Ahmed Ally azidi kuwakera Yanga abandika gari lake mabango la msimamo wa Kundi A alilotoka Yanga michuano ya CAF

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC Ahmed Ally leo January 20,2025 ameamua kulipamba gari lake msimamo wa Kundi A alilotoka Yanga

SC Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na lengo la kuwakera.

Ahmed Ally amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha Watu akisema sababu ni kwamba hapa kati kulikuwa na mambo mengi na ameacha hivyo kwa muda wiki tatu hadi mwezi.

Simba SC wao wamefuzu kwenda robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakati Yanga wametolewa hatua ya makundi baada ya kumaliza nafasi ya tatu.
 
Ila ingekuwa vice versa mzee mashabiki wa simba mngetukana sana mngeanza kusema msemaji ahainge na team yake aachane na timu yenu ila kwa kuwa kafamya yeye mnaona yuko sahihi
 
Ila ingekuwa vice versa mzee mashabiki wa simba mngetukana sana mngeanza kusema msemaji ahainge na team yake aachane na timu yenu ila kwa kuwa kafamya yeye mnaona yuko sahihi
Malipo ni hapa hapa duniani. Ubaya ubwela. Nyie mliweka bango mlipomfunga Simba 5-1. Acha wanasimba tufurahi ni wakati wetu . Wanasimba ni wakati wetu huu.
 
Lina muda basi labda wafike fainali nje ya hapo wakitolewa tu robo atalipachua.

Sema pia ndo utani wa jadi hivyo sioni kama ametukosea.
 
Ni sawa, ni wakati wake kufurahi.

Ila ikifika zamu yetu ya kuweka mabango hatutaki matusi, kuweni wapole kama sisi.
 
NI UTOTO TU AKIKUA ATAACHA.
 
Ila ingekuwa vice versa mzee mashabiki wa simba mngetukana sana mngeanza kusema msemaji ahainge na team yake aachane na timu yenu ila kwa kuwa kafamya yeye mnaona yuko sahihi
Mbona mnakuwa wepesi hivi kusahau? Vipi kuhusu kero yenu ya bango/mabango ya 5-1? Malipo ni hapa hapa Bongo. Ubaya Ubwela!πŸ˜…
 
Ni sawa, ni wakati wake kufurahi.

Ila ikifika zamu yetu ya kuweka mabango hatutaki matusi, kuweni wapole kama sisi.
Kama sisi tulivyokuwa wapole kwa mabango yenu ya 5-1? Au umesahau mtani? Kutesa kwa zamu.
 
Ila ingekuwa vice versa mzee mashabiki wa simba mngetukana sana mngeanza kusema msemaji ahainge na team yake aachane na timu yenu ila kwa kuwa kafamya yeye mnaona yuko sahihi
Yale mabango ya mitaani ilikuwaje
 
TUMEFURAHI πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
#NguvuMoja 🦁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…