Explainer
JF-Expert Member
- Dec 16, 2015
- 517
- 506
Habari wana JF, nafahamu fika kuwa hapa ndio nyumbani kwa ma great thinker.
Mara nyingi zaidi nimekuwa nikipendelea kutembelea majukwaa mawili tu hapa JF nayo ni Jamii intelligence na lile la habari na hoja mchanganyiko, lakini mara nyingi sikupendelea sana kuandika mada mbalimbali.
Hii ilitokana na ukweli kwamba JF ilijitosheleza sana katika kila sekta, nadhani wenye ufahamu mtakuwa mnanielewa hapa.
Tukiachana na hayo, maana nisije KUINGILIANA na misingi na maamuzi ya watu yaliyokwisha jengeka humu, Mimi leo napenda tushirikishane jambo moja tu muhimu.
Unaweza tamka "The making of scruptor" (usilemae tafuta mwenyewe maana yake) tafadhali kilichoandikwa kwenye mabano sio maana yake. Kabla hatujazungumzia zaidi kuhusu habari ya Agents and the making of scruptor ningependa kutoa wazo kwa msomaji kuwa umakini wako katika kusoma habari hii ndio utakaokusaidia kung'amua chochote kile, ila kama utakuwa na mambo mengi sana, hapa utaambulia patupu. Pia kutokana na muda na ukubwa wa habari hii, kutakuwa na mgawanyiko wa sehemu tatu kuu ili usichoke kusoma.
Utangulizi
Msomaji chunga sana mienendo yako. Kama utashindwa kujichunga basi jaribu kuwa na uwezo mzuri wa kumbukumbu, hii itasaidia kujiweka sawa katika nafasi zile ulizoshindwa kujichunga mwanzoni. Nielewe hapa.
"Siku moja nikiwa katika mgahawa mmoja mdogo tu, nadhani kwa wakazi wa hapa nyumbani TZ hasa wale wenye maisha ya kawaida ndio kimbilio letu huko kwa kina mama ntilie, wakati nikiwa napata chai pale mala ghafla wakaja wateja wengine watatu, wateja hawa watatu walikuwa ni vijana wa lika ya kati wenye asili ya kimasai, kwa ufupi walikuwa ni wamasai haswaaaa.
Wakati tukiendelea na huduma nilihisi kitu toka kwao, maana baada ya salamu na kuagizia chakula wao waliendelea kuzungumza kwa kimasai tu muda wote, lakini kwa maono yangu niligundua walikuwa wakiniongelea mimi wazi wazi, na kwa mawazo yao mafupi walizani kwa kuwa sisi sio wamasai kama walivyokuwa wao basi hatutofahamu wanazungumza nini juu yangu.
Walisahau kuificha body language yao!![emoji1]. Unajua baada ya tabia zetu tuzijuazo sisi kuna tabia nyingine nyingi zaidi wazijuazo watu wengine tofauti na sisi, na mara nyingi tukitajiwa tabia hizo tunazikataa kabisa. Mfano watu wanakuona wewe ni mbinafsi, huku wewe nafsini unajiona upo sawa tu, tena watu wanakuona wewe katili na mtesaji, huku wewe unajiona mtu mwema.
Hii yote ni ukweli kabisa maana huwezi kuificha body language yako, uwezi kuificha tabia yako ya asili, na kama utajaribu kuficha chochote kukuhusu kwa sababu unauelewa kidogo kuhusiana na mambo hayo itakuchukua wiki mbili pekee kufahamika, tena haya ni makadilio makubwa sana, inaweza kuchukua saa moja, masaa 24, siku tatu, wiki moja na zaidi na zaidi kulingana na muhusika mwenyewe.
Wale Masai hawakuweza kuficha hisia za wakiongeleacho kwa lugha yao. (Mtu yeyote anaweza akaacha utambulisho wake kwa kupitia jambo lolote dogo tu, either kwa njia ya utembeaji wako, uvaaji wako, uongeaji, ulalaji na mengine mengi sana, na kati ya hayo yote hata ukiyaficha vipi yatajionesha tu maana kitu kama sio asili yako kitakutoka tu.
Utaigiza mwondoko, uvaaji, ulalaji na kila kitu ikiwa ni pamoja na uongeaji, matendo fulani hivi yasiyo asili yako...lakini mwisho wa siku asili yako ya nini kusudio lako itabaki vile vile na itajionyesha wazi wazi machoni mwa watu. Sasa hapa ndio unapotakiwa kuitumia mbinu namba mbili, mbinu ya kuwa na kumbukumbu, maana ulishashindwa kuchunga mienendo yako hapo mwanzo.
Baada ya wale Masai kuhisi nimegundua kuwa wananizungumzia mimi, kutokana na wao kuzungumza kisha kila mmoja ananiangalia, mwingine tena anarudia hivyo hivyo kisha wanaendelea tena kuzungumza, tena kana kwamba wanabishana jambo kunihusu mara nyingine wananyoosha na vidole kabisa ( Unajua muda mwingine mtu anaweza kujisahau kabisa na kisha kuanza kukutuhumu wazi wazi, anatoka katika hali ya kujificha na kuingia katika hali ya wazi pasi yeye kujitambua, hii inatokea pale pindi upande wa pili unapoitaji uthibitisho au ushahidi wa wazi, mfano halisi Battle kati ya Mr Engineer na Mr Humble African. Mara nyingi mwisho wa siku unakuja kugundua tatizo baadae sana au unaweza usigundue kabisa, na kama utagundua tatizo, basi jaribu kuwekeza katika kumbukumbu ili usijekurudia tatizo hilo)
Siku ile ilipita hivyo, wale Masai walijiona wajinga na kujiuliza ni kwanini mtu asiejua kabisa lugha yao kufahamu ni nini walikuwa wananizungumzia!! Aibu sana .
Huo ulikuwa ni utangulizi wa habari yetu hii iliyobeba kichwa cha habari cha Agents and the making of scruptor.
Agents kama lilivyo, ni neno la kigeni kwetu, tena lenye maana pana kidogo. Hapa nchini kwetu kuna maajenti wengi sana, wengi kweli kweli, natumai kila mwenye kutumia jina hilo vyema atakuwa anayajua Matunda ya kazi yake kubwa anayo fanya.
Usitishike na neno Agents, maana hawa ni mawakala tu kama walivyo wale wa tigo pesa mitaani kwetu huko, maajenti wa magodoro, usafirishaji na mambo mengine mengi sana. Msingi wa habari yangu na wale vijana wa kimasai ni mpana sana na imekuwa hivyo ili walau kuleta kueleweka kwa urahisi wa nini namaanisha katika habari hii.
Tuonane katika sehemu ya pili
Sent using Jamii Forums mobile app