GE2025 Aggrey Mwanry arejesha fomu asema hatua iliyobaki ni kumuomba Mungu

GE2025 Aggrey Mwanry arejesha fomu asema hatua iliyobaki ni kumuomba Mungu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Baada ya kurejesha rasmi fomu ya kuwania nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mmoja wa watia nia ameeleza kuwa hatua iliyobaki sasa ni kumuomba Mungu ili aweze kupata kibali cha kuteuliwa na chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la kurejesha fomu, mtia nia huyo alisema:

"Juzi tulikuja hapa kuchukua fomu, tukapata maelekezo kwamba tukazijaze kama tulivyoelekezwa na chama. Tumerudisha fomu, tumekutana na Katibu wetu wa chama, amezikagua na kuridhika. Tunamshukuru Mungu, mambo yote yamekwenda vizuri."

Pia, Soma: Aliyewahi kuwa RC Tabora, Agrey Mwanri aitaka Siha, asema Bungeni hawaendi kina Tyson

Hata hivyo, mtia nia huyo alisisitiza kuwa ni mapema mno kueleza mipango yake endapo atateuliwa, akisema:

"Kwa sasa hivi ni mapema mno kusema nimejipangaje. Siwezi kusema lolote kwa sasa. Mimi nilichojipanga ni kumuomba Mungu ili aone katika vikao hivi, na akanitazame ili niweze kuteuliwa. Iwe kama ilivyo matarajio yangu, familia yangu, pia wananchi na wanachama wenzangu."

Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM linaendelea katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini, huku wagombea wakitakiwa kufuata taratibu zote za chama kabla ya kufikishwa kwenye mchujo wa majina.

 
Back
Top Bottom