Mkuu utaniwia radhi kwa kufupisha mchango wako ili niweze kuchangia kwa urahisi ila si kitu kwani bado mchango wako uko hapo juu. Mkuu umeanza kwa kuniondoa hofu kuwa Jk atakuwa salama pia sheria haiwezigusa mambo ya zamani ila mwishoni ukapata kigugumizi kama changu kwamba endapo tutapata msingi wa sheria yan katiba mpya si kuna mambo yatahojiwa kama mali za ccm zilizokuwa mali ya Serikali,pia ujue hapa kuna watu walijichukulia mali za umma. Kumbuka Molinge Sokoine kabla ya kupata ajali ambayo iliwagusa wengi,alikuwa amehaidi kuwakamata wahujumu uchumi waandamizi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa! Inaonekana dhairi kuna mali yetu walibaki nazo watu wachache ambao Sokoine alitaka awalete mbele za Pilato. Bado naamini kuwa sheria halipi fadhila,yaweza kumkuta hata aliyeipitisha,rejea A.Chenge aliyeisimamia sheria kama A.G lakini ile ile ilitaka kumweka kolokoloni kama si visenti vyake. Upande wa pili nakubali kuwa Jk kaingia moja kwa moja ktk vitabu vya historia kwa kuleta katiba mpya lakini haimaanishi kwamba kama kesi au matatizo yaliyokuwapo yanafutwa kutokana na katiba mpya,hapana ila hapa yatapewa ufumbuzi kwa ujumla wake,na ufumbuzi huu waweza kumtia wavuni uyu mkulu! Ikumbukwe nchi moja kusini mwa Tanzania ambako rais alipitisha katiba mpya iliyompelekea kuhojiwa mtangulizi wake kwa maela aliyokomba serikalini. Ila kwetu kwa jambo lililonipa wasiwasi ni kwamba mkwere anashutuma ya kuongoza kipindi cha pili kwa kulazimisha au kulazimishwa na Nec,sasa kama tatizo litapata dawa kabla ilo tatizo alija expire,pia ata mlalamikaji ajaamua kuleta lalamiko lake kwa kuwa alidai anakusanya ushaidi,si itakuwa tafrani kama akishapata ruhusa ya kuhoji kwa katiba mpya? Mi naona kuna kamba mbele ya mkwere sijui atikwepaje hapa! Naomba unipe uhakika kama katiba mpya itaweza kumfanyia hisani kwa dhambi zake kwa kuwa kaiasisi yeye. Ikumbukwe kila mtu anafurahi kwa hoja ya mkwere ya kutoa katiba tegemeo la wengi,ila je ataruka ivyo viunzi? Remember Law is inclusive and has no time limit,zipo hata kesi za mwaka 70 ambazo hadi leo zinatolewa hukumu! Nakushukuru!
Mkuu, kwanza ujue kwamba ili katiba hiyo ipate kuanza kufanya kazi ni lazima yeye JK kama rais wa wakati huu asaini maamuzi ya Bunge ili iwe sheria kamili na ianze kung'ata. Kama ataanza kuingiwa hofu na kipengele chochote hataruhusu kamba hiyo imnyonge mwenyewe. Kadhalika, anao wapambe kibao ambao lazima watauchambua mswada wa katiba mpya hiyo kujua usalama wake kuondoa vipengele ambavyo vinaweza kutumika kwa visasi. Usisahau kwamba hata kama ataipitisha, katiba hiyo mpya haitawaondoaa wateule wake aliowaweka kwenye sehemu nyeti kama mwanasheria mkuu na majaji na prosecutor. Ili kesi iwe kesi ni lazima prosecutor akubali kwamba kesi ipo na majaji wakubaliane naye. Mwanasheria mkuu wa serikali atakuwa pale kuhakikisha bosi wake haumizwi, na hivyo usitegemee kukwea ulingoni kwa ajili ya makosa ambayo JK hakuhusika moja kwa moja kama JK. Nilikuambia kwamba uraisi ni taasisi. Uchakachuaji hakufanywa na JK bali waateule wake ambao SIO MMOJA bali ni system. Utawala ni system ambayo daima inajiwekea kinga wasijerudiwa. Sio wajinga wale.
Hata hivyo vitu walivyohodhi CCM watatafuta lugha ili wapate kutopoteza uhodhi huo, wakishinikizwa sana watatoa vichache, maana mashirika mengi walishayaua kwa uroho wao kitambo kwa jina la chama kushika hatamu. Sana sana viwanja vya mpira ambavyo wanaweza kuviachia iwe mali ya serikali, ambayo mpaka hapo mtawala wa serikali hiyo atakuwa ccm wenyewe. Wakiwa bado madarakani watachakachua mali hizo hata yabaki maghofu tu ambayo itakuwa aghali kuyarudisha kwenye hali ya kawaida.
Kumbuka mifano ya karibuni ya wabunge wa CHADEMA Mbeya na Mwanza ambako wabunge wa ccm walipokataliwa na wananchi waliamua kufilisi ofisi za majimbo yao kwa visingizio kwamba samani zilizokuwamo zilinunuliwa na pesa zao kutoka mifukoni mwao wakati hata wao wanajua kwamba wananchi wanaelewaa kulikuwako pesa ambazo wabunge walipewa kuendeshea ofisi hizo. Roho ya ufilisi ni msingi wa CCM pata picha mwenyewe. Hata hizo mali zitakazoanza kupigiwa kelele kwamba ziende serikalini wanaccm watazichakachua kiasi cha kutotamanika maana ni mafundi wa kuchakachua hao na huwezi kuwashinda kwa kuongea tu.
Kaatiba mpya itaanza kuonyesha makucha yake hasa wakati wa kuingia awamu ya Tano ya utawala, waliopo sasa watatukuzwa tu,la vilaza ambao hawakuchukuwa vyao mapema ndio watakaoathirika. Kipindi hiki hujaona vingunge wa ccm wanavyojitayarishia maisha bora baada ya 2015? Miradi mingi inagawanywa kwao. Angalia Kingunge na mradi wa packing system, angalia ante plates writing wanaosema wa Masasi uliza walioko ni nani huko; vipingamizi kwao watu hao ni wale wanaoogopa ufisadi wa mchana kama kina Maghufuli ambao wanaonekana kama maadui kwa ccm conservatives ambao wanatafutiwa dawa kila kukicha.
Siamini kwamba watanzania watakengeuka na kuanza kuchokonoa mambo ya Kikwete ya zamani, maana wanaelewa kwamba hakuna msafi hata kwa watangulizi wake. Hata JKN anayo mapungufu mengi lakini ubaba wa Taifa ndio kinga pekee. Kama leo ingeruhusiwa ashitakiwe mtu yeyote mahakamani pasingetosha kwa viongozzi wote. Angalia watu walivyohamishwa kwa nguvu wakati wa operation vijiji vipya na wakapoteza mali zao na hata maisha wengine enzi za JKN, bado watu kibao wana donge na hilo. Mrema aliposhika dhahabu Airport na kusababisha atimuliwe kazi unajua zilikuwa mali za nani enzi za mzee Ruksa? Kiwira coal mine aliyeifilisi wakati wa Mr Clean ni nani? Sasa tunasumbuliwa na bei za umeme, unafikiri lili matatizo haya yalianza kubambikizwa deni la wageni wa Nskanska kama sio tangia JK akiwa waziri wa madini na nguvu ya umeme? Maukurutu ya benki kuu Kagoda enzi za Mkapa na Meremeta huoni viunganishi hapo?
Bado naamini kwamba katiba mpya kazi yake itakuwa kuziba mianya na sio kuchokonioa yaliyopita ambayo ni visasi, watanzania hatuwezi kulinganishwa na malawi na Zambia, maana JKN alijitahidi sana kutufanya kuwa wapole tunaoweza kuchunwa huku tukigugumia kimyakimya. Angalau JK na katiba mpya atazuia machafuko ambayo yalikuwa dhahir kutokea kama angeiachia ccm ishupae shingo na virakla vyake.