Ahadi ya kuajiri askari wapya wa wanyamapori itatekelezwa lini?

Ahadi ya Rais kwa waziri mkuu ,tangu mwaka 2022 lakini mpaka sasa bado hatujasikia kutekelezwa kwa kutolewa hizo ajira 6000 za majeshi ya uhifadhi kama Tanapa ,Ngorongoro Ncca ,Tawa ,Tfs ,Nk tofauti na majeshj ya wizara ya mambo ya Ndani kama polisi ,uhamiaji na magereza ambao wametoa nafasi lukuki wa vijana wazalendo was kitanzania kuajiriwa sasa wahusika lini hili litatekelezwa kabla ya bajeti mpya ya mwaka wa fedha 2023/2024 maana Mhe Rais alishakwisha Toa Tamko ila bado utekelezwaji wake umekuwa ni hafifu na kusuasua ccPindi Chana
 
Aliitoa Rais kwenda mhe waziri mkuu then waziri husika Dr chana ashughulikie lakini imekuwa ni hafifu na utekelezwaji wa kusuasua
 
Kuna uhaba mkubwa wa askari wa wanyama pori. Vituo vyao vina askari wachache na ulinzi na doria vimedorola. Matokeo udhibiti wa wawindaji haramu ni mdogo hasa mapori yanayo zungukwa na vijiji. Wasanii wanakopeshwa hela wakatunge nyimbo za kusifu CCM badala ya kuelekeza kwenye ajira, kilimo na tiba.
 
Na ndio majangili yameanza kurudi Mpaka yule Simba wa Serengeti National park "Bob junior" ameuliwa na majangili halafu hawataki kuajiri na kigezo mtu taaluma anayo mafunzo yote anayo huja ajiri kwa miaka takribani 7 halafu unasema kigezo eti miaka 25 ndio kigezo cha umri cha kuajiriwa halafu ajira zenywe ni za umma kwa nini vinawekwa vigezo kama vile ni ajira za taasis za binafsi GENTAMYCIME utusaidie mkuu kulisemea hili maana imekuwa inakatisha tamaa sana TumainiEl @Tanapa @Mchengerwa @Wizara ya Maliasili na Utalii
 
Subira yavuta kheri...
Mkuu ,bado miezi 3 bajeti ya kiserikali iishe na hao askari 6,000 ajira hazijatangazwa mpk sasa halafu pia vigezo ni dhaifu sana ..watu wako na taaluma zao na mafunzo ya umahiri wa taaluma wanayo kwa nini uwawekee ukomo wa miaka 25 kuajiriwa na wkati umri wa miaka 55-60 ni umri wa kisheria wa kustaafu hawajafikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…