Lobapula
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 2,389
- 1,584
Rais SAMIA SULUHU alitoa agizo kuwa wakulima wasitozwe Ushuru wa mazao kwa magunia yasiyozidi tani moja akiwa Tabora.
Jambo la ajabu hapa Mkoa wa Rukwa wilaya Sumbawanga kuna kizuizi cha Mazao njia ya kwenda Tunduma kinaitwa Laela wananchi wanatozwa ushuru wa mazao mfano leo tarehe 24/05/2022 majira ya saa nne na nusu asubuhi wamesimamisha bus na kuanza kukagua walikuta gunia 5 za alizeti wametozwa ushuru, kuna dada alikua na gunia moja la mahindi ametozwa ushuru pia kuna kijana alikua amebeba maharage debe tatu katozwa ushuru.
Hapa tunajiuliza tamko la rais huko tabora lilikua la kufurahisha genge na watendaji wamegoma kulitekeleza na kulisimamia?? Au watendaji wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mkirikiti,Mkuu wa wilaya Sumbawanga na Mkurugenzi wa Sumbawanga Vijijini wameamua kuwaumiza wananchi kwa makusudi?
Au ndio dhana ya Kazi iendelee?