GE2025 Agnesta Kaiza: Mikopo ya Asilimia 10% ni haki yenu

GE2025 Agnesta Kaiza: Mikopo ya Asilimia 10% ni haki yenu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mtiania wa ubunge Jimbo la Segerea mkoani Dar es Salaam kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Agnesta Kaiza, ameendelea na ziara zake za vikao vya ndani ambapo Agosti 16, 2025, alikutana na wanachama pamoja na wadau katika Kata ya Vingunguti, Mtaa wa Kombo.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Kaiza ameeleza kuwa moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa eneo hilo ni namna mikopo isiyokuwa na riba inavyotolewa kwa upendeleo na baadhi ya wenye mamlaka, hali inayosababisha walengwa kushindwa kunufaika.

Ameeleza kuwa wananchi wanakosa fursa ya kupata mikopo yenye masharti nafuu, badala yake wanalazimika kukimbilia kwenye mikopo ya kinyonyaji, inayowabebesha mzigo mkubwa badala ya kuwasaidia kuondokana na changamoto za kiuchumi.

Kaiza amesisitiza kuwa ili kuondoa hali hiyo, wananchi wanapaswa kushirikiana na kuungana kwa dhati ili kuhakikisha mabadiliko ya kweli yanapatikana kupitia uchaguzi ujao, akiahidi kusimama kidete kwa maslahi ya wananchi wa Segerea iwapo atapata ridhaa ya kuwakilisha jimbo hilo bungeni.
 
Back
Top Bottom