Agenda ya utekaji yawa vita ya Kenge na Ponjoro!

Agenda ya utekaji yawa vita ya Kenge na Ponjoro!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Mwanzo wa ngoma ni lele na ukisikia zindindi, zimbombo haziko mbali. Haya siyo maneno yangu bali ni maneno ya wahenga wa waswahili.

Tangu mjadala ya utekaji ushike kasi, ni wazi kumeibuka makundi mawili; Moja likiwa ni 'kundi linaloshutumu utekaji' lingine likiwa ni 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' kuwa kauli zao zimekosa staha.

Wakati malumbano haya yakiendelea, Mh. Tauhida Gallos akiwa sehemu ya 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' alilitambua 'kundi linaloshutumu utekaji' kama KENGE wa ndani na KENGE wa nje. Na leo katika mahumbiri yake, Askofu amemtambua mwanakikundi wa 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' kuwa ni PONJORO. Ni rasmi sasa haya ndio majina mapya ya makundi; yaani KENGE kwa upande mmoja, na PONJORO kwa upande mwingine.

Ingawa kwa muktadha wake, maneno ya Askofu leo, yalifanana sana na Kauli ya Rais Kikwete kwa Kagame 2013, aliposema; "Ushauri si amri. Unayohiari ya kuukubali au kuukataa. Mtu muungwana husema: ‘Siukubali ushauri wako.’ Hakuna haja ya kutumia matusi au maneno yasiyofaa."

Tofauti na msimamo aliouchukua Rais Kikwete kwa kusema; "Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake." Mwelekeo wa msimamo wa Askofu ni kuwa; "Niguse nikuchanechane na viwembe"

Dalili ya mvua ni mawingu. Kwa hali ya joto la mjadala huu lilivyo kwa sasa, tunasubiri kuona majibu ya walioitwa Ponjoro, ili mtetezi wa Kenge akiwashe. Wenzetu wa betting watatupa odds za huu mpambano wa KENGE na PONJORO utakavyohitimishwa.

Nakumbuka katika mtihani wangu wa Taifa wa darasa la saba 2002, kulikuwa na swali la kumalizia methali iliyosema "Aliye kando ...." jibu lake likawa "haangukiwi na mti." Ya Rabbi nafsi yangu, Kwenye hii vita acha nibaki kuwa mpenzi mtazamaji, huenda nitapata la kujifunza.
 
Mwanzo wa ngoma ni lele na ukisikia zindindi, zimbombo haziko mbali. Haya siyo maneno yangu bali ni maneno ya wahenga wa waswahili.

Tangu mjadala ya utekaji ushike kasi, ni wazi kumeibuka makundi mawili; Moja likiwa ni 'kundi linaloshutumu utekaji' lingine likiwa ni 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' kuwa kauli zao zimekosa staha.

Wakati malumbano haya yakiendelea, Mh. Tauhida Gallos akiwa sehemu ya 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' alilitambua 'kundi linaloshutumu utekaji' kama
KENGE wa ndani na KENGE wa nje. Na leo katika mahumbiri yake, Askofu amemtambua mwanakikundi wa 'kundi linalowashutumu wanaoshutumu utekaji' kuwa ni PONJORO. Hii majina mapya ya makundi haya; yaani KENGE kwa upande mmoja, na PONJORO kwa upande mwingine.

Ingawa kwa muktadha wake, maneno ya Askofu leo, yalifanana sana na Kauli ya Rais Kikwete kwa Kagame 2013, ambapo alisema; "Ushauri si amri. Unayohiari ya kuukubali au kuukataa. Mtu muungwana husema: ‘Siukubali ushauri wako.’ Hakuna haja ya kutumia matusi au maneno yasiyofaa."

Tofauti na msimamo aliouchukua Rais Kikwete kwa kusema; "Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake." Mwelekeo wa msimamo wa Askofu ni kuwa; "mkimwaga mboga, namwaga ugali"

Mwanzo wa mvua ni mawingu. Kwa hali ya joto la mjadala huu lilivyo kwa sasa, tunasubiri kuona majibu ya walioitwa Ponjoro, ili mtetezi wa Kenge akiwashe. Wenzetu waqa hii ya betting watatupa odds za huu mpambanofa wa KENGE na PONJORO utakavyohitimishwa.che

Nakumbuka katika mtihani wangu wa Taifa wa darasa la saba 2002, kulikuwa na swali la kumalizia methali iliyosema "Aliye kando ...." jibu lake likawa "haangukiwi na mti." Ya Rabbi nafsi yangu, Kwenye hii vita acha nibaki kuwa mpenzi mtazamaji, huenda nitapata la kujifunza.
Kwa hii ya ponjoro hata CCM wenyewe wanacheka
 
Back
Top Bottom