Agizo la kuondoa wamachinga Kariakoo Oktoba 24, 2026 lasitishwa

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Maelekezo ya kuondolewa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) katika mitaa ya Soko la Kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, yamesitishwa. Hatua hiyo imechukuliwa kwa maelezo kuwa wafanyabiashara hao wanaandaliwa soko jipya watakalohamia katika eneo la Kigogo Sambusa, lililopo Jangwani, mara litakapokamilika.

Awali, yalikuwa yametolewa maelekezo ya kuwataka wafanyabiashara hao kuhama katika maeneo wanayofanyia biashara ifikapo Oktoba 24 mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wamachinga hao, Mwenyekiti wao, Steven Lusinde, amesema watashirikiana na Serikali na kuendelea na shughuli zao za biashara wakisubiri kukamilika kwa soko hilo.

Imeelezwa kuwa Uamuzi huo unafuatia maelekezo mapya yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 
Kariakoo na mbagala hizo ni sehemu ngumu sana kuwaondoa hao watu.
 
Hapa si inasukumwa kete wasiunge maandamano,yanayopangwa kuvutwa.
Tufikirie muwazuie hawana sehemu ya kuuza ikitokea watashindwa kuingia njian kufany vurugu
 
Maelekezo ya kuondolewa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) katika mitaa ya Soko la Kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, yamesitishwa. Hatua hiyo imechukuliwa kwa maelezo kuwa wafanyabiashara hao wanaandaliwa soko jipya watakalohamia katika eneo la Kigogo Sambusa, lililopo Jangwani, mara litakapokamilika.

View attachment 3695718
Awali, yalikuwa yametolewa maelekezo ya kuwataka wafanyabiashara hao kuhama katika maeneo wanayofanyia biashara ifikapo Oktoba 24 mwaka huu.

View attachment 3695723
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wamachinga hao, Mwenyekiti wao, Steven Lusinde, amesema watashirikiana na Serikali na kuendelea na shughuli zao za biashara wakisubiri kukamilika kwa soko hilo.

Imeelezwa kuwa Uamuzi huo unafuatia maelekezo mapya yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Maelekezo ya kuondolewa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) katika mitaa ya Soko la Kimataifa la Kariakoo, jijini Dar es Salaam, yamesitishwa. Hatua hiyo imechukuliwa kwa maelezo kuwa wafanyabiashara hao wanaandaliwa soko jipya watakalohamia katika eneo la Kigogo Sambusa, lililopo Jangwani, mara litakapokamilika.

View attachment 3695718
Awali, yalikuwa yametolewa maelekezo ya kuwataka wafanyabiashara hao kuhama katika maeneo wanayofanyia biashara ifikapo Oktoba 24 mwaka huu.

View attachment 3695723
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wamachinga hao, Mwenyekiti wao, Steven Lusinde, amesema watashirikiana na Serikali na kuendelea na shughuli zao za biashara wakisubiri kukamilika kwa soko hilo.

Imeelezwa kuwa Uamuzi huo unafuatia maelekezo mapya yaliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Nu mwendo wa kulitengeneza tatizo na kulitanzua.

Na sifa zote zimwendee yule aliyelianzisha tatizo hilo la kuwaharass wafanya biashara na sasa amelisitisha.

Tunamshukuru sana.
 
Back
Top Bottom