WA WATU?? mnywa damu za watu?

Tangu lini Bwana huyu amekuwa MTU MWEMA na MSIKIVU kama haheshimu katiba na sheria za nchi?

Tangu lini na kwa indicators gani Bwana huyu akawa MTU MWEMA na MSIKIVU iwapo haheshimu utu wa mtu na watu wake?

Mnasema haya na kumpaka rangi hii kwa sababu ya uchaguzi ili achaguliwe na kuendeleza UKATILI WA KUDHULUMU UHAI WA WATU na UOVU wake siyo?

Bwana John Pombe Magufuli ni mtu MWONGO, MBUMBUMBU na MNAFIKI sana....

Kila kinachosemwa kuhusu katiba na wapambe wake anaowatuma na kuwaagiza kutenda UOVU wa kila namna kama alivyowaagiza kwa hili la katiba, basi maana yake ndivyo ITAKAVYOKUWA kama huyu mtu atashinda tena...!!

Tusidanganyane hapa. Tumedanganywa sana huko nyuma. Sasa basi, inatosha...
 
Hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya...
 
Endeleeni kujidanganya na kubebesha watu wengine mzigo wa lawama huku kwa makusudi mkuhadaa umma na kumuachia mhusika mkuu......

Yani ajenda ya kuongezewa muda sio ya rais? Unakumbuka ndugai na wapambe wengine walisema? Je unakumbuka fadhira alizopewa ndugai baada ya kusema watamlazikisha magufuli kuongeza muda?

Utasema pia musiba hatumwi na ikulu kutukana na kudharirisha watu kwa kisingizio cha Kumtetea rais?

Utasema pia kikundi cha kikabila kinachoratibiwa na gwajima na makonda kwa ajiri ya rais sio mpango wa ikulu?

Kwa taarifa yako....... Ingekua kweli wapambe ndio wanaoanzisha hayo mambo basi umgesikia kauli mzito sn ya rais juu ya mambo hayo mazito kabisa kwa mustakabali wa nchi....

#WATZSIOWAJINGA
 
Hawa wote waliobadilisha katiba, hawakuwahi kutamka kwa vinywa vyao kuwa wangependa kubadilisha katiba ili kujiongezea muda.

Kagame aliwahi kutamka kuwa hataongeza hata dakika moja lakini baadaye aliongeza kwa kisingizio kuwa siyo yeye bali ni wananchi wanaotaka katiba ibadilishwe.

Hapa kwetu, Magufuli hajawahi kutamka kuwa anataka kubadilisha katiba ili kujiongezea muda lakini watu kadhaa ndani ya chama chake wakiwemo Rais mstaafu Mwinyi, wabunge na wakuu wa mikoa wamewahi kutamka hadharani kuwa wanataka katiba ibadilishwe ili Rais Magufuli aongezewe muda.

Ili kuthibitidha kuwa yeye Rais Magufuli yupo kinyume na kauli hizo zinazoleta hamaki alistahili kutoa karipio, CCM ilitakiwa kutoa kauli ya onyo kwa wanachama wake wanaotoa kauli hizo, lakini haijawahi kutokea.

Kama CCM ina uwezo wa kuwaita, kuwahoji na kuwaonya wanachama wake waliowahi kutamka tu, 'Rais Magufuli ni mshamba', imeshindikana nini kufanya hivyo hivyo kwa wanaotoa kauli zilizo kinyume na katiba ya nchi na CCM na zinazojenga pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh kama ni mke wa mtu na kauli ile unaona itahatarisha ndoa yako lazima umnyamazishe.
sasa anayekwambia anakupenda si ndo huyohuyo wa ndani mwako? unaanzaje kumnyamazisha?
Kwa sababu wanaopenda aendelee hata baada ya 2025 hawatoki upinzani.
Ni wa ndani mwake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…