Ibrahim300
JF-Expert Member
- Nov 29, 2010
- 390
- 68

Agness Masogange akirusha nyavu haikosi.
Wakati huu imemnasua Jux, bwanake Jack Patrick, Juma Khalid a.k.a Jux.
Kulingana na chanzo kilichowanasua wawili hao, walionekana wakitembea sako kwa bako mitaa ya Sinza Kamanyola jijini Dar.
Wawili hao walibambwa kwenye duka moja lililopo maeneo hayo baada ya Jux kutua kutoka China huku Agnes akionekana kama anayemfariji kwa tukio la Jack kunaswa na madawa ya kulevya.
Masogange alipohojiwa kuhusu uhusiano wake na Jux alidai "Wala hakuna lolote kati yangu na yeye. Mimi na wale akina Jux pamoja na dada yake ni watu wangu wa karibu sana tunaojuana muda mrefu hivyo tulikuwa tunabadilishana mawazo tu."
Jux na Jack wamekuwa wakionekana katika mitaa ya China wakila bata huku kukiwa na madai kuwa ni wapenzi na kuonekana kwa Jux na Masogange wakijiachia kumeibua maswali mengi.