Ahmed Ally: Simba imepanda viwango vya ubora CAF, sasa ni ya 7

Nafasi kwenye viwango vya CAF tunaambiwa ni ukusanyaji wa alama kuanzia makundi kwenda juu kwa muda wa miaka mitano.
Hii kutoka 9 kwenda 7 kigezo nini au ni viti maalum?
Simba tayari inamisimu mitano hesabu Toka kipindi tunapigwa hamsa
 
Simba tayari inamisimu mitano hesabu Toka kipindi tunapigwa hamsa
Nilikua namaanisha mechi ya mwisho ya Simba ya kupanda viwango vya ubora ilikua dhidi ya WYDAD. Hiyo nafasi ya 9 aliipata kwa kufika ROBO baada ya hapo hakuna mechi aliyocheza ambayo ingeweza kumpandisha viwango.

Hata hivyo jibu nimeshalipata kupitia kwa hisani ya mchambuzi MBWADUKE.
Ni kwamba mwaka mpya(msimu mpya) wa CAF umeanza rasmi, hivyokuna recalculation za points.
Point za miaka miaka 5 uliopita zimeondolewa, za miaka minne uliopita zitazidishwa kwa 1 badala ya 2, na za miaka mitatu iliyopita zitazidishwa kwa 2 badala ya 3, na miaka miwili iliyopita kwa 3 badala ya 4 na mwaka mmoja uliopita (uliosha siku chache zilizopita)alama zake zitazidishwa kwa nne badala ya 5 na mwaka huu (msimu huu ulioanza siku chake zilizopita) alama zinazidishwa kwa 5, lakini kwakua hakuna mechi zilizochezwa, timu zote zimejikusanyia alama 0x5.
Kutokana na recalculation hii kuna timu ki rank zimenufaika na nyengine zimeathirika. Kialama zote zimeathirika kwa viwango tofauti.
Hata Yanga amepanda kutoka 18 mpaka 16 ingawa alama zake zimeshuka kutoka 20 mpaka 16.
 
Kuna kitu hakipo sawa juu ya kauli ya msemaji wa Simba. Sio kweli
 
Utopolo nao wana rank yao wakiwa nafasi ya 5 afirika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]jamaniiiii......

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Kwa rank ya sasa ambayo ndio itakayotumika katika mashindano ya msimu ujao ni kwamba Simba inashika nafasi ya 9 na Yanga inashika nafasi ya 18. Hiyo ya Ya Simba kushika nafasi ni 7 na Yanga nafssi ya 16 ni assumption tu ya msimamo wa msimu wa msimu wa 2023/2024 itakayotumika katika msimu wa mwaka 2024/2025 ambapo haijajulikana timu zita perform vipi Uhalisia ni kwamba Simba inashika nafasi ya tisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…