GE2025 Ahmed Salum achukua fomu kuomba ridhaa ya kuendelea kulitumikia Jimbo la Solwa

GE2025 Ahmed Salum achukua fomu kuomba ridhaa ya kuendelea kulitumikia Jimbo la Solwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga, Mhe. Ahmed Ally Salum, leo Juni 28, 2025, ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea tena nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
IMG_5404.jpeg

Ahmed Salum, ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa tangu mwaka 2005, ambapo mara baada ya kuchukua fomu, ameonekana mwenye furaha na matumaini makubwa ya kuendelea na dhamana hiyo ya kuwatumikia wananchi.

"Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutufikisha mpaka siku ya leo tukiwa wazima, lakini pia nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuniamini, leo nimechukua fomu kwa nia ya kugombea kwa awamu nyingine tena Ubunge katika Jimbo la Solwa, kuteuliwa kugombea ni kitu kingine, Chama kitafanya maamuzi ya nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo la Solwa", amesema Ahmed Salum.
 
Mbunge wa Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga, Mhe. Ahmed Ally Salum, leo Juni 28, 2025, ameonesha nia ya kuendelea kulitumikia jimbo hilo kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea tena nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.

Mhe. Ahmed Salum, ambaye amekuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa tangu mwaka 2005, ambapo mara baada ya kuchukua fomu, ameonekana mwenye furaha na matumaini makubwa ya kuendelea na dhamana hiyo ya kuwatumikia wananchi.

"Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kutufikisha mpaka siku ya leo tukiwa wazima, lakini pia nakishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kuniamini, leo nimechukua fomu kwa nia ya kugombea kwa awamu nyingine tena Ubunge katika Jimbo la Solwa, kuteuliwa kugombea ni kitu kingine,Chama kitafanya maamuzi ya nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo la Solwa",amesema Ahmed Salum.
SaveClip.App_513872748_1851507258728857_7112167623148144102_n.jpg
 
Back
Top Bottom