Agnes Marwa atoa projector, awataka wanafunzi wa Mwembeni kung'ara kitaifa

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
AGNES MARWA ATOA PROJECTOR, AWATAKA WANAFUNZI WA MWEMBENI KUNG'ARA KITAIFA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Mhe. Agnes Marwa, amekabidhi projector ya kufundishia pamoja na taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwembeni, akisema lengo lake ni kuunga mkono juhudi za kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni hapo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Agnes amesema anatamani kuona Shule ya Sekondari Mwembeni ikitajwa miongoni mwa shule zinazofanya vizuri kitaifa, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanategemea nidhamu, bidii na kujituma kwa wanafunzi.

"Natamani sana kuisikia Mwembeni iking'ara kitaifa. Ninyi ndiyo mtakaolibeba na kulipandisha jina la shule yenu. Kumbukeni kuwa elimu mnayoipata ni uwekezaji wa maisha yenu wenyewe, hivyo jitumeni kwa bidii ili kutimiza ndoto zenu," amesema.

Mhe. Agnes ameahidi kuendelea kushirikiana na shule hiyo kadri atakavyopata uwezo, huku akiwahimiza wanafunzi kuendelea kuenzi uzalendo na kuilinda amani ya Tanzania.

"Tuwafundishe watoto wetu uzalendo na kuipenda nchi yao. Mambo ya kisiasa yabaki kwenye siasa, lakini suala la kuilinda Tanzania ni jukumu la kila mmoja. Huwezi kuiharibu nchi yako kwa mikono yako mwenyewe halafu utegemee maendeleo," amesisitiza.

Your browser is not able to display this video.
 
well done mh.Agness 👊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…