LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 866
- 1,109
Dkt. Tulia amelazimika kuahirisha shughuli za Bunge hadi Aprili 15, 2024.
Ahmed Yahya Abdul-wakil enzi za uhai wake
Mwili wa Mbunge wa Kwahani (CCM), Ahmed Yahya Abdulwakil (65) unatarajiwa kuzikwa leo Jumanne, Aprili 9, 2024 kijijini kwao Buyuni Zanzibar.
Taarifa za kifo chake zilitangazwa jana Jumatatu Aprili 8, 2024 na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kuwa kifo hicho kilichotokana na shinikizo la damu, kilitokea Zanzibar.
“Amefariki ghafla kwa shinikizo la damu. Mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho (leo) Aprili 9, 2024 kijijini kwao Buyuni Zanzibar.”
Amesema kwa mujibu wa kanuni za Uendeshaji wa Bunge ya 173 kufuatia msiba huo, leo Jumanne Aprili 9 hakuna kikao cha Bunge ili kutoa fursa ya wabunge kushiriki katika msiba huo.
Abdulwakil alizaliwa Mei 19, 1958. Enzi za uhai wake amekuwa kuwa Mwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar 2017/2020 na katika uchaguzi mkuu 2020 aligombea uvunge katika Jimbo la Kwahani na kuibuka mshindi.
Jimbo hilo awali lilikuwa linaongozwa na Dk Hussein Mwinyi ambaye mwaka 2020 alipitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea urais wa Zanzibar na kushinda.
Abdulwakil ni mbunge wa nane kufariki dunia katika Bunge la 12, kati yao watano ni wabunge wa majimbo na wawili wa viti maalumu.
Wabunge wengine waliofariki dunia ni Atashasta Nditiye (Muhambwe), Elias Kwandikwa (Ushetu), William Ole Nasha (Ngorongoro), Said Khatibu Haji (Konde), Martha Umbula na Irene Ndyamukama waliokuwa wabunge wa viti maalumu.