Agizo la Aweso larejesha huduma ya Maji Mbokomu

Agizo la Aweso larejesha huduma ya Maji Mbokomu

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) imetekeleza Agizo la Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso (Mb) la kuhakikisha huduma ya maji inarejea kwa wakazi wa Kata ya Mbokomu ifikapo Septemba 2, 2024.

Mamlaka imetekeleza agizo hilo kwa kuhakikisha miundombinu ya Majisafi iliyoharibiwa na mafuriko imerejeshwa. Mamlaka kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 ilitenga kiasi cha Tsh Milioni mia moja kwa ajili ya kufanya matengenezo ya miundombinu inayojumuisha bomba za maji zenye urefu wa mita 700 pamoja na ukarabati wa chanzo cha Mrusunga

Akizungumza urejeshaji wa huduma hiyo, Kaimu Mtendaji wa Kata ya Mbokomu Bibi Stella Mrema amesema wanaishukuru Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Moshi kwa jitihada za haraka kwani na sasa huduma imerejea na Wananchi wanafurahia kwani hakuna changamoto katika eneo lao.

Wananchi wa Kata ya Mbokomu walipata kadhia ya kukosa huduma kwa miezi kadhaa kutokana na mvua kubwa zilizonyesha Mkoani Kilimanjaro kuharibu miundombinu ya Majisafi.
IMG-20240907-WA0052.jpg
IMG-20240907-WA0049.jpg
 
Back
Top Bottom