GE2025 Agnesta: Kwa miaka kumi Segerea ni kama haikuwa na Mbunge

GE2025 Agnesta: Kwa miaka kumi Segerea ni kama haikuwa na Mbunge

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia CHAUMMA, Agnesta Kaiza, ametambua changamoto kubwa zinazowakabili wakazi wa kata ya Kisukuru ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara

Akizungumza katika muendelezo wa kampeni zake, Agnesta amesema hali hiyo imekuwa ikiathiri maisha ya wakazi hao, hasa wakinamama wanaopata taabu kubwa wakati wa kwenda kujifungua kutokana na barabara kutopitika

Ameongeza kuwa ajali za bodaboda na bajaji zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara kutokana na ubovu wa barabara za ndani ya kata hiyo

Aidha, Agnesta ameelezea kutoridhishwa kwake na michango ya mara kwa mara inayotozwa kwa wazazi katika shule za msingi na sekondari, kinyume na sera ya Serikali kuwa elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne


 
Back
Top Bottom