PreGE2025 Ahadi Hewa za CCM: Barabara Nyingi zina hali mbaya, zimechakaa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mfikirishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,418
Reaction score
13,747
ccm, Samia na machawa wenu iwafikie taarifa kuwa barabara nyingi za lami kuunganisha mikoa na wilaya zimechakaa!
Mifano michache ni barabara za Arusha mjini! Ongezea barabara kuu inayounganisha mikoa ya Manyara, Singida na Ngeza!
Kutoka Utegi kwenda Shirati kule Rorya ukirejea salama hujaumwaa mgongo unamshkuru MUNGU! Mashimo mengi utafikiri kilimo cha migomba ama sesa!
ccm, Samia na machawa wote msidanganye wananchi kwa blablablah nyingi za mama anaweza... Mama kafanya... Mama mitano tena!
Wananchi wamechoka kurubuniwa! Wanataka REFORMS!
 
Attachments

  • PXL_20250601_164551826.MP.jpg
    PXL_20250601_164551826.MP.jpg
    2.7 MB · Views: 27
  • PXL_20250601_164553308.jpg
    PXL_20250601_164553308.jpg
    1.2 MB · Views: 24
  • PXL_20250601_164604659.jpg
    PXL_20250601_164604659.jpg
    1.1 MB · Views: 25
Wanaobubujikwa na machozi walisha bubujikwa mpaka kwa wema sepetu ambaye yupo hapa JF lucas mwashamba ni stive mangere
 
Barabara nyingi za kuingia mitaani ni mbovu mbovu mbovu utadhani nchi inaongozwa na vipofu. Hii nchi tumekosea sana kwenye mipango miji hasa Dar Es salaam. Na watawala wanatumia ubovu wa hizo barabara kama mtaji wa kupata kura.

October ndo mwisho wa mama yenu, Hakuna kupewa uongozi bila reforms! Nchi irudi kwa watanganyika sasa.
 
Barabara nyingi za kuingia mitaani ni mbovu mbovu mbovu utadhani nchi inaongozwa na vipofu. Hii nchi tumekosea sana kwenye mipango miji hasa Dar Es salaam. Na watawala wanatumia ubovu wa hizo barabara kama mtaji wa kupata kura.
Ahadi hewa zisizotekelezeka! Mtu akihoji publicly anaambiwa analeta Gwajimanization!
 
Barabara ya kwenda mikoa ya kusini unaweza kutoa machozi hii barabara inaongoza TANZANIA nzima Kwa ubovu.... barabara Kwasasa haina lami ni mwendo wa tope Tu
 
ccm, Samia na machawa wenu iwafikie taarifa kuwa barabara nyingi za lami kuunganisha mikoa na wilaya zimechakaa!
Mifano michache ni barabara za Arusha mjini! Ongezea barabara kuu inayounganisha mikoa ya Manyara, Singida na Ngeza!
Kutoka Utegi kwenda Shirati kule Rorya ukirejea salama hujaumwaa mgongo unamshkuru MUNGU! Mashimo mengi utafikiri kilimo cha migomba ama sesa!
ccm, Samia na machawa wote msidanganye wananchi kwa blablablah nyingi za mama anaweza... Mama kafanya... Mama mitano tena!
Wananchi wamechoka kurubuniwa! Wanataka REFORMS!
Inasikitisha saaana
 
Mawaziri waliambiwa waibe kwa kujikadiria ilimradi wasivimbiwe 😂😂😂😂. Hizi nyimbo tutaimba wote.
MITANO TENA 😄😄😄😄😄
 
Wanaobubujikwa na machozi walisha bubujikwa mpaka kwa wema sepetu ambaye yupo hapa JF lucas mwashamba ni stive mangere
Hii mkuu ya kutajana majina siku hizi inaruhusiwa?
 
Barabara ya Bagamoyo maeneo ya Zinga Hospital,

Kuna mtu anatafuna pesa za rais samia kwa kuziba mashimo kwa kokoto na cement....! Mvua inaponysha tu, dongo lile linaondoka na panazidi kuchakaa

Hizi pesa za Samia nami naziomba jamani
 
Hivi uliona wapi eti barabara ya lami inazibwa viraka kwa moram, kokoto, sementi na udongo?
Kodi na tozo zetu wanatumbua tu kwa burudani, anasa na starehe zao wanatuachia majeraha ya viungo!
Anyways ngoja wajichumie laana... Hawato baki salama!
 
Barabara ya Bagamoyo maeneo ya Zinga Hospital,

Kuna mtu anatafuna pesa za rais samia kwa kuziba mashimo kwa kokoto na cement....! Mvua inaponysha tu, dongo lile linaondoka na panazidi kuchakaa

Hizi pesa za Samia nami naziomba jamani
Hivi uliona wapi eti barabara ya lami inazibwa viraka kwa moram, kokoto, sementi na udongo?
Kodi na tozo zetu wanatumbua tu kwa starehe zao wanatuachia majeraha ya viungo!
Laana hizi hazitowaacha salama!
 
Back
Top Bottom