Ahadi za uongo za marafiki

Ahadi za uongo za marafiki

The Spirit of Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2020
Posts
1,045
Reaction score
1,868
Amani iwe kwenu.

Ninapitia kipindi cha kuumia sana.

Hivi rafiki mnayeheshimiana akikuahidi atakusaidia kutatua tatizo lako la kipesa halafu baadae hapokei simu wala hajibu SMS zako na pesa hakusaidii kama alivyoahidi, ila unaona anaweka status tu WhatsApp huwa mnachukua hatua gani wakuu?

Jamaa yangu mmoja amenifanyia hivyo, hajui tu ameniumiza kiasi gani.
 
Kila mtu na maswaibu yake mwamba kuna wengine hawajui kukataa .Mi kuna Uncle wangu ukimwambie niazime elf 20 utasikia sawa badae kidogo uncle ,milioni 5 nayo ni hivyo hivyo utasikia nipe muda hii niweke kwenye account yako au.Lakini hatumi hata 100.
 
Nouma
 
  • Thanks
Reactions: EEX

Pitia uzi huu, utajifunza kitu. hutopata hasara.
Baadhi ya Wanawake ni Binadamu wa pekee sana, nawapa Pongezi muishi miaka mingi ya Kobe
 
Tangu nazaliwa mpaka namaliza chuo yaani mpaka leo sijawai kuomba msaada wa fedha kwa rafiki wala kumkopa,Nina marafiki wengi ila naona ni watu ninao fahamiana nao sio kama unavyochulia ...

Mi nimejitegenezea formular nikikosa basi mmekula kwangu basi hustling zangu sio za kitoto ...kwa imani yangu kuomba omba ni laana na sio vizuri ni aibu kabisa ... kuhusu kulala njaa nishalala sana kwangu sio kesi haswa kipind nipo advance nategemea wazazi wakikosa ndo basi ila sijui niombe mshkaji, dada, kaka, shangazi,mjomba ,ba mkubwa au mdogo siwezi kabisa .
 
Amani iwe kwenu.

Ninapitia kipindi cha kuumia sana.

Hivi rafiki mnayeheshimiana akikuahidi atakusaidia kutatua tatizo lako la kipesa halafu baadae hapokei simu wala hajibu SMS zako na pesa hakusaidii kama alivyoahidi, ila unaona anaweka status tu WhatsApp huwa mnachukua hatua gani wakuu?

Jamaa yangu mmoja amenifanyia hivyo, hajui tu ameniumiza kiasi gani.
Ujui magumu alokuwa nayo so ucmlaumu mzee
Tafuta msaada mwingine!!
 
Amani iwe kwenu.

Ninapitia kipindi cha kuumia sana.

Hivi rafiki mnayeheshimiana akikuahidi atakusaidia kutatua tatizo lako la kipesa halafu baadae hapokei simu wala hajibu SMS zako na pesa hakusaidii kama alivyoahidi, ila unaona anaweka status tu WhatsApp huwa mnachukua hatua gani wakuu?

Jamaa yangu mmoja amenifanyia hivyo, hajui tu ameniumiza kiasi gani.

Mkuu pole nakushauri usitegemee watu sana kwenye shida watakuvunja moyo,
PIli hamna mtu yoyote mwenye wajibu kukusaidia isipokuwa wewe na huwezi jua labda alishasaidia ila msaada wake ukageuka mwiba kwake.
Tatu ni nzuri hajakusaidia inauma lakini na wewe ingekubidi ulipe fadhila.
Na mwisho Mungu analeta watu wa namna hiyo ili ufumbue macho ujue ni watu wa namna gani.
 
Kila mtu na maswaibu yake mwamba kuna wengine hawajui kukataa .Mi kuna Uncle wangu ukimwambie niazime elf 20 utasikia sawa badae kidogo uncle ,milioni 5 nayo ni hivyo hivyo utasikia nipe muda hii niweke kwenye account yako au.Lakini hatumi hata 100.
Hahaha, nimecheka Kwa sautj, nina dada yangu nae yuko hvyo, utasikia saiz Niko mbali na vibanda vya Mpesa , ngoja nitume ata mtu akakutumie. Ukipiha cm haipokelewi tena
 
Si kwamba hataki kukusaidia ila hana uwezo huo wa kukusaidia usimchukulie vibaya
yaani mkuu alikuwa hadi ameniambia muda wa kutuma na nimpe account number,basi baada ya hapo akaacha kupokea simu,ila status zake yuko sherehe tu anaweka,na hata hilo tatizo nilimuambia,sasa kama ameona amebadili mawazo si angesema hanipi tu nikawa na amani.

nakumbuka niliwahi kumsaidia kiasi aanzishe biashara yake,na hakinilipa chote,ila nilichukulia kama rafiki na ndio kwanza alikuwa ameoa.
 
Back
Top Bottom