It is very funny, maana hata marekani yenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote, yenye watu zaidi ya milion 300 haijaweza kufanya hayo maajabu. Nchi zilizoendelea ajira 1000 huwa hata waziri husika anatoa tamko, kwa maana ni mafinikio yasiyo kidogo.
Turudi bongo, ni kwamba baada tu ya JK kutangaza hiyo ahadi wizara ya Kapuya ikaingia kazini, Kila mwajiri alilazimika kusubmitt no ya watu alioajiri kwa mwezi regardless ni permanent, kwamkataba au kibarua. Hawa jamaa walikuwa happy kuona tu namba inaongezeka na hivyo kumfurahisha bosi. Nakumbuka one time nikiwa bongo in one of the consulting firms tulipewa kazi kwenye one of the mines. Tukaajiri watu 6 for like 6 weeks, baadae nillitwa HR dept kwa ajili ya details za hao watu. Nilipoulizwa why nikaambiwa zinatakiwa wizara ya kazi ili kujua ni ajira ngapi zimezalishwa. I told them but this is temporary wakasema hata kama ni siku moja, data need to be submitted as per maagizo ya wizara.
ISSUES:
1. Je ni ajira ngapi zimepotea katika utaratibu huo huo unaotumiwa na wizara ya kazi in these four years?
2. Nna amini kabisa hata JK haamini hizi takwimu pamoja na kwamba ni ahadi aliyotoa yeye. I am sure akibanwa kwenye 18 atairuka kama alivyoiruka ilani ya uchaguzi ya CCM.
3. Je ni indicators zipi zinasupport kuzalishwa kwa hizo ajira? It is funny kuona kwamba NSSF ambao ndiyo mfuko mkubwa wa social security na hasa kwa private firms, idadi ya member wake ni kama 500,000 tu an increase of about 60,000 kwa miaka minne. Sasa hawa waajiriwa wapya wako mifuko ipi ukizingatia mfuko kama LAPF member hawafiki hata laki mbili.
4. Hivi Kapuya na watu wake wanafahamu milioni moja maana yake ni nini wasije wakawa wanachanganya na 1000 kama ndugu zetu wa nyumba ya Gavana. Anyways kwa ufafanuzi zaidi, watu milioni ni sawa na abiria kutosha vipanya 50,000 au nchi nzima ya Botswana, au idadi ya wananchi wote mkoa wa Rukwa au Ruvuma. Ukikusanya hao waajiriwa wapya ni wengi kuliko watu wote mkoani Lindi.
5. Akina Kapuya wanweza kumegamega hizo takwimu zao at least tukajua kila wilaya zimezalishwa ajira ngapi?
6. Kapuya mwenyewe kama waziri wa kazi and in this sense the smartest in the world amezalisha ajira ngapi jimboni kwake?