Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, ameibua ameitaka klabu ya Yanga kurejesha kiasi cha shilingi milioni 40 serikalini, akidai kuwa klabu hiyo imepokea kiasi kikubwa cha fedha kuliko idadi ya mabingwa waliyofunga katika mashindano ya kimataifa.
Hoja hiyo inakuja kufuatia jana APrili 16, 2026 ambapo klabu ya Yanga ilikabidhiwa kitita cha Shilingi Milioni 60 kama sehemu ya zawadi ya "Goli la Mama", inayotolewa kwa klabu zinazofanya vizuri na kufunga mabao kwenye mechi za ushindi katika mashindano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Ahmed Ally, mwongozo wa zawadi hiyo unatoa fedha kwa kila goli lililopatikana kwenye mechi ya ushindi pekee. Katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, Yanga imeshinda michezo miwili pekee:
Ushindi wa 1-0 dhidi ya FAR Rabat (Goli 1).
Ushindi wa 3-0 dhidi ya JS Kabylie (Mabao 3).
"Kwa mantiki hiyo, Yanga walistahili kupata Milioni 20 pekee kwa mabao manne ya ushindi, na siyo Milioni 60 waliyokabidhiwa jana," ameandika Ahmed Ally