Ahmed Rajab, Yusuf Himidi na Simba Waziri

Mkuu, lakini hao wamakonde walipofika Zanzibar,.... Waliongozwa na John Okello kwenye Mapinduzi .. . Okello ndio alikuwa front line kwenye mapambano....Halafu hicho kitabu nasikia kilipigwa marufuku.
Vito...
Ungekuwa mjanja na unataka kuelimika ingekuwa mapema ushatambua kuwa unajadiliana na mjuzi anaeifahamu vyema historia ya mapinduzi.

Usingekuwa unajifanya kujua ilhali huna moja ulijualo.

Sasa nakupa nafasi ya kuuliza maswali nikufunze historia ya mapinduzi.

Hiyo picha hapo chini niko katika ufukwe wa Kipumbwi wakati wa utafiti kuliangalia pori la mafunzo na sehemu majahazi yaliyokuwa yakiwavusha Wamakonde yalipokuwa yakiegesha nk. nk.

Unasema kitabu kilipigwa marufuku.
Kilipigwa marufuku lini ilhali hata hicho kitabu hakijafika nchini?

Kwa nini huandika mambo unayoyajua?

 
Hapo sasa tutaenda sawa,. .... nieleweshe rolle ya John Okello, Kassim Hanga kwenye mapinduzi Zanzibar?. Na kwanini Okello alifukuzwa Zanzibar?
 
Hapo sasa tutaenda sawa,. .... nieleweshe rolle ya John Okello, Kassim Hanga kwenye mapinduzi Zanzibar?. Na kwanini Okello alifukuzwa Zanzibar?
Vito...
Katika kitabu cha Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni...'' (2010) Okello anaelezwa kama mtu aliyetumika kutisha watu kupitia radio kwa kutangaza mapinduzi.

Alitakiwa kwa ile lafidhi yake ili Wazanzibari wawe na fikra vichwani mwao kuwa nchi imevamiwa.

Alivikwa blanketi kama inavyoelezwa ajione yeye ni mtu muhimu kwa kuwekwa mbele ili ikiwa patatokea lolote la mapinduzi kushindwa yeye ndiye atiwe hatiani.

Khamis Abdalla Ameir (2022) anamtaja John Okello kama mtu msumbufu aliyetaka kujitia kila mahali na kuwa bughudha akitoa maneno ya ovyo hadharani.

Hii ndiyo sababu akafukuzwa Zanzibar.
Ama kuhusu Kassim Hanga yeye nimekwisha kumueleza.
 
Mkuu, lakini hao wamakonde walipofika Zanzibar,.... Waliongozwa na John Okello kwenye Mapinduzi .. . Okello ndio alikuwa front line kwenye mapambano....Halafu hicho kitabu nasikia kilipigwa marufuku.
Kitabu kilopigwa marufuku ni 'Ukweli ni huu'
Nishamsahau muandishi
 
Kitabu kilopigwa marufuku ni 'Ukweli ni huu'
Nishamsahau muandishi
Angel,
Mwandishi ni Aman Thani na kitabu hiki alinipa nyumbani kwake Dubai mwaka wa 1999 na hakikuwa kimepigwa marufuku.
 
Kwaheri Uhuru ,Kwa heri ukoloni nacho kimepigwa marufuku.... Said Mohamedi ni ubishi tu, hapendi kusikia mambo asiyoyapenda
Vito...
Unazungumza vitu ambavyo huvijui.
''Kwaheri Ukoloni...'' hakijafungiwa na kinauzwa toka kilipoingia nchini mwaka wa wa 2010.

Kitabu hiki mimi nilikuwa Mtafiti Msaidizi wa mwandishi Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti hiki kitabu.
Mambo yapi nisiyoyapenda nisiyotaka yasemwe?

Mimi nahusika sana katika historia ya Tanzania niamini.
Wewe ndiye mbishi na mkaidi.


Dr. Harith Ghassany na mimi nyumbani kwake Muscat
 
Shukrani na pongezi za kipekee ziende kwa Mkombozi na Shujaa wetu aliyetuletea Uhuru, amani, Upendo, Umoja na Mshikamano Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
 
Jo
John Okello umemsahau
 
Wewe sio mtu wa Vitabu ndio sababu hujui hata Kitabu gani kimezuiwa au kipi hakijazuiwa
Kwaheri Uhuru ,Kwa heri ukoloni nacho kimepigwa marufuku.... Said Mohamedi ni ubishi tu, hapendi kusikia mambo asiyoyapenda
 
Shukrani na pongezi za kipekee ziende kwa Mkombozi na Shujaa wetu aliyetuletea Uhuru, amani, Upendo, Umoja na Mshikamano Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mzalendo...
Nilialikwa Zentrum Moderner Orient (ZMO) kufanya utafiti na niandike academic paper moja ambayo itabaki kwao.

Nilipangiwa pia kufanya mhadhara mmoja kisha ndiyo nifanye hayo mengine.

Mada niliyowasilisha ni: "Tanzania a Nation Without Heroes."

Baada ya mhadhara huu nikaona ukumbi mzima umesinyaa na katika maswali na majibu ubaridi uliongezeka.

Nilifahamishwa baadae kuwa hapajatokea mtu aliyehadhiri ZMO aliyeieleza historia ya Julius Nyerere namna nilivyoieleza mimi.

Kwao ilikuwa historia mpya ambayo hawakupata kuisikia hata siku moja wala kuisoma popote.

ZMO ni taasisi kubwa sana ulimwenguni katika utafiti wa historia na wanaalika wanazuoni kutoka kila pembe ya dunia kuzungumza hapo.

Niliwauliza kwani wao wanaijua historia gani?

Wakanifahamisha.

Umenikumbusha muda niliokuwa ZMO, Berlin na historia ile iliyowatia simanzi.


Ofisini ZMO, Berlin
 
Maelezo haya hayaniingii akilini.... Hahahahaaa, eti alitumika kutisha watu... Ili wakubali mapinduzi....

Na alivikwa blanketi... La utiisho!!!!

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Maelezo haya hayaniingii akilini.... Hahahahaaa, eti alitumika kutisha watu... Ili wakubali mapinduzi....

Na alivikwa blanketi... La utiisho!!!!

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Kapu...
Kuamini au kutoamini hii ni khiyari yako hakuna wa kukulazimisha.

Mimi nimeshiriki katika utafiti wa mapinduzi na nimefika hadi Kipumbwi ilipokuwa kambi ya Wamakonde na nimeshuhudia kote kulikohusishwa na mpango huo.

Nimesikiliza mahojiano baina ya Dr. Harith Ghassany na Mohamed Omari Mkwawa ambae Mzee Karume alimpa jina la Tindo wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar.

Mkwawa ndiye aliyetufikisha Kipumbwi na nyumbani kwa Victor Mkello, Nguvumali Tanga.

Huyu Mkwawa hakupata kufungua kinywa chake kwa mtafiti kabla ya Dr. Ghassany.

Nimesikiliza mahojiano ya Dr. Ghassany na Victor Mkello kuhusu Kipumbwi.

Huyu pia alikuwa kimya miaka yote.

Kuna watu hadi leo hawakubali kuwa kuna Wamakonde walivushwa kuingia Zanzibar 1961 kupigia kura ASP na 1964 kusaidia mapinduzi.

Sishangai kuwa wewe huamini haya niliyokueleza kuhusu John Okello.

Nitashangaa ikiwa utakuwa unaamini John Okello alikuwa Field Marshall.
 
Habari Mzee,
Kabla ya uhuru na hata miaka ya mwanzoni baada ya uhuru Nyerere alikuwa na uhusiano mzuri na Uingereza pia hakuwa mpingaji wa sera za kibepali, nini sababu iliyopelekea Nyerere akabadilika na kuegemea sera za ujamaa hadi kuja na Azimio la Arusha(1967)?
 
Richard...
Kibepari si kibebali.
Sina jibu la swali lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…