Agent anahitajika wa kuuza unga wa sembe

Bigeso JMR

Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
14
Reaction score
2
Ndugu wapenzi wa JamiiForum Salaam zenu!
Mimi naprocess na kupaki unga safi wa sembe na dona kutoka jijini Mbeya kwa jina la MBEYA FOOD. Unga ni Mzuri sana wadau.
Kwa sasa nahitaji maajent wanaoweza kuuza huo unga jijini Dar es salaam. Nitakuletea huo unga hadi dukani / ofsini kwako ila unatakiwa kununua kuanzia nusu tani ambayo inaghalimu sh 475,000 na kwa mahitaji ya Dar nahisi utauza ndani ya siku tatu mpaka nne unakuwa umemaliza huo mzigo.
Unaweza kupiga 0783566761 kwa mawasiliano zaidi au Email: mbeyafood@bmmarketing.co.tz
 

Attachments

  • mbeya.jpg
    36.7 KB · Views: 722
Wamesema tusile unga, sijui ugali tutasonga na nini? Je ni kipi special ktk huo unga wako.
 

hapo kwenye red unatoa proof ipi
 
fanya research mwenyewe hii sio siasa ni biashara sawa

Mbona mkali sana

450,000 ni hela nyingi kwa kundi ulilo li target. Hivyo toa maelezo ya kina

au uza mwenyewe huo unga wako kama ni rahisi kiasi hicho.
 
Mbona mkali sana

450,000 ni hela nyingi kwa kundi ulilo li target. Hivyo toa maelezo ya kina

au uza mwenyewe huo unga wako kama ni rahisi kiasi hicho.
lengo ni kutengeneza ajira kwa vijana ambao mnaona 450,000 ni hela kubwa
 
Nkastuka, nkajua mambo ya kina binti kiziwi na Jack Cliff
 
Mbona unausifia sana huo unga?! au una video ndani yke?!
Hata ule unga mwingine hausifiwagi ivo.
 

Ni ushauri tu:
Pata muda u research kidogo ufahamu bei ya sembe dar kwa sasa ni pesa ngapi,mara ya mwisho kama mwezi hivi uliopita kiroba cha 25kg kilikua kinauzwa kwa 19000.
Ukifanya hesabu utagundua kwa kilo ni 760.
Nimejaribu kufanya hesabu kwa hio sembe yako mpaka inamfikia customer wako itagharimu 950/kg.
Nakushauri kwa bei hio tafuta segment nyingine ila kwa dar hilo haliwezekani,vinginevyo fuatilia kwanza ujue kama kutokana na hili sakata la umeme kupanda labda na sembe itakua imepanda.
 
kwa Dar kuna aina nyingi za sembe maana kuna hata sembe ya sh 500 kwa kilo kwa hiyo inategemea quality na aina ya watu kwa eneo husika kwa mfano kwa Dar unaweza pata chumba cha kulala kuanzia sh 2000 hadi hata laki tano kwa siku so be careful with your research, sio kwamba ndo nataka kuanza kuleta sembe Dar kwa Mara ya kwanza no ipo sokoni kwa bei tajwa usiwakatishe tamaaa wenzako.
 
Mkuu kwa uzoefu ni ngumu sana kutoa sembe mbeya kuleta dar, ushindani wa soko ni mkubwa sana, kifupi ni bora ufanyie production dar, soko la sembe la dar ni lakujuwana halafu sio cash inakwenda kwa mkopo hadi iuzwe ndio upewe chako, wafanyabiashara wa dar, wanatumia mizani mbili ipo ya kununuliya mahindi kutoka kwa wakulima na i[po ya kuuzia sembe wakati wanafanya packing, piya wanatumia ujanja wa kukata vumbe kwa kila gunia la kilo 1oo may be wanakata kg 1 hadi 2 halafu wanatoa kg 1 ya mfuko ukijumlisha kwa wastani mkulima anaebiwa kg5 ambazo ni sh 2000/= ndio maana bei za sembe zipo chini dsm, huwezi shindana nao kirahisi
 
Mbeya Sembe
Wazo zuri, ila fafanua vizuri juu ya aina ya ajenti unayemkusudia. Jaribu vilevile kuwa na uvumilivu kwa maoni tofauti tofauti toka kwa memba wa hapa!

Kwa mfano bandiko no:14 linatoa picha fulani ya ujanja unaotumika hapo Dar, sijui kama unalijua hilo.. aidha kuna bandiko no: 12 lina taarifa nzuri, licha ya wewe kulijibu kijuu juu tu!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna tofauti ya kufanyia production Dar na Mbeya maana itakulazimu kusafirisha raw materials mahindi ambapo utakuwa hujapunguza chochote, unga unasafirishwa mpaka Zambia ww unazungumzia Mbeya mpaka Dar? alafu ishu ya kujuana sio issue sana, tiyari unga upo sokoni hapo Dar mm nahitaji maajent zaidi. Too much business research and analysis huwezi fanya chochote utaishiwa kuajiriwa tu. Wajasiliamali hatufanyi hivyo!
 
Hongera kwakuwa unajuwa kila kitu mbeya sembe, mimi nina kama machines changu manzese nitakuja mbeya unifundishe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tumia akili ya kawaida tu kaka (panadol za mbeya ) aina ya mahindi mbeya songea, rukwa na iringa zikikobolewa zinatoa unga mchache ukilinganisha na mahindi ya dodoma, tani kumi za mahindi ya dodoma zinatoa unga mwingi kulinganisha na tani 10 za mbeya mahindi ya mbeya yanatoa pumba nyingi yakikobolewa pumba inazidi na soko la dsm limeshikwa na mahindi ya dodoma vitu kg 25 ya sembe super nzuri hazidi 19500/= na kg 50/=39000/- hizo ndio bei za soko,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…