Ahmed Rajab, Yusuf Himidi na Simba Waziri

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AHMED RAJAB, SALIM HIMIDI NA SIMBA WAZIRI

Picha ya kwanza niliyoweka hapa kaniletea rafiki yangu Mohamed Abdul Rahman kutoka Ujerumani.

Picha hii kulia ni Salim Himidi katikati ni Joachim Chisano na kushoto ni Ahmed Rajab.

Joachim Chisano alikuwa rais wa pil wa Msumbuji.

Mohamed kaniletea picha hii kwa makusudi kwani Ahmed Rajab, Salim Himidi ni kaka zetu na tumeingiliananao kwa mengi kwa miaka mingi utotoni.

Picha hii ndiyo ilinifanya niingie Maktaba nitafute picha za zamani sana za hawa kaka zangu za miaka ya mwanzoni 1960.

Picha ya chini ya hiyo alinletea yeye huyo Mohamed kiasi cha miaka miwili iliyopita alipofariki Salim Himid ikimuonyesha Salim Himidi kushoto akiwa na Ahmed Rajab katikati na Simba Waziri kulia.

Maka hiyo mimi ni mdogo sana ndiyo nakua katika mitaa ya Kariakoo na nakumbuka nilikuwa nikienda nyumbani kwao Simba Waziiri, Mtaa wa Tandamti mdogo wake sasa ni marehemu Iddi Waziri alikuwa akinionyesha picha za kaka yake Simba Waziri wakati huo mwanafunzi chuo cha kijeshi Uingereza, Sandhurst.

Nakumbuko moja ya picha ambayo niliona ni hiyo ambayo ilipigwa Trafalgar Square hapo kwenye njiwa wengi akwa na Ahmed Rajab na Salim Himidi.

Haikunipitikia wakati ule hata kwa mbali kuwa ipo siku nitasimama hapo Trafalgar Square nikiwa na Ahmed Rajab na ntapiga picha.

Nakumbuka kama jana vile nina umri wa mika 15 au zaidi kidogo na ilkuwa tukimaliza kutazama picha tunamaliza kwa kuimba nyimbo za Cliff Richard na Iddi Waziri nyimbo yake aliyokuwa akiipenda sana ilikuwa ''High Class Baby.''

Wala haikunipitikia miaka ile ya mwanzoni 1960s kuwa hawa ninaowaangalia katika picha hiyo ya Trafalgar Square nitakuja kukutananao hapa nyumbani Tanzania na Ulaya na kwengineko na watakuwa marafiki na wazungumzaji wangu wakubwa.

Picha ya juu niko na Ahmed Rajab ofisini kwake Barbican, London wakati huo alikuwa Mhariri wa Jarida, Africa Analysis.

Hawa wote watatu kaka zangu nitakuja kukutananao Ulaya, Ahmed Rajab na Simba Waziri London na Simba tukakutana tena Tehran, Iran miaka mingi sana baada ya kukutana London.

Wakati huo Smba Waziri akiwa Mwambata wa Kijeshi katika Ubalozi wa Tanzania.

Nimeweka picha hapo chini ya mwisho nikiwa na Simba Waziri Tehran.

Salim Himidi nimekutananae Tanga kwa mara ya kwanza nkajulishwa kwake na ndugu yake Mohamed Mshangama na tukawa marafiki wakubwa akawa akija Dar es Salaam ananitembelea nyumbani kwangu.

Nilimtembelea Salim Himidi Paris mwaka wa 2011 safari ambayo kwa hakika ndipo nilipomjua Salim Himidi vizuri sana.

Maisha yake yangetosha kwa Steven Spielberg kutengeneza senema ya kusisimua.

Kijana mdogo wa Kizanzibari aliyesafari ''overland,'' akivuka mipaka nchi moja baada ya nyingine hadi Cairo kisha akavuka Bahari ya Mediterranean hadi akaingia Ulaya na kufika Ufaransa akasoma vizuri.

Akarudi nyumbani akajikuta Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Comoro.

Serikali yake ikapinduliwa na mamluki kutoka Afrika Kusini wakiongozwa na Bob Denard.

Nilikuwa sichoki kumsikiliza Salim Himidi kutwa nzima tukiranda mitaa ya Paris.

Nilikwisha kumwomba kuandika kumbukumbu zake.

Hakuandika.

Moja ya picha nilzopiga na Salim Himid Paris ambayo naipenda sana ni hiyo nimeiweka chini kabisa tuko katika hoteli tunakunywa chai, sambusa na kababu.

Salim Himidi alikuwa akinambia kuwa akiwa katika hoteli hii akinywa chai na sambusa inamkumbusha Zanzibar.
Miaka imekwenda.

Picha tatu zilizobaki ikiwa utapenda kuziona ingia: https://m.facebook.com/story.php?st...W2GCkTLdqAyEbhLf7DpxXwwxEl&id=100022121633704

 
Hii yote ni matunda ya Uhuru. na Umoja ulioasisiwa na J.K.Nyerere.....
 
Hii yote ni matunda ya Uhuru. na Umoja ulioasisiwa na J.K.Nyerere.....
Vito...
Kanuni za uandishi unatumia dots 3 tu ...

Usidhani kuwa naandika ili kumdogosha Mwalimu Nyerere.

Umoja haukuasisiwa na Mwalimu Nyerere.
Mwalimu hakuwakuta watu wa Tanganyika katika mapambano.

Kawakuta wananchi wanaishi kwa amani katika sehemu zao.

Baada ya Vita Vya Maji Maji 1905 - 1907 na baada ya Waingereza kuingia Tanganyika kama watawala wapya wananchi hawakufikiria tena kunyanyua silaha.

Waingereza walikuwa watawala ''wastaarabu,'' tofauti sana na Wajerumani.

African Association ilipoanzishwa Dar es Salaam 1929 taratibu ikaenea nchi nzima kama chombo kilichowaunganisha Waafrika wote wa Tanganyika.

Mwalimu Nyerere hii ndiyo hali aliyoikuta.
Haikuwa yeye ndiye aliyeleta umoja na utulivu huu.
 
Tuwekee picha ya shujaa John Okelo (christian) aliyewakomboa waisilamu wa Zanzibar kutoka kwenye manyanyaso ya utumwa ya waisilamu wenzao wa Oman
Umekosea sana.Jina sahihi ni Fiel Marshall John Okelo,bila huyu Mwamba mpaka kesho Zanzibar ingekuwa inatawaliwa na Oman.
 
Umekosea sana.Jina sahihi ni Fiel Marshall John Okelo,bila huyu Mwamba mpaka kesho Zanzibar ingekuwa inatawaliwa na Oman.
Ngongo,
Kuna kitabu kipya kimetoka karibuni sana na kitaingia nchini si muda mrefu.

Mwandishi wa kitabu hiki Khamis Abdulla Ameir ''Maisha Yangu Miaka Minane Ndani ya Baraza la Mapinduzi Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?'' ni alipata kuwa Mjumbe wa Baraza la Mpainduzi (MBM).

Katika kitabu hiki anamtambulisha John Okello na hicho cheo chake cha ''Field Marshall'' kakiwekea ''inverted comma,'' kwa maana kuwa hakuwa na cheo hicho.

Khamis Abdulla Ameir anamweleza katika kitabu hicho kuwa Okello alikuwa fundi-mwashi na anamweleza vyema katika kitabu hiki kiasi ya kumwita ''khabithi.''

Yapo mengi Khamis Abdulla Ameir kayaeleza kuhusu John Okello.

Lakini kama unadhani kuwa John Okello alikuwa chembelelecho ''Mwamba,'' wa Mapinzuzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964, Kassim Hanga utamuitaje?

Yawezekana hujui historia ya Hanga na historia ya wengi waliofanikisha mapinduzi wala huijui kamwe historia yenyewe ya mapinduzi.

 
Tuwekee picha ya shujaa John Okelo (christian) aliyewakomboa waisilamu wa Zanzibar kutoka kwenye manyanyaso ya utumwa ya waisilamu wenzao wa Oman
Lupwelo,
Kwa uandishi wako wa namna hii kwangu inakuwa tabu kufanya majadliano ya maana.
 
ndio hivyo wale wote waliofanya mapinduzi walitimuliwa akiwemo John Okkelo
 
Okello ndio alikuwa "mastermind" na kiongozi wa mapinduzi Zanzibaar...akina Hanga walikuwa ni watekelezaji wa mipango ya Okello.
 
Okello ndio alikuwa "mastermind" na kiongozi wa mapinduzi Zanzibaar...akina Hanga walikuwa ni watekelezaji wa mipango ya Okello.
Khaswa bila huyu Mwamba hata urojo usinge lika huko Kibanda Maiti.
 
Kabisa hata Mzee wetu Mohamed Said anajua bila shujaa,Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere angekuwa anasoma elimu ahera tu.
Ngongo,
Elimu iliingia Pwani ya Afrika Mashariki pamoja na Uislam.
Waislam ndiyo watu wa kwanza kujua zle zinazoitwa 3Rs ya Reading Writing na Arithmetic.

Ishumi ameliandika hili vizuri bahati mbaya sikumbuki jina la hii paper.
Wajerumani wamefika wamewakuta Waislam wanajua kusoma na kuandika.

Kusema kuwa Nyerere...
Soma ndugu yangu.
 

Nakubaliana na wewe kabisa,walijua kusoma,kuandika na kuhesabu lakini kuanzia kuliakwenda kushoto.

Walipewa elimu hiyo na Waarabu ili iwe rahisi kutawaliwa.
 
Okello ndio alikuwa "mastermind" na kiongozi wa mapinduzi Zanzibaar...akina Hanga walikuwa ni watekelezaji wa mipango ya Okello.
Vito...
Huijui historia ya mapinduzi.

Mipango ya kuipindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte ilikuwa inaratibiwa Tanganyika na iliwekwa kambi Kipumbwi, Tanga ambako Wamakonde kutoka Shamba la Sakura walikuwa wakipewa mafunzo.

Wasimamizi wa kambi hii walikuwa Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe Regional na District Commissioner wa Tanga.

Wengine waliokuwa katika mpango huo katika kuwatafuta Wamakonde watakaovushwa kwenda Zanzibar walikuwa Victor Mkello kiongozi wa wafanyakazi wa mashamba ya mkonge na Mohamed Omari Mkwawa.

Huyu Mkwawa yeye ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamakonde usiku katika majahazi wakijifanya wavuvi na kuwafikisha Zanzibar.

Waliokuwa wanasimamia mipango hii walikuwa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.

Unaweza kusoma historia hii kwa ukamilifu katika kitabu hicho anachokionyesha Mohamed Omari Mkwawa hapo chini:

 
Nakubaliana na wewe kabisa,walijua kusoma,kuandika na kuhesabu lakini kuanzia kuliakwenda kushoto.

Walipewa elimu hiyo na Waarabu ili iwe rahisi kutawaliwa.
Ngongo,
Hapana Waarabu hawakutawala nchi yoyote.
Soma historia utajua.

Kwani kwako wewe kujua kusoma ni lazima usome Roman script?
Ukisoma hati za Kihindi au Kichina hujui kusoma?
 
Khaswa bila huyu Mwamba hata urojo usinge lika huko Kibanda Maiti.
Ngongo,
Chukueni tahadhari mnasomwa na watu wengi sana hapa.
Hamuonyeshi kuwa mna elimu ya kuweza kujadili somo hili.
 
Mkuu, lakini hao wamakonde walipofika Zanzibar,.... Waliongozwa na John Okello kwenye Mapinduzi .. . Okello ndio alikuwa front line kwenye mapambano....Halafu hicho kitabu nasikia kilipigwa marufuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…