GE2025 Agnesta Kaiza aahidi kuwafuta machungu Wananchi wa Segerea

GE2025 Agnesta Kaiza aahidi kuwafuta machungu Wananchi wa Segerea

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Agnesta Kaiza, ameahidi kuwafuta wananchi machungu waliyoyapata wakati wa uongozi uliopita chini ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Bonnah Kaluwa.

Akizungumza Oktoba 26,2025 katika moja ya mikutano yake ya kampeni, Kaiza amesema kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Segerea, atahakikisha analeta mabadiliko chanya na kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo.

Aidha, mgombea huyo ametoa wito kwa wakazi wa Segerea kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kutumia haki yao ya kidemokrasia kumchagua kiongozi atakayesimamia maendeleo ya kweli.

 
Back
Top Bottom